Thursday, June 19, 2014

DOTNATA AMKINGIA KIFUA WEMA SEPETU. INGIA USOME




MJASIRIAMALI na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ ameibuka na kusema anachukizwa na watu wenye kasumba ya kumsema vibaya mwigizaji Wema Sepetu ‘Beutiful Onyinye’, waache
Akipiga stori na paparazi wetu Dotnata alisema anakerwa sana na watu wanaokuwa na chuki na mwigizaji huyo ambaye yeye anamchukulia kama lulu katika tasnia ya uigizaji.
“Siwapendi wanaomchukia Wema ambaye mimi huwa namuona kama nyota katika sanaa, wamuache mtoto wa watu afanye kazi zake, si watafute kazi za kufanya kuliko kumuongelea mabaya,” alisema Dotnata pasipo kuwataja majina watu hao

No comments: