Friday, June 6, 2014

KUELEKEA TUZO ZA MTV HAYA NDO MAONI YA WATU KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ SHEMEJI WA BONGO MOVIES.

                                     DIAMOND PLATINUMZ AKIWA NA MNAIGERIA DAVIDO
Kwanza kabisa wengi wanamjua Davido ni mwanamziki anayejulikana Africa nzima, japo kiumri ni katoto ka mwaka 92, baba yake ni billionea huko Nigeria, bwana inasemekana Davido kakoma kabisa na anajilaumu kwanini alikubali kushirikishwa na Diamond kwenye wimbo wa my number one, maana baada ya ile ngoma tu Diamond hashikiki tena yani umaarufu wa Diamond unakua kwa kasi kama ule wa Lupita Nyong'o, yani Davido ye alijua anamsaidia tu Diamond kwasababu ni mwanamziki mchanga anayejulikana Tanzania tu, weeeeeee kibao kimegeuka, DIAMOND NDO KAWA MPINZANI MKUU WA DAVIDO, yani unaambiwa kila kipengele anachowekwa Davido na Diamond ndani, Davido hakutegemea kumuona Diamond BET nusu apate presha alivyomuona Diamond tena wanashindania kipengele kimoja, sasa hivi SOUTH wako wote wakitoka hapo wanaongozana tena mpaka Marekani,yani Davido hivi sasa anamuogopa Diamond kuliko anavyomuogopa DBANJI, akyanaani mwacheni Diamond aitwe Diamond. ( maneno ya watu hayo sio yangu)

DIAMOND AKIWA NA PAUL OKEYE WA PSQUARE NIGERIA
Paul ni mmoja wa wanaounda kundi la muziki la Psquare yuko yeye na pacha wake Peter, bwana kipindi hii picha inapigwa ilikua ni kwenye harusi ya pacha mwenzie huko Nigeria kwa bahati nzuri Diamond alikuwepo pande hizo basi naona akapewa kadi na Davido ili ahudhurie bila hiyana kijana akaenda na kupiga picha na Paul, baada ya week, Paul akaja akahojiwa na EATV, akaulizwa ulipiga picha na mwanamziki mkubwa Tanzania Diamond unamjua, Paul akasema simjui na sijawahi kumsikia namjua AY tu. weeeeee UNAAMBIWA PAUL ANAJUTIA MANENO YAKE, YANI ANATAMANI ANGEUNDA USHOGA NA DIAMOND KABLA HAWAJAONDOKA TANZANIA, manake mwaka huu wenyewe tuzo za BET wanazisikia radioni lakini Diamond anashindania moja ya tuzo hizo, unaambiwa Psquare wanahaha na Diamond sasa hivi.

DIAMOND NA TIWA SAVAGE WA NIGERIA
HAPO JUU DIAMOND NA IVON CHAKACHAKA WA A.KUSINI
HAPO JUU DIAMOND NA VICTORIA KIMANI WA KENYA
DIAMOND NA IYANYA WA NIGERIA
DIAMOND SIJUI NA NANINANI WA NIGERIA
DIAMOND NA MWANAMZIKI ANAYEUZA KULIKO WOTE AFRICA DBDANJ WA NIGERIA

NA HUYU NDO DIAMOND WETU PEKE YAKE

WAPENZI TUMUWEKENI DIAMOND KWENYE MAOMBI KWANI KUPITIA YEYE TANZANIA INATANGAZWA, NAIMANI KABISA USHINDI UNAKUJA KWETU SIJUI KWANINI LAKINI MOYONI NINAAMINI KABISA KWAMBA HUU NI WAKATI WETU.
MUNGU MBARIKI KIJANA WETU.

No comments: