tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Monday, June 9, 2014
MPYA KUHUSU MUIGIZAJI LULU MICHAEL
Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe.
Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu.
Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo.
“Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.
Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”
HAYO NI MANENO YA GAZETI LA LEO, ILA KA LULU NAKO KASIRI HUWA HAKAWEKI WAZI KABISA MAMBO YAKE KWA HIYO PENGINE KUNA UKWELI AU NI UZISHI PIA, SI MNAKUMBUKA KUHUSU KANUMBA HAKUNA ALIYEDHANIA KWAMBA KA LULU KANATOKA NA MAREHEMU KANUMBA, anyway lakini mambo ya mapenzi ni mambo private kwa hiyo muhusika anamaamuzi ya kujiweka wazi au kuweka siri, si kazi yetu ni kusubiri tu movie zake tuangalie.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment