Saturday, October 4, 2014

MUIGIZAJI LULU MICHAEL ATAKIWA KWA UDI NA UVUMBA NA PEDEJEE

                         MKONGO MWAMI

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima, inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu ‘Mkongo’ ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ‘kumalizana’ na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kwa gharama yoyote

Akizoza na gazeti hili ndani ya Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, Dar, mapema wiki hii, Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si vinginevyo.
“Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper, Husna mara Wema, si kweli, hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi (Kenya) kwa lengo la kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu,” alisema Mwami bila soni
Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa ndoto zake.
“Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena sana,” alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha zimemtembelea.
Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar, hakuwepo hivyo juhudi za kumpata zinaendelea
                                           
                                        LULU MICHAEL

No comments: