Wednesday, October 22, 2014

MUIGIZAJI BABY MADAHA ADHAMIRIA KUWAPANGA WANAUME KISA KIKIWA NI KUONA HAOLEWI




MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha ambaye anadaiwa kuishi kinyumba na meneja wake Mkenya, Joe Kariuki wa Kampuni ya Candy n Candy Records, ametoa mpya baada ya kudai kuwa kutokana na kusubiri kwa muda mrefu ili apate mwanaume anayefaa kwa ajili ya kumuoa bila mafanikio, sasa ameamua kuwapanga foleni bila kujali idadi yao
Akipiga stori na gazeti hili juzikati, Baby Madaha alisema amesubiri sana kuolewa lakini hajamuona mwanaume anayefaa, hivyo ameamua kuwapanga kama mafungu ya nyanya kama wao wanavyowapanga wanawake na ikitokea mmoja  ‘akamzingua’ anaachana naye na kumchukua mwingine
Mimi sasa hivi nawapanga tu wanaume maana sioni anayenioa ndiyo maana nimechukua uamuzi huu, wanaume wamezoea kutupanga sisi wanawake sasa mimi ndiyo nimewageuzia kibao nao waone utamu wake na ikitokea huyu amenizingua namuacha nahamia kwa mwingine,”alisema Baby Madaha
                                          BABY MADAHA AKIWA NA MWANAMZIKI WHYRE


                         AKIWA NA JOE




MH JAMANI HIVI HAYA MAMBO MENGINE NI YA KWELI AU GAZETI MNATAKA TU LIUZIKE, SIDHANI KAMA MSCHANA NA AKILI ZAKE ANAWEZA KUSEMA HAYO MANENO HADHARANI.

No comments: