Wednesday, October 1, 2014

WEMA SEPETU TENA APEWA MANENO KUNTU NA MWANDISHI WA GAZETI....






KWAKO Miss Tanzania usiyechuja tangu mwaka 2006 hadi leo? Hongera kwa ‘ku-maintain’ ustaa wako tangu miaka hiyo hadi leo.
Ni matumaini yangu u-mzima wa afya. Ukitaka kujua afya yangu, namshukuru Mungu niko poa, naendelea kulisogeza gurudumu la maendeleo kupitia kalamu yangu.Madhumuni ya kukuandikia barua hii si tu kukujulia hali, bali pia kukukumbusha juu ya maisha yako ya kistaa.
Eee, we ni staa kwelikweli nani asiyekujua!
Kwa kipindi cha hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia juu ya mbwembwe zako na jeuri ya fedha. Ulianzia kwenye Bendi ya Skylight ukafanya kufuru, baadaye mtoto wa kike ukasababisha tena kwa Yamoto Band, kijana Aslay atakuwa kakushukuru kweli kwa mvua ya fedha uliyomwagia.
Yawezekana upo katika ‘kaligi’ ka upinzani na aliyekuwa shosti wako, Kajala Masanja ambaye naye alionesha mbwembwe za namna hiyo hivi karibuni lakini pointi ya msingi hapo ya kujiuliza, zipo nyingi kiasi cha kuzimwaga
Kila mtu anatambua kwamba fedha zinazotoka bila kuingia mwisho wake ni nini? Zitaisha.
Nakumbuka kabla haujaendesha kaligi ulikoibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya mpinzani wako Kajala, ulikuwa kimya kuonesha zilikuwa zimeanza kukata.
Sasa naona zimekutembelea kwa mara nyingine, jeuri imerudi palepale. Unamwaga fedha ili zikuzoee? Mh! Sidhani kama ni sawasawa.
Japo sina uhakika sana uwepo wa miradi yako, lakini nafikiri ukianzisha miradi kupitia fedha unazozimwaga kwa sasa zinaweza kukusaidia huko mbeleni. Starehe zipo lakini ‘kuzi-controo’ ni muhimu.
Hata katika eneo lako la kazi, mashabiki wako wamekuwa wakilalamika sana hawapati kazi mpya kutoka kwako. Kupitia fedha hizo, unaweza pia kuimarisha kampuni ya kuzalisha filamu na ukatoa filamu za kukidhi mahitaji ya mashabiki wako lukuki walioko nchi nzima


Una bahati ya kupendwa, una wafuasi wengi wanaokufuata kwa nini usiitumie vizuri nafasi hiyo kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama kipindi kile ulichokuja moto na kipindi cha In My Shoes? Hivi kiliishiaga wapi kile kipindi? Nini kilitokea?
Ninachopenda kuona kutoka kwako ni wewe kuzitumia fedha kwelikweli lakini pia ziingie kwelikweli, zaidi ya zile zinazotoka



No comments: