Saturday, June 21, 2014

RAY KIGOSI NA MAINDA KUNANI?

Mainda kama unavyomuona hapo juu ni binti mrembo muigizaji wa bongo movies, alikua na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji mwenzake anayeitwa Ray lakini hivi sasa uhusiano huo uko chali baada ya Ray kudakwa na mwanadada Chuchu Hans ambaye pia ni muigizaji, kulitokeaga maneno maneno ikisemekana Mainda ni chui na paka na chuchu na Ray hata status zao kwenye mitandao ya kijamii zikawaga zinaashiria marumbano, leo Mainda huko instagram kashuka na hii (DONT BE TOO CONFIDENT WHEN SOMEONE TELLS YOU THAT THEY LOVE YOU.......nakutaadharisha tu usije ukalia kama watu wanavyolia siku hizi) haikupita muda Ray nae akatupia maneno haya..............
                                             RAY KIGOSI NA CHUCHU HANS
maneno ya Ray hayo..(MTASEMA SANA LAKINI SISI BADO TUNAPEPEA.) Wadau hapo alikua anajibiwa Mainda au ni coincidence tu,




Safari hii kaka Ray kashikwa kashikika maana hafurukuti kabisa na kila mara amekua akipost picha akiwa na Chuchu na huwa anaelezea jinsi anavyompenda binti huyo kitu ambacho kilikua si kawaida ya Ray hapo zamani, hatukuwahi kusikia Ray akimnadi Mainda wala Johari hadharani ila siku hizi ni full kujiachia na mrembo Chuchu, ila wasiwasis ni kwamba inaonekana Ray kakolea zaidi kuliko Chuchu maana sisi waschana ndo huwa tunatabia ya kujitamba na wapenzi wetu kwenye social media  lakini kwa Ray ni kinyume, hata ukijaribu kufuatilia profile za Chuchu huwezi kukuta anaweka picha wakiwa na Ray hovyo au kuyafagilia hovyo mapenzi yao, anyway tunawaombea wadumu na wafikie kwenye hatua ya ndoa kama ni kweli wote wawili wanapendana,

No comments: