DIAMOND AKIWA NA RAIS MAREKANI WALIPOKUTANA KWA BAHATI KWANI KILA MMOJA ALIKUA KIKAZI
Mwanamziki wetu anayepeperusha vyema bendera ya Tz Diamond alikua Marekani kwenye ziara yake ya kimziki, kwa bahati nzuri Rais wetu nae alikua marekani kikazi, basi Rais wetu kama mnavyomjua anavyopenda kusaidia wasanii akamuunganisha Diamond na manager wa mwanamziki mkubwa wa Marekani TRAY SONGZ.
kilichoniudhi ni maoni ya watu niliyoyakuta kwenye mitandao, yani watu hawana jema jamani, hebu soma
Global Publishers
- Comment by richardngeze 14 hours ago
- Wananchi wanakufa kwa Dangue yeye anakalia kuhangaika na Bongo fleva? kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Filauni!
- (jibu ) HIVI JAMANI KWA HIYO KAKA, RAIS YUKO KIKAZI HUKO BAHATI NZURI KAKUTANA NA KIJANA ANAYEJITUMA ALIYETOKA TANDALE LAKINI SASA HIVI AFRICA INAMTAMBUA, HIVI NI KOSA RAIS KUMSAIDIA HATA CHEMBE, KWA HIYO WALIVYOKUTANA ULITAKA WALE HALAFU KILA MTU ASHIKE HAMSINI ZAKE WAKATI WAKO MAREKANI NA HUKO NDO KWENYE SOKO ZURI KIMZIKI, RAIS ANGEKUA KAACHA SHUGHULI ZAKE KAENDA MAREKANI KUMSINDIKIZA DIAMOND SAWA, LAKINI WAMEKUTANA KIBAHATI HIYO DENGUE YAKO KAMA NDO RAIS KAENDA KUFANYA MCHAKATO WA DAWA JE? WATANZANIA TUWE NA JEMA HATA KIDOGO.
HII INA TIJA GANI KWA NCHI???!!!
(jibu ) HIVI MSANII KUSAIDIWA ILI ASIKIKE DUNIANI UNAULIZA INALETA TIJA GANI KWA NCHI, HIVI UNAJUA NENO KUPEPERUSHA BENDERA MAANA YAKE? ngoja nikusaidie, hii inaleta tija sana kwa nchi kwani mwanamziki atakapojulikana Duniani basi kila mtu ataijua Tanzania na itatusaidia kwa mambo mengi hasa utalii na mambo ya biashara.
Sasa huyu JK angeweka mkakati wa kuwasaidia wasanii ambao bado wanasuasua huku chini. Huyo mzee wa ngololo ameshafika hatua fulani ambayo hahitaji saaaaana sapoti ya rais wa nchi. Kuzidi kumnyanyua huyu ni kuongeza pengo kati yake na wasanii ambao bado hawajajlikana(
(jibu)Hivi unajua Diamond alijinyanyuaje? au unafikiri alitokea kwenye familia ya kitajiri masaki? Diamond alitoka Tandale nyimbo yake ya kwanza alirekodiwa kwa msaada, aliuza vyuma chakavu, aliuza mitumba, alikua mpiga picha, alipovuma kimziki hakuacha kumuheshimu mama yake na kumtegemea Mungu ndo maana leo hii Marekani anaenda kama sebuleni kwa hyo hao wasanii wako wachanga waambie waige mfano huo hakuna linaloshindikana ukiweka nia na heshima kwa waliokuzidi, wasanii wengi waliopataga mafanikio hapa Bongo walikua wanaendekeza pombe, sembe na mademu, nyumbani hawakumbuki unafikiri watafanikiwa kweli, wakilipwa hela ya shoo wanafunga bar, badala ya kuwekeza na kusonga mbele ili wafike kimataifa, waambie hao wasanii wako wajisaidie kwanza juhudi zao zionekane halafu ndo watasaidiwa KAMA ALIVYOJISAIDIA DIAMOND AKIWA ANAUZA VYUMA CHAKAVU NA SASA ANAKULA MEZA MOJA NA RAIS NDO MAANA RAIS KAONA JUHUDI ZAKE KAAMUA AMSAIDIE.
HUWA INAUMA SANA KUONA MSANII ANAYEJITAHIDI NA ALIYETOKA CHINI KIMAISHA ANAPONDWA KWA VITU VISIVYOKUA NA MAANA, HEBU KABLA HAMJAMPONDA MUANGALIENI HUYO MNAEMPONDA KATOKA WAPI NA KAHANGAIKAJE MPAKA KUFIKA HAPO, MBONA OBAMA HUWA YUKO BENET NA JAY ZEE, KIKWETE KUA BENET NA DIAMOND POVU LINAWATOKA? DIAMOND TUNAZIDI KUKUOMBEA UCHUKUE USHINDI. UNDERGROUND KAZANENI, KAMA DIAMOND NA SHILOLE WAMETOKA HATA NYIE MTAWEZA.
No comments:
Post a Comment