Wednesday, October 29, 2014

SHAMSA FORD KALETA MAPINDUZI MAPYA


               SHAMSA FORD A.K.A CHAUSIKU AKIWA NA JB



Baada ya movie ya Chausiku kutoka muigizaji aliyecheza kinara anayeitwa SHAMSA FORD lakini kwenye movie alicheza kama CHAUSIKU amepata umaarufu mara mbili ya alivyokua awali, hii imefanya nione kwamba kumbe sasa wananchi hawaangalii sura wanaangalia kazi, yani ukiwa mrembo kama Kim Kardashian halafu ukacheza utombo kwenye movie hakuna atakayepoteza muda kukuangalia, sasa hivi watu wanataka mtu upige kazi kweli kweli sio kuringaringa kwenye movie, nimewapenda sana wabongo safari hii kwani hii imewapa watu motisha ya kufanya kazi kwa umakini, Shamsa alishacheza movie nyingi sana lakini hakuwa na kiwango che nyewe lakini kwenye movie ya chausiku Shamsa kaonyesha kipaji halisi bila kufake chochote kitu ambacho kimemfanya Shamsa apendwe mno na watu hivi sasa na watu wamemchukulia very serious kwenye kazi zake hivi sasa, mimi ninafuraha sana kwasababu nilikuwaga naumia ninapoona waschana wa bongo movie wanavyochululiwa kama wanajiuza tu kupitia movie wanazocheza lakini kwa mwendo huu aliounyesha Shamsa na wakina Riyama kwenye KIGODORO lazima tufike mbali na tuheshimike pia , mpaka nimefikiria kuanza kuiga, yani urembo unatakiwa uende na kupiga kazi yenye kiwango lakini urembo ukienda na upupu mtu utabaki kudharaulika kila siku.


NI HAYO TU WAPENZI NIONDOKE HUMU NDANI KESHO NARUDI TENA NA MAMBO MATAMU BYEEEEE

No comments: