WAKIGEUKA HAWA LAZIMA WAGEUKE NA BONGE LA SUPRISE TUANDAE MACHO
Hivi majuzi muigizaji Wema Sepetu amepost picha nyingi akiwa kwenye ndege bila kueleza anakoelekea ila amekua akionyesha mandhari ya ndani ya ndege ambapo alikaa first class, basi wapanda mabasi tukashuhudia mambo makubwa makubwa ya first class kwenye Emirates kutoka kwa Wema, ila pamoja na picha zote hizo na caption tofauti tofauti Wema hakudiriki kusema anakwenda wapi,........................naendelea kushuka kama ifuatavyooo.....
cha kustua kikawa ni marafiki wa Wema wakubwa ambao ni PETIT MAN WAKUACHE NA MARTIN KADINDA, ambao nao kwa pamoja wamepost picha wakiwa kwenye ndege hiyo hiyo nao picha zao zimebeba maelezo kibao lakini hakuna aliyetamka wanakoelekea na hata walipofika wameendelea kupost picha wakiwa maeneo mbalimbali ila hakuna aliyesema wako nchi gani basi mimi nikatoa macho kuangalia hizo picha walau nione hata kibao barabarani labda kilichoandikwa kichina ili nihisi wako china wapi, labda kilichoandika mji wowote nikatoka holaa, ..................bado story inaendelea.........................
Jana the King him self mr DIAMOND PLATNUMZ ambaye ni mchumba wa Wema na yeye kapost video kwenye page yake ya instagram inayomuonyesha anasikiliza mziki ila yuko kwenye ndege mwisho akaonekana Wema kumbe ndie aliyekua akirecord hiyo video kwa hiyo ni kwamba Wema na Diamond walikua pamoja kwenye hiyo ndege wanakwenda wapi hatujui, walianza lini safari hatujui, Diamond huwa anakawaida ya kuwaeleza mashabiki zake kila anapokwenda ila safari hii Diamond nae mdomo umewekwa plasta jamaa kimyaaa kasepa......
Hivi jamani safari gani hii wakaenda wote yani Wema, Diamond, Martin na Petit man, wameenda nchi gani na kufanya nini? HIVI MNAFIKIRIA NINACHOFIKIRIA WAJAMENI?
MIMI NAONA NDOA YA WEMA NA DIAMOND IMESHAIVA NA NAHISI HII SAFARI YA GROUPE ZIMA KWA MPIGO NI KWA AJILI YA MAANDALIZI, NASUBIRI MAPICHA TU MIE NIWARUSHIE NA PIA KWA KUA NAWAPENDA SANA HAWA WATU NAWAOMBEA SANA MAISHA MEMA.
No comments:
Post a Comment