Sunday, October 19, 2014

WAREMBO BONGO MOVIES PIGENI CHABO KWA MWAMVITA MAKAMBA.....

                                                MWAMVITA MAKAMBA
 
Huyo hapo juu ni mwanadada mwenye heshima tele Tanzania anaitwa Mwamvita Makamba ni motto wa mzee Yusuph Makamba wa CCM, Mwamvita hajafika hata miaka 35 lakini amepata mafanikio makubwa mno katika kazi yake, yeye ni mmoja wa maboss wa juu kabisa VODACOM, .........
 
Watu wengi wamezoea kuona wanawake wengi wanaofika ngazi za juu kiasi hicho wakiwa hawajipendi kimuonekano yani wenyewe ni kazi kwa kwenda mbele mpaka wanasahu kuvaa hata heleni, kwa huyu dada ni tofauti, katuonyesha kwamba unaweza kua mtu wa kuheshimika kwenye jamii, ukawa na nyazifa kubwa kazini lakini ukawa FASHIONISTA pia, hakuna kitu kinachonivutia kwake kama swala la fashion, yani huwa namfollow ili nimuangalie jinsi anavyopigilia, ukimuona unaweza kujua labda she is a movie star from Hollywood, yani level za kina Gabriella Union,
 
Ukimuona hapo juu kavaa kigauni kizuri cheupe kiko juu ya magoti, hicho kigauni wangevaa Bongo movies actress lazima wangesemwa wako uchi unajua ni kwanini? NI KWASABABU YA JINSI WANAVYOBEHAVE, KUMBE MTU YOU CAN WEAR ANYTHING ILA TU UHAKIKISHE UNAKUA CLASSIC HAUTASIKIA MTU AKIKUSEMA, lakini ukavaa nguo fupi halafu mara unatembea mapozi ya kujibinua, mara mikao unayokaa yakimahaba niue, mara pembeni mivulana inakushikashika, mara unafakamia mipombe halafu ukilewa ndo unazidi kukaa kihasara utaachwa kutolewa kwenye gazeti vibaya, MCHEKI HAPO JUU MWAMVITA UKIMUANGALIA KILA KITU KIKO ON POINT, JINSI ANAVYOONGEA,JINSI ANAVYO KAA YANI KAMA MAMA OBAMA VILE PIA ANAWEZA KUNYUKA KIMINI LAKINI HAKUNA MTU ATAKAYELALAMIKA KWASABABU SHE IS CLASSIC,
 
sasa waschana wenzangu waigizaji kama tunataka kuheshimika ni lazima tufuate mifano kama ya dada yetu hapo juu, hatukatazwi kwenda na fashion ila tu tuwe na heshima ya mwanamke, hakuna atakayekutoa kwenye udaku front page kwamba umekaa uchi kama ukibehave vizuri, madala yake utasifiwa na kila mtu kwamba u look nice, utaalikwa kwenye sehemu mbalimbali kubwa kubwa na za heshima, utapewa ubalozi wa macampuni mbalimbali,
 
NI HAYO TU WAPENZI NGOJA NIISHIE HAPA MSIJE KUNICHUKIA BURE KWA KUTOA MAKAVU,

1 comment:

nacy wandi said...

Nimekuelewa sana wifiake