Wednesday, October 22, 2014

KUHUSU DIDA NA EZDEN LEO..




WATANGAZAJI wawili waliokuwa wanandoa kabla ya kutengana hivi karibuni, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne, mwishoni mwa wiki walikaushiana kama watu wasiofahamiana baada ya kukutana katika hafla iliyofanyika katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam

Wawili hao walikutana wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo wa Namchukua wa Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambapo mwanaume alikuwa mshereheshaji huku mke akiwa miongoni mwa wageni waalikwa



Hata hivyo, Dida alionekana kuwa na mbwembwe zaidi huku akipiga ulabu na kuonekana kukolea kiasi cha kujiachia na kukata mauno mbele ya halaiki ya watu pasipo kujali uwepo wa mumewe huyo wa zamani, ambaye alikuwa mpole na aliondoka eneo hilo mara tu baada ya kumalizika kwa shughuli iliyompeleka



No comments: