Friday, June 13, 2014

MKE WA MAREHEMU TYSON, MONALISA ATOA YA MOYONI LEO ASUBUHI

   MONALISA AKIWA NA MWANAE WA KWANZA SONIA ALIYEZAA NA TYSON



Leo asubuhi kupitia insta page yake mke halali wa marehemu George Tyson amewatolea uvuvi wale wanaomsema kwamba alienda kwenye msiba na kukubali kupewa pole kwa kuji[endekeza wakati yule mwanaume walishaachana nae, Monalisa amesema kwamba, hata kama Tyson alipofariki aliacha wanawake kumi, yeye atabaki kua mke halali wa Tyson kwani yeye ndie mwanamke pekee waliefunga nae ndoa tena ya kanisani, na kama mjuavyo ndoa ya kanisani ni mpaka kifo kiwatenganishe, Mona amechukizwa sana na maneno ya watu na amewataka wanaotembea na waume za watu kujua kwamba hata utembee nae vipi MWISHO WA SIKU YULE MWANAUME SI WAKO AKIUMWA AU AKIFA MKE HALALI WA NDOA NDIE ATAKAE MSIMAMIA KWA KILA KITU, Mona amesikitishwa sana na maneno hayo, pia amesema kwa wale wanaodhani Mona anazinyemelea mali za Tyson waachane na hizo fikra kwani marehemu kamuachia utajiri wa maisha ambao ni MWANAE SONIA, hivyo hizo mali za duniani huwa zinaisha na mtu akifa anaziacha kama Tyson mwenyewe alivyoziacha.


ya kwangu; Wajameni kweli dunia inamambo, hivi kila mtu anachofanya kwa walimwengu kibaya, Dada wa watu kabeba jukumu la kumlilia mumewe kwasababu anajua dini yake inasema nini juu ya ndoa ya kanisani, sasa watu hawakutaka? hivi kwanini mnafikiri Tyson hakuwaoa hao wengine mliotaka wapewe pole? ye mwenyewe marehemu alikua anajua mkewe aliyepewa na Mungu ni mmoja tu, na hivi Monalisa asingeshiriki msiba si ndo mngemtoa macho kabisa, YANI MTU KASHIRIKI MNASEMA, ASINGESHIRIKI PIA MNGEMSEMA, na hizo mali mnazozihesabia kama Mona angezitaka yeye ndo mmiliki halali kwasababu yeye ndo mwenye vyeti vya ndoa na motto wa kwanza wa marehemu ni Sonia.


JAMANI MSEMENI MTU MAVAZI, MITINDO YA NYWELE, KUJISHAUA, LAKINI MSIMSEME MTU MAUMBILE AU MSIMSEME MTU ANAPOKUA KWENYE MATATIZO KAMA MSIBA, HIVI MNAFIKIRI KILA MONALISA ANAPOFIKIRIA MWANAE HANA BABA ANAJIFIRIAJE? TUWE NA HURUMA JAMANI.

No comments: