PICHA HAPO JUU DIAMOND AKIWA NA BEST ACCESSORY YAKE WEMA SEPETU MALKIA WA TANZANIA.
Jamani jamani hakuna kitu kilichonisikitisha kama KUONA MTU ANACHEKELEA DIAMOND ALIVYOSHINDWA, halafu huyo mtu ni mTanzania kabisa, kweli jamani mtu unaweza kua na chuki kiasi hicho, yani siku TAIFA STARS IKICHEZA FAINALI KOMBE LA DUNIA NA ITALY UTAIOMBEA ITALY ISHINDE? chuki hii yote ni kwasababu ya Wema, Diamond hata akishindwa bado Diamond sio Wema, Wema ni number one actress in Bongo na Diamond ni number one musician in Bongo, kuhusu uhusiano wao ulikua baada ya majina yao kujulikana,
kwa mliofurahia Diamond kushindwa sikieni hii
1. DIAMOND ATABAKI KUA MSANII WA KWANZA KUTOKA TANZANIA KU PERFOM KWENYE MTV AWARDS(mmenipata)
2. KITENDO CHA DIAMOND KUA NOMINATED PEKEE NI USHINDI TOSHA HII INAASHIRIA KWAMBA AFRICA INAMTAMBUA DIAMOND
3.HATA KAMA DAVIDO NDO KAMFANYA DIAMOND AJULIKANE KUMBUKA KWAMBA HATA DAVIDO HAKUZALIWA NA KUA SUPERSTAR SIKU HIYO HIYO NA YEYE ALIKUA UNDERGROUND AKANYANYULIWA AKAFIKA HAPO ALIPO HIVYO NA DIAMOND ATAFIKA TU.
4. DAVIDO NI MTOTO WA BILIONARE, DAIMOND MTOTO WA MAMA SANDRA KUTOKA TANDALE LAKINI LEO HII BET WAKO PAMOJA, MTV WAKO PAMOJA, nyie mko wapi? nani anawajua?
5. IKUMBUKWE KWAMBA HII NDO MARA YA KWANZA DIAMOND KUSHINDANIA HIZO TUZO, HATA AKISHINDWA MWAKANI ATASHINDA TU, KUNA WANAOSEMA BORA WANGEENDA WEUSI, KWANI KUNA MTU KAWASHIKA MIGUU HAO WEUSI WENU? SI WANGEENDA TU? HATA FEMI KUTI HUWA ANASHINDWA SANA GRAMMYS LAKINI HAZOMEWI BALI ANATIWA MOYO.
6. KWA WALIOTAKA ASIENDE NA WEMA, MLITAKA AENDE NA NANI, KAMA MAMA SANDRA NA DADA ESMA WAMERIDHIA WEMA AENDE HIYO YATOSHA MAONI YA WAPINZANI HAYANA MAANA.
Namalizia na haya, kuweni wazalendo, mioyo ya chuki mpaka kufikia hatua ya kumuombea mtanzania mwenzenu ashindwe maana yake ni kwamba nyie ni watu wenye uchungu sana hata maisha yenu sidhani kama yanabaraka manake chuki yenu ni FIRST CLASS. yani mpaka sasa siamini kama kuna mtanzania anaweza akasema bora Davido alivyomshinda Diamond, Diamond WILL FOREVER BE THE FIRST TANZANIAN TO PERFOME IN MTV AWARDS, kama kuna anayebisha kuhusu hilo alete picha zake akiwa anaperfom MTV.
2 comments:
Rachel hapo umenena inasikitisha sana kuona baadhi ya watanzania hawana uzalendo. Jana niliona instagram kuna mmoja star akapost kumfagilia mwanamusic wa nchi nyingine watu wakaanza kumponda kwa sana akafuta haraka na kuweka post nyingine inayomuhusu Diamond na kumfagilia. Harafu kuna wengine wanafagilia ushindi wa davino na kuandika boraa. Inasikitisha sana na inashangaza sana. Diamond ni kijana anayejituma sana sana. Anastahiri pongezi kubwa mno hapo alipofikia. Penye nia pana njia Kutokana na juhudi zake. Mwenyezi Mungu atamsaidia.
Halafu kuna kitu kingine kinasikitisha sana ni wasanii wenyewe wamusic. Hawana kusupportiana wengine wamekalia roho za chuki. Diamond alikuwa analiwakilisha taifa Jana wangeungana kumsupport lakini ndo kwanza wanapost mambo ya kufagilia wengine. Ukweli utabaki pale pale Diamond anaimba vizuri na kuwazidi wengi wao. Sisi tuliokuwa nje ya nchi ukiwa na watu wa mataifa mengine waafrika kwa wazungu hawaelewi baadhi ya maneno yaliyokuwa kwenye wimbo wa my no one. Lakini wanaupenda sana. Diamond yupo juu anastahiri pongezi nyingi mno na Mwenyezi Mungu aendelee kumbariki.
Post a Comment