Friday, June 6, 2014

CHONDECHONDE WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL



Juzi Wema kamsindikiza my baby wake kwenda south kwenye tuzo za MTV, lakini rafiki kipenzi wa Wema Aunt Ezekiel nae pia aliunga tela kama mnavyojua marafiki kusapotiana ndo mpango mzima, Bwana, basi baada ya watatu hao kukwea pipa watu kwanza wakalalamika kwanini Aunt kaenda na yeye, wasiwasi mkubwa ukiwa ni kwamba, wawili hawa huwa hawaaminiki wanapokua pamoja hasa kwenye maswala ya mavazi, Yani hawa kuvaa SARESARE MAUA KWAO NI JAMBO LA KAWAIDA kitu ambacho hakitakiwi kwa mastar wakubwa kama hao, Sasa mashabiki wakawa wanasema yani wangejua Aunt nae anaunga tela wangemnyang'anya begi mmoja wao ili akifika huko imlazimu akanunue nguo nyingine hivyo sare sare maua iwe imesimamishwa kwa muda, kwanza kama kawaida yao wakati wanasepa wakajipangia wote wavae matshirt na cheni mbili mbili, na leo tunajua pia watakua na sare zao, ila kesho siku ya tukio CHONDE CHONDE MNAOMBWA WAREMBO WETU KILA MTU ATOKE KIVYAKE VYAKE, halafu mkishamaliza kwenye after party ndo mnaweza mkaendelea na sare sare au wakati wa kurudi..(maneno ya watu hayo)

ANYWAY, MI NAJUA KAMA WEMA NA YEYE YUKO HUKO BASI NI LAZIMA DIAMOND ARUDI NA TUZO NYUMBANI KWANI TUNAMJUA WEMA JINSI ALIVYO LINAPOKUJA SWALA LA BAHATI, KILA ANAPOTUA LAZIMA USHINDI UWE KWETU. TAIFA STARS NAO WANGEKUA WANAMUALIKA UWANJANI NAHISI KOMBE LA DUNIA TUNGECHUKUA,    TUNAWAOMBEA SANA.


No comments: