Monday, June 30, 2014

CHANZO KIKUU CHA TALAKA YA DIDA NI SHINDANO LA BIG BROTHER.........

Dida ambaye alipata umaarufu kupitia uigizaji, hivi majuzi ametengana na mumewe mtangazaji mwenzake Ezden the rocker, mengi yameandikwa juu ya kutengana kwa wawili hao lakini TANZANITEMOVIES BLOG inakupa kisa kamili cha kutengana huko,
                                DIDA NA EZDEN ENZI ZA NDOA YAO
Chanzo cha talaka ya Dida ni shindano la BIG BROTHER, inasemekana kwamba eti Dida ambaye ni mke wa mtu na mama wa motto mmoja alikua anataka kwenda kwenye shindano la big brother la mwaka huu, lakini mumewe EZDEN alikua anapinga kwa nguvu zote jambo hilo, na sababu ya mumewe kupinga ni kutokana na kwamba Dida ni mke wa mtu na big brother siku zote inalalamikiwa haina maadili ya kiafrica, hasa kwenye yale mambo ya kuonyesha watu wakiwa wanavaa,kuoga n.k kitu hicho EZDEN kama mume hakua tayari kukishuhudia, hakuwa tayari kuona mkewe akiwa anaonekana Africa nzima akivaa au kuoga, au akiwa tungi, mume yeyote wa kiafrica hawezi kuwa tayari kushuhudia jambo hilo,


                                                      DIDA NA EZDEN ENZI ZA NDOA YAO

Basi baada ya kuona mumewe hataki yeye akashiriki BIG BROTHER inasemekana DIDA aliamua kama mumewe hataki yeye ashiriki big brother BASI AMPE TARAKA YAKE. kwani hawezi kuacha ndoto zake kisa mume, kwa hyo bora BIG BROTHER KULIKO NDOA.

ni hayo tu wapenzi, haya yote nimeyapata kutoka kwenye chanzo makini, nimefanya mahojiano maalumu, hii ndio sababu kubwa kwa mujibu wa mahojiano, hayo mnayosoma magazetini hayana ukweli yakusema eti ndoa imevunjika kisa password ya simu, hawajamuhoji mtoa talaka.

2 comments:

Mlay said...

That's a real woman right there!! Big up dida

Anonymous said...

Real woman my foot msimpe mwenzenu kichwa cha ujinga kuachwa kila cku mwisho una one kana una problem