Wednesday, October 22, 2014

DIAMOND PLUTNUMZ NA LUPITA NYONG'O WASANII PEKEE WA EAST AFRICA WANAOJULIKANA KIMATAIFA




Kwanza kabisa hiyo picha sijui kwanini, anyway, mi bado naendelea kuumia toka tukio la huyu kijana kuzomewa , bado sioni kosa lake ni nini, nachoumia zaidi ni jinsi alivyotoka kwenye maisha ya shida na kuamua kufanya kazi kwa bidii ili ajikwamue halafu watu wanaona wivu na kutaka kumshusha, DIAMOND SIKU ZOTE nimekua nikijifunza vitu vingi kwake, vingi mno, kwanza kila ninapojitahidi kufanya kitu kikawa kigumu huwa naangalia mfano kwa Diamond halafu najipa moyo then nasonga mbele, huwa nasema kama Diamond aliyekulia kwenye shida namna ile kapambana mpaka Dunia inamsikia kwanini mimi nishindwe, kila nikiona anafanikiwa nawazaga kumbe jambo Fulani linawezekana mbona Diamond kaweza, kwa hyo amekua mfano mkubwa na ananipa chachu sana ya maendeleo, wasanii wengine wa mziki walikua hawanipi chachu maana nilikua sioni kitu kipya kwao zaidi ya nyimbo mpya, lakini kwa Diamond sio nyimbo mpya tu bali ni hatua anazopiga kila siku kuelekea kimataifa hizo ndo zilizokua zinanipa changamoto,

SIKU ZOTE DIAMOND NA LUPITA NYONG'O ndo nimekua nikiwaangalia kwa ukaribu na wananipa moyo kwamba ipo siku nitafika, kwamba kumbe kufika mbali mpaka dunia ikutambue haijalishi umetokea Nigeria au Marekani kwamba hata East Africa pia unaweza kufanya juhudi ukatambulika duniani.

NA KWA HARAKA HARAKA HIVI NI WASANII GANI WANAOJULIKANA SANA KUTOKA EAST AFRICA, JIBU NI LUPITA NA DIAMOND PLUTNUMZ. kijana tunapiga goti kukuombea kwasababu umetumotivate sana kwenye maisha yetu ya kila siku.

                                     LUPITA NYONG'O

1 comment:

Anonymous said...

Mh wapo wasanii kbao wanaong'ara n kujulikana ila we sema unampenda huyo diamond lazma akubaliane n challenge kha so kisa ye yupo juu now basi wasanii wengne wasje juu et anapgwa vita loh n hapo wa kulaumiwa n hao mashabik n sio Ali kiba nyie watu wa media n blogs n magazet ndo mnakuza bifu kwa hela gan alznazo huyo kiba ndo alipe watu wazomee loh