Wednesday, June 18, 2014

HAKIKA HAKUNA RAIS KAMA KIKWETE LINAPOKUJA SWALA LA KUWAINUA WASANII. SOMA ALIVYOMSIFIA DIAMOND JUZI.

              MUHESHIMIWA RAIS KIKWETE AKIWA NA SHEMEJI WA BONGO MOVIES DIAMOND



Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”


“Diamond alilitangaza taifa letu kupitia shoo hiyo na muziki wetu wa Tanzania, hivyo hatupaswi kuwa mbali na wasanii wetu kwani natambua wazi Diamond bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za BET ambazo ni tuzo kubwa sana nchini Marekani na naweza kusema kuwa hata kutambuliwa kwake kuwepo kwenye tuzo hizo nalo ni jambo la kujivunia kwani uwepo wake ni njia moja ya kulitangaza Taifa letu hata kama hatabahatika tena kuchukua tuzo hizo,”



Najaribu kuwatia sana moyo na kumwambia Diamond kuwa awe na uvumilivu kwani nimeshaanza kuonyesha njia ya kumsaidia maana juzijuzi nilimkuta Marekani na nilimkutanisha na mdau mkubwa sana wa muziki duniani ambaye ndiye alimtoa Jay z, Usher Raymond  na wasanii wengine wakubwa na nilimuomba amsaidie kumwelekeza namna anavyoweza kukua kwenye ulimwengu wa muziki”,
“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa yetu,” alisema Rais Kikwete
Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani hatapata chochote.HAYO NDO MANENO YA RAIS WETU.


                WEMA NA DIAMOND



Jamani hakuna Rais wa watu kama Kikwete, kwenye kampeni zake aliahidi kwamba atawasaidia wasanii na kweli baba ametimiza ahadi, kwanza anajitoa kushiriki kwenye misiba ya wasanii, msiba hata ukiwa wapi anaenda na yeye, pili msanii anapopata matatizo huwa anajitoa kuwasaidia mfano mzuri ni alivyookoa maisha ya mwanamziki Ray c, 
MUHESHIMIWA KIKWETE MIMI NINAVYOKUPENDA BABA YANGU, YANI HUNA MAMBO YA KIZAMANI AU YA KIZEE, UNAENDA NA WAKATI NA UNATAMBUA SANAA ILIVYO NA MCHANGO MKUBWA KWENYE NCHI. HONGERA SANA RAIS WETU KIPENZI CHA WATU.
 ila muheshimiwa aliniua alivyowataja wakina Luda na Neyo, nikasema du kumbe Rais yuko deep, hadi wakina Ludacris anawajua, tena akamsifia luda anaimba vizuri, walah ningekua na baba kama muheshimiwa ningefurahi sana.

No comments: