Saturday, October 25, 2014

MCHEKI MDOGO WAKE NA TONY BRAXTON KWENYE HII REALITY SHOW ALIVYO MAPEPE.



Hii hapo juu ni reality show ya mdogo wake na mwanamziki mashughuli Tony Braxton ambaye alitamba sana wakati huo na wimbo wa UN BREAK MY HEART. Mdogo wake huyo ni anaitwa TAMAR BRAXTON ni mama wa motto mmoja na ni mke waa producer maarufu na tajiri anayeitwa Vince Herbert.



                                   TAMAR BRAXTON AKIWA NA MUMEWE VINCE HERBET



Show yao hiyo huwa inaonyeshwa kwenye television ya WE ya huko Marekani kama una dstv unaweza kuiona na pia huonyeshwa kila alhamis, show inaitwa TAMAR AND VINCE. hii show imeanza mwaka juzi na jana ndo ilikua season 3 inaanza kwa hiyo hiyo video hapo juu ndo show ya jana ambayo ni season 3 episode ya kwanza kabisa, kwa amabye hauna muda wa kukaa kwenye tv kama mimi unaweza ukawa unaicheki utube kila ijumaa, manake kule wanaionyesha alhamis kwa hiyo ijumaa wanakua tayari wameiweka kwenye utube.



                                     TAMAR BRAXTON



Ndani ya hiyo show unapata nafasi ya kumuona Tamar Braxton mwenyewe ambaye yeye ni mdogo wa mwisho kuzaliwa wa Tony Braxton, mwanamama huyo ambaye anamiaka 38 na anamtoto mmoja anayeitwa Logan ni machachari ile mbaya, yani huyu Tamar ingekua ni wapa bongo basi tungesema ni mzaramo, kwanza anaongea hatari yani ukilianzisha ye analimaliza kinoma noma basi yani nianachekesha mno, yani dada zake huwa wanamkoma, mume wake mwenyewe ni anakoma yani, ila umapepe wake umekua burudani kwa watu maana show yake inazidi kupata viewers kila siku, na kizuri hasa kwenye hii show ni kwamba WHAT U SEE IS WHAT U GET, NO SCRIPTING, sio kama wakina KARDASHIAN show yao wanai edit kwa hiyo everything u see is not real fekero kwa kwenda mbele, hawa yani ukiona wametifuana basi ni mtifuano kweli yani hawakati, ndo maana sasa hivi show ya kina KARDASHIAN iko mbioni kusitishwa hakuna anayeiangalia huko Marekani watu hawataki habari za kudanganyana na ufake watu wanataka maisha halisi yaonekane.



                                TAMAR AKIWA ON STAGE





Hapo mwano Tamar na dada zake watatu walikua wanaimba kama background singers wa dada yao wa kwanza Tony, yani Tony akiimba wenyewe ndo waitikiaji, lakini Tamar akaona ntakua muitikiaji mpaka lini, sasa imefika wakati wa mimi pia kushine, basi akawashauri dada zake waanzishe reality show ya familia nzima, ambapo kipindi hicho walikua hawajulikani ila Tony tu ndo alikua anajulikana, lengo lao lilikua ni kwamba kwenye hiyo Reality show madam dada yao Tony ambaye ni maarufu atakuwepo basi lazima watu wataangalia na hapo ndo itakua nafasi ya wao kushine, basi hiyo reality show ikaanzishwa inaitwa THE BRAXTON FAMILY VALUES. show hiyo ilipoanza ambapo sasa hivi inaseason 4 basi watazamaji ndo tukawajua ndugu wa Tony Braxton akiwepo huyu mdogo wake wa mwisho ambaye ni machachari sana TAMAR BRAXTON. wakati show hii ikiendelea watu wakavutiwa zaidi na huyu mdogo wake Tony wa mwisho Tamar yani watu wakawa wamempotezea mpaka Tony , basi ndipo TAMAR alipopewa deal la kuanzisha show yake yeye na mumewe tu ambayo ndo hiyo inaitwa TAMAR AND VINCE.



  MUME WA TAMAR ANAYEITWA VINCE NA MTOTO WAO WA PEKEE LOGAN



Huyu motto wao amezaliwa mwaka jana pia alionyeshwa akiwa anazaliwa yani kuanzia mimba mpaka motto huyu anazaliwa hospitali watazamaji tulionyeshwa kwenye show yao.



HUYU NDO TONY BRAXTON MWENYEWE AMBAYE ALIIMBA un break my heart.

I wanaamini huyu ndo sababu ya ndugu zake kua maarufu kutokana na umaarufu wake, Tony ni mwanamziki classic , legend kama wakina Maria carey  na Celin Dion. yeye anawatoto wawili ila mumewe walishaachanaga, na ndie dada wa kwanza anawadogo zake watano, hapo alipo anakaribia miaka 50 au ndo anahamsini na kama sikosea maana mdogo wake wa tano ambaye ni Tamar anamiaka 38.

Weng



 NA HAWA NDO THE BRAXTON GILS, ILA WANAKAKA YAO MMOJA





Hii familia ya BRAXTON ni familia ya watoto sita ambapo Tony ndo wa kwanza halafu wa pili ni wakiume anaitwa MICHAEL, embu nikuorozeshee majina yao, kuna TONY BRAXTON, TOWANDA BRAXTON, TRACIE BRAXTON, TRINA BRAXTON, TAMAR BRAXTON NA KAKA YAO MICHAEL BRAXTON.



Familia hii Mungu amewabariki wote sauti za kuimba, yani hao wote unaowaona hapo juu ni wanaimba kama vinanda, na maisha yao yote wameishi kwa kutegemea mziki tu, wameajiriana wenyewe kwa wenyewe,

sasa hao wanadada wote wane huwa wanapelekeshwa puta na huyo mdogo wao wa mwisho TAMAR BRAXTON mpaka wanaomba poo.



MIMI HUWA NAWAFUATILIA SANA KWANI NAPENDA SANA REALITY SHOW, PIA NAMPENDA SANA TAMAR BRAXTON KWASABABU AMEKUA AKINI INSPIRE SANA KATIKA SAFARI YAKE YA MAISHA, alishakataliwa albam tano na record lebel, akaambiwa hawezi kua star kama dada yake Tony, akaambiwa hajui kuimba na nyimbo zake sio nzuri licha ya kwamba mumewe ni producer mkubwa aliyemtoa LADY GAGA na Tony Braxton kimziki na pia mumewe ni tajiri sana pia, lakini yote hayo bado TAMAR hakufanikiwa kimziki,alisota miaka kumi na tano mpaka mwaka juzi ambapo alitoa single yake ya kwanza ya LOVE AND WAR ikapendwa sna na kushika namba moja kwenye chat za mziki , baada ya hapo ni storynyingine maana kawa maarufu hivi ssasa kumpita hata dada yake TONY, TAMAR kashatoa albam moja inayoitwa love and war na imeuza vizuri sana na hivi majuzi katoa single yake mpya inaitwa LET ME KNOW kamshirikisha FUTURE na yuko mbioni kuachia albam yake ya pili.......





UNAWEZA KUJIULIZA KWANINI NIMEWAWEKA HAWA WAKATI SIO WAIGIZAJI, MIMI NAWAWEKA HUMU WAIGIZAJI NA PIA YOYOTE MWENYE REALITY SHOW NAWAWEKA KWASABABU REALITY SHOW NI BURUDANI KAMA YA MOVIE TU ILA TOFAUTI INAKUA PALE HAWAIGIZI KILA KITU NI REAL.



niko hoi hapa mh uhandishi kazi kweli maaana kuwaandikia hii story mpaka jasho limenitoka embu nisepe mie ntarudi baadae kidogo ngoja ninywe maji .

No comments: