tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Friday, October 31, 2014
MUIGIZAJI AUNT EZEKIEL ADAIWA KUINGIA MITINI NA CHENI YA WATU YA SHILINGI MILIONI SITA
NYOTA wa sinema Bongo, Aunty Ezekiel ameingia matatani na maafande wa Kituo cha Polisi Pangani, Ilala jijini Dar akidaiwa kutokomea na cheni ya Shabani Limo yenye thamani ya shilingi milioni 6
Kwa mujibu wa chanzo, mwishoni mwa Februari, mwaka huu, Aunty alikwenda kwa Shabani na kuazima cheni hiyo kwa makubaliano ya kuirejesha baada ya muda jambo ambalo hakulifanya na baadaye, Septemba mwaka huu, akasafiri kwenda Marekani kutangaza utalii wa ndani.
Baada ya kurejea, Oktoba mwaka huu, Shabani alimkomalia Aunty na kufikishana Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar ambapo staa huyo alisema na yeye alimwazima cheni hiyo rafiki yake aitwaye Neema.
Ilidaiwa kuwa, Neema baada ya kubanwa alikiri na kusema aliiweka bondi cheni hiyo na hapo ndipo danadana zilipoanza hivyo jamaa akaamua kwenda kufungua madai mengine Kituo cha Polisi Pangani.
Jumatano iliyopita, mapaparazi wetu walifunga safari mpaka kituoni hapo ambapo baadhi ya askari walikiri kuwepo kwa kesi hiyo lakini waligoma kutoa namba za kumbukumbu za jalada ‘RB’ wakidai mwenye uwezo huo ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova
Ni kweli hapa kuna hiyo kesi na ilianzia Oysterbay japo hatuwezi kuitolea maelezo ya kina kwa vile jambo lenyewe limekaa kimapenzi zaidi,” alisema askari mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Shabani alipotafutwa kwa njia ya simu na kuulizwa juu ya taarifa hizo alisema alimuazima Aunty cheni hiyo ambapo naye alimpa shoga yake.
Aunty alipopatikana na kuulizwa alikana kumfahamu Shabani na kudai hana taarifa zozote za kuwepo kwa ishu hiyo.“Mh! Huo ni uzushi, hakuna kitu kama hicho na wala hizo taarifa sizifahamu, huyo mwanaume simjui ndiyo kwanza namsikia kwako,”alisema Aunty
REALITY SHOW YA WEMA SEPETU KUANZA IJUMAA UNAJUA NANI ATAONEKANA NDANI YA SHOW HIYO?
WEMA NA DIAMOND
Ile reality show ya muigizaaji WEMA SEPETU sasa inaanza tena ijumaa ijayo ambapo huu utakua ni msimu wa pili wa show hiyo, nilichofurahi kusikia ni kwamba humo ndani DIAMOND atakuwepo pia, ntaachaje kuiokosa show hii mimi jamani, maana ninavyompenda DIAMOND yani kama mdogo wangu wa tumbo moja. ntakuwa nawaletea mfululizo mzima wa show hizo humu na kuzichambua.
Ile reality show ya muigizaaji WEMA SEPETU sasa inaanza tena ijumaa ijayo ambapo huu utakua ni msimu wa pili wa show hiyo, nilichofurahi kusikia ni kwamba humo ndani DIAMOND atakuwepo pia, ntaachaje kuiokosa show hii mimi jamani, maana ninavyompenda DIAMOND yani kama mdogo wangu wa tumbo moja. ntakuwa nawaletea mfululizo mzima wa show hizo humu na kuzichambua.
UNAANZAJE KUIKOSA HII MOVIE MPYA YA ACTION YA BRAD PITT ILIYOTOKA JUZI
Wengi wafuatiliaji wa movie za action mnajua ma meeen BARD PITT huwa hakosei kwenye swala Zima la kuigiza, basi hembu kaicheki hii movie mpyaaaa imetoka week mbili zilizopita inayoitwa FURY, humu ndani ni ma action ya kivita ya kufa mtu.
NISIWAMALIZIE UHONDO, AGIZA POPCORN NA PEPS YAKO BARIIIDI UITAZAME
MCHEKI MDOGO WAKE KIM KARDASHIAN ALIVYOFANYA OPARATION YA KUONGEZA LIPS
ANAITWA KYLIE NI MDOGO WA MWISHO WA KIM KARDASHIAN.
embu tazama hizo picha na jinsi lips zake zilivyokua zinakua kubwa siku hadi siku
PICHA YA CHINI KABLA HAJAZIFANYIA UKARABATI LIPS
CHINI HAPO TENA BADO HAJASTUKA KAMA HANA LIPS
PICHA YA CHINI AMESHASTUKA HANA LIPS AKAKIMBIA MBIO KWA DOCTOR KWENDA KUONGEZA LIPS ILI AWE KAMA ANGELINA JOLIE
LIPS ZIMECHACHAMAA NA ANAZIPAKA LIPS STICK KIMADOIDO ILE MBAYA NA MAPOZI YA PICHA ZAKE YE NI KUONYESHA LIPS TU WAKATI DADA YAKE AKIWA BUSY KUONYESHA MAKALIO
Ndo hivyo kama mnavyomuona motto huyu ambaye sasa hivi kawa gumzo huko Marekani kutokana na kitendo cha kufanya operation ya kuongeza lips wakati yeye bado ni mdogo anamiaka 17 tu, LIPS ni midomo jamani kwa wale msiojua, motto huyo amekuwa akiulizwa mara kwa mara juu ya kulikoni kazaliwa na vilips vidogo halafu leo hii anamilips mikubwa, amekuwa akiwajibu kwamba hajafanyiwa operation bali ni make up tu ndo zinamfanya aonekane hivyo,
WAAFRICA TUMEBARIKIWA LIPS NZURI NA MAUMBILE MAZURI NA NGOZI NZURI, ZAMANI WAZUNGU WALIKUA WANATUONA KAMA MANYANI HIVI SASA WANASHINDA JUANI ILI NGOZI ZAO ZIWE ANGALAU NYEUSI HATA KIDOGO, WANAFANYA MA OPARATION YA KUONGEZA LIPS NA MAKALIO ILI WAWE NA MAUMBO KAMA YETU, bora nilivyozaliwa muafrica nimepunguza gharama za ma operation ya lips.
embu tazama hizo picha na jinsi lips zake zilivyokua zinakua kubwa siku hadi siku
PICHA YA CHINI KABLA HAJAZIFANYIA UKARABATI LIPS
CHINI HAPO TENA BADO HAJASTUKA KAMA HANA LIPS
PICHA YA CHINI AMESHASTUKA HANA LIPS AKAKIMBIA MBIO KWA DOCTOR KWENDA KUONGEZA LIPS ILI AWE KAMA ANGELINA JOLIE
LIPS ZIMECHACHAMAA NA ANAZIPAKA LIPS STICK KIMADOIDO ILE MBAYA NA MAPOZI YA PICHA ZAKE YE NI KUONYESHA LIPS TU WAKATI DADA YAKE AKIWA BUSY KUONYESHA MAKALIO
Ndo hivyo kama mnavyomuona motto huyu ambaye sasa hivi kawa gumzo huko Marekani kutokana na kitendo cha kufanya operation ya kuongeza lips wakati yeye bado ni mdogo anamiaka 17 tu, LIPS ni midomo jamani kwa wale msiojua, motto huyo amekuwa akiulizwa mara kwa mara juu ya kulikoni kazaliwa na vilips vidogo halafu leo hii anamilips mikubwa, amekuwa akiwajibu kwamba hajafanyiwa operation bali ni make up tu ndo zinamfanya aonekane hivyo,
WAAFRICA TUMEBARIKIWA LIPS NZURI NA MAUMBILE MAZURI NA NGOZI NZURI, ZAMANI WAZUNGU WALIKUA WANATUONA KAMA MANYANI HIVI SASA WANASHINDA JUANI ILI NGOZI ZAO ZIWE ANGALAU NYEUSI HATA KIDOGO, WANAFANYA MA OPARATION YA KUONGEZA LIPS NA MAKALIO ILI WAWE NA MAUMBO KAMA YETU, bora nilivyozaliwa muafrica nimepunguza gharama za ma operation ya lips.
EPISODE YA PILI LEO YA SHOW YA MDOGO WAKE TONI BRAXTON EMBU WATAZAME WALIVYOENDA KULA BATA MEXICO
Leo ni episode ya pili ya reality show ya TAMAE AND VINCE, kama nilivyowaambia Tamar ni mdogo wa mwisho wa Toni Braxton, basi kwenye episode hii utapata nafasi ya kuwaona wakienda vacation MEXICO, wenyewe pamoja na marafiki zao, raha zaidi inakuja kwenye vituko vya TAMAR, nisikumalizie uhondo tazama video hiyo hapo juu. BYEEEEEEEEEE
UNAIJUA HII MOVIE YA THE NOTE BOOK? KAMA UNAPENDA MOVIE ZA HOLLYWOOD INGIA USOME
Movie hii inaitwa THE NOTE BOOK, kwa wapenda movie za Hollywood embu wahi uicheki fasta, humu ndani amecheza RYAN GOSLING na RACHEL MCADAMS, kwa ufupi story ya movie inamuhusu binti ambae katoka kwenye familia njema yani mambo safi, halafu kapendana na kijana mzuri, mwenye tabia njema, mapenzi ya kweli lakini kijana katoka kwenye familia choka mbaya, sasa embu itafute uangalie mambo yalivyokua hapo, vikwazo walivyopitia manake hapo kuna lijamaa lenye pesa na lenyewe linamnyemelea huyo binti yani movie tamu sana hii.
WEMA SEPETU NA DIAMOND UHUSIANO UMEKWISHAAA.......INGIA UPATE UHONDO
Safari hii ndiyo basi tena! Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
KUMBE NI MUDA MREFU TU
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa.
SAFARI YA CHINA
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana na wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin Kadinda na Petit Man.
KAMA MBWAI, IWE MBWAI
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili wapo kwenye mabano, jambo ambalo Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita, hakuliafiki suala hilo lakini Madam akasema liwalo na liwe yaani kama ‘mbwai iwe mbwai’ hivyo akampuuza na kwenda zake China!
AHADI HEWA?
Chanzo hicho kilidai kwamba, kuna wakati Madam alimuomba Dangote au Chibu ampe fedha kwa ajili ya mtaji ambapo jamaa huyo alikubali lakini siku zikawa zinayoyoma bila dalili hivyo Wema akaona wa nini kama mtu mwenyewe hawezi kumsaidia?
ANAMTUMIA KIBIASHARA?
Ilisemekana kwamba, baada ya kuona hali hiyo, Wema alijiongeza na kuanza kukubaliana na makelele mengi kuwa jamaa huyo anamtumia kibiashara huku yeye akilamba shoo na kupiga fedha ndefu ndani na nje ya Bongo
UBAHILI WAMPONZA DIAMOND
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, tabia ya Diamond ya ubahili, nayo imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani jamaa huyo siyo mkataji wa mkwanja kama ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema, Clement.
“Wewe unamuonaje Wema? Yule mtoto bei mbaya bwana. Matunzo yake si mchezo. Sasa Dangote na ubahili wake ndiyo hivyo atamsikia Madam kwenye bomba,” kilisema chanzo hicho
BMW LATAJWA
Chanzo hicho kilitiririka: “Unalikumbuka lile BMW (gari) alilodaiwa Wema kapewa na Kadinda siku ya bethidei yake? Unajua Diamond alikuwa Marekani, sasa aliporudi akataka kujua BMW imetoka wapi maana yeye alitoa Murano, hapo ndipo moto ukawaka na wakawa hawaivani tena.”
BETHIDEI YA DIAMOND
Habari ziliendelea kupeperushwa kwamba siku ya bethidei ya Diamond ambapo jamaa huyo alizawadiwa BMW X6 na uongozi wake wa Wasafi, Wema alikwenda kwenye shughuli tu ili kuonekana kwenye kamera.
Ilisemekana kwamba, ndiyo maana kwenye shughuli hiyo Diamond ndiye aliyekuwa akihaha kuhakikisha Wema hapati usumbufu tofauti na Wema aliyekuwa anafuata tu maelekezo ‘kishingo upande’ kwani ndani yake hakuna mapenzi tena.
UKIMYA WAPITA
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio lile kulipita ukimya fulani huku kila mmoja akiishi kwake tofauti na awali ambapo Diamond alikuwa akijinasibu kuwa huwa analala nyumbani kwa baby (Wema), Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.
DRAMA KWENYE BETHIDEI YA AUNTY EZEKIEL
Kwenye bethidei ya mwigizaji ambaye ni shosti wa Wema, Aunty Ezekiel, Diamond ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ukumbini kwenye Mgahawa wa Rodizio uliopo Masaki jijini Dar, huku kukiwa na taarifa kwamba Madam asingekuwepo kwa kuwa alikuwa safarini
Wakati shughuli ikiendelea, Diamond alionekana mwenye furaha akiwa na timu yake lakini ghafla alipoibuka Wema upepo ukabadilika.
Wema alipoingia ukumbini akitokea safarini hata kabla ya kwenda nyumbani, alimpita Diamond, akaenda kusalimiana na Aunty kisha akaanza kuzunguka kwenye meza kusalimiana na mtu mmojammoja, cha ajabu alipofika upande aliokuwa ameketi Diamond na timu yake, aliwaruka na kwenda moja kwa moja kusalimiana na mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe
MINONG’ONO KILA KONA
Ishu hiyo iliibua minong’ono kila kona ya ukumbi huo na kuthibitisha zile tetesi kwamba hawapo kwenye uhusiano mzuri.Wakati Wema akifanya yake na Aunty, Diamond alipishana naye kama hawajuani na kukimbilia kwenye gari akiwa na timu yake tayari kwa kutimua.
‘HUYU DEMU SIYO’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kwa nini Diamond na ‘kruu’ yake waliacha sherehe wakitaka kutimua, mmoja wa memba wa timu yake ya Wasafi alisikika akisema ‘huyu demu siyo, hata ungekuwa wewe ingekuuma. Jambo alilomtendea mshikaji siyo poa kabisa’.
WEMA VIPI?
Alipododoswa Wema juu ya kuzama kwake ukumbini na kumfanya Diamond achomoke bila ya kusalimiana alishindwa kutoa majibu ya kina na kusema hakujua nini kilimkimbiza ila yeye alikuwa pale kwa ajili bethidei ya Aunt na si kingine.
DIAMOND ANASEMA?
Alipofuatwa Diamond kuzungumzia juu ya kutoka nduki baada ya Wema kuingia ukumbini hapo, aliomba mwandishi wetu amwache kwa maana kwamba ampotezee na kuzama kwenye ndinga lake na kuondoka kwa mbwembwe.
Hata kesho yake alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi ili aweze kuzungumzia hilo hakuonesha ushirikiano kwani simu yake ya kiganjani haikupokelewa muda wote alipopigiwa.
TUMETOKA MBALI
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha.
Wawili hao waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kisha kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji
Penniel Mungilwa ‘Penny’ huku cha Wema kikiwa kwa yule kigogo wake, Clement
SASA TEAM WEMA NAWAPENDA SANA MAANA MNAUPENDO WA DHATI KWA WEMA SEPETU, ILA TUNAWAOMBA MSIANZE KUMSEMA SEMA DIAMOND KAMA WEMA MWENYEWE ALIVYOAMUA KUKAA KIMYA BASI NA NYIE MUHESHIMU HILO NA MUWAACHE WAACHANE KWA AMANI KWANI MUDA SI MREFU WATARUDIANA SIMNAWAJUA HUWA HAWAWEZI KUISHI MBALIMBALI, SASA WAKIJAKUPATA ITAKUA HAILETI PICHA NZURI NA KAMA MNAVYOJUA MATUSI HAYAFUTIKI MOYONI , MSIANZE KUMSIMANGA , DIAMOND NI KIJANA CHAPAKAZI ALIPOTOKA NI MBALI NA ATAFIKA MBALI, WEMA NI BINTI MWENYE MOYO WA UPENDO NA ANAJUA SANA KUJISHUSHA NA NI MKARIMU KWA WATU, NAJUA MANAPOKUTANA MASUPERSTAR WAKUBWA NI KAZI SANA KUMAINTAIN MAHUSIANO YA KIMAPENZI KWASABABU VISHAWISHI NI VINGI, LAKINI KWENYE MAPENZI YA KWELI LAZIMA MAMBO YOTE YASHINDWE NA PENZI LISHINDE KWA HIYO WATARUDIANA TU, SO PULIZ WAPENZI MSIUNDE TEAM ZA KUANZA KUWATUKANA MKIFIKIRI MTAMFURAHISHA WEMA AU DIAMOND, MTAZIDI KUWAUMIZA TU.
EMBU MCHEKI JANEFER LOPEZ ANAMIAKA 45 LAKINI MMHH, KWELI UZEE MWISHO BONGO MAREKANI KILA MTU BABY.
Huyu ni muigizaji na pia mwanamziki wa Marekani anaitwa Janefer Lopez, hapo alipo JLO anamiaka 45 na anawatoto wawili, lakini ukimtazama kama anamiaka 25 jamani, kwa haraka haraka bongo movies wetu anayejitahidi kufuata nyayo zake naona ni LULU MICHAEL NA JOKATE, na MIMI RACHEL (natania) jamani
Thursday, October 30, 2014
GENEVIEVE NNAJI WA NIGERIA KAMA WEMA AKIWA NA MBWA WAKE EMBU MCHEKI
Muigizaji Gennevieve wa Nigeria huyo, wengi walikua hawajui kwamba Genevieve nayeye kumbe ni mpenzi wa hivyo vimbwa, lakini siku si nyingi alionekana na kimbwa chake basi watu wakachukua mapicha ya kumwaga, mi nimemfananisha na Wema maana na Wema wetu akiwa na kimbwa chake shughuli, mi naviogopaje nikianda nyumba yenye hutu tumbwa shuti kukipiga na pochi maana kung'atwang'atwa vidoleni sitaki.
MCHEKI KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST WALIVYOTOKELEZEA
Hii couple ilikua inasemwa sana huko Marekani lakini sasa hivi wenyewe wamewakubali, Kim analipenda sana hilo jacket naona hii ni mara ya nne kulivaa, sasa mastar wetu mnaoogopa kurudia nguo chukueni mfano hapo, nguo ununue mwenyewe kwa hela yako na umeipenda halafu unaogopa kuirudia kisa utaonekana umechacha, hii ni SHIDERRR.
anyway naweka habari za Kim Kardashian kwasababu pia ameshacheza movie kama mbili hivi, najua mtashangaa kwanini namuweka wakati yeye si muigiza humu hata ukicheza movie moja habari zako ntakua na ziweka na ma reality star pia nawaweka.
Wednesday, October 29, 2014
SHAMSA FORD KALETA MAPINDUZI MAPYA
SHAMSA FORD A.K.A CHAUSIKU AKIWA NA JB
Baada ya movie ya Chausiku kutoka muigizaji aliyecheza kinara anayeitwa SHAMSA FORD lakini kwenye movie alicheza kama CHAUSIKU amepata umaarufu mara mbili ya alivyokua awali, hii imefanya nione kwamba kumbe sasa wananchi hawaangalii sura wanaangalia kazi, yani ukiwa mrembo kama Kim Kardashian halafu ukacheza utombo kwenye movie hakuna atakayepoteza muda kukuangalia, sasa hivi watu wanataka mtu upige kazi kweli kweli sio kuringaringa kwenye movie, nimewapenda sana wabongo safari hii kwani hii imewapa watu motisha ya kufanya kazi kwa umakini, Shamsa alishacheza movie nyingi sana lakini hakuwa na kiwango che nyewe lakini kwenye movie ya chausiku Shamsa kaonyesha kipaji halisi bila kufake chochote kitu ambacho kimemfanya Shamsa apendwe mno na watu hivi sasa na watu wamemchukulia very serious kwenye kazi zake hivi sasa, mimi ninafuraha sana kwasababu nilikuwaga naumia ninapoona waschana wa bongo movie wanavyochululiwa kama wanajiuza tu kupitia movie wanazocheza lakini kwa mwendo huu aliounyesha Shamsa na wakina Riyama kwenye KIGODORO lazima tufike mbali na tuheshimike pia , mpaka nimefikiria kuanza kuiga, yani urembo unatakiwa uende na kupiga kazi yenye kiwango lakini urembo ukienda na upupu mtu utabaki kudharaulika kila siku.
NI HAYO TU WAPENZI NIONDOKE HUMU NDANI KESHO NARUDI TENA NA MAMBO MATAMU BYEEEEE
MADAI YA KWAMBA AUNT EZEKIEL NI MJAMZITO JE YANAUKWELI WOWOTE.
Baada ya muigizaji Aunt Ezekiel kuonekana akiwa na kitumbo ndi kwenye birthday party yake week end hii, wengi wametoa maoni kwamba Aunt kanasa ujauzito, huku wengi wakiwa hawaelewi kama ujauzito ni wa mumewe Sunday Demonte au wa yule mcheza show super handsome wa Diamond kwasababu hivi karibuni Aunt alizushiwa kwamba anamahusiano na mcheza show huyo, Kama ni kweli Aunt ni mjamzito hongera zake manake kapendeza mno yani nilivyomuangalia mbona nimetamani motto ghfla.
PICHA YA CHINI NI AUNT EZEKIEL AKIWA NA RAFIKI YAKE LE BIG SHOW LE MUTUZ NATION U KNOW, HAPO LEMUTUZ ALIKWENDA KUMPONGEZA AUNT KWA KUZALIWA TENA U KNOW, LEMUTUZ HUWA ANASEMA NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA KWA HIYO HAPO LEMUTUZ ALIKUA ANARUKA NA NDEGE WANAOFANANA , HAKUKUWA NA LE GADEM MAZAFANTAZZ MBURULAZZ U KNOW.
PICHA YA CHINI NI AUNT EZEKIEL AKIWA NA RAFIKI YAKE LE BIG SHOW LE MUTUZ NATION U KNOW, HAPO LEMUTUZ ALIKWENDA KUMPONGEZA AUNT KWA KUZALIWA TENA U KNOW, LEMUTUZ HUWA ANASEMA NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA KWA HIYO HAPO LEMUTUZ ALIKUA ANARUKA NA NDEGE WANAOFANANA , HAKUKUWA NA LE GADEM MAZAFANTAZZ MBURULAZZ U KNOW.
LEO MUIGIZAJI MREMBO GABRIELLA UNION AMEZALIWA
MWADADA HUYO KAMA MNAVYOMUONA ANAITWA GABRIELLA UNION NI MUIGIZAJI EXPENSIVE WA HOLLYWOOD LEO NI BIRTHDAY YAKE NA AMETIMIZA MIAKA 42, mmmhhh bidada anamiaka 42 lakini kama anamiaka 25, anyway moja ya movie alizocheza ni pamoja na THINK LIKE A MAN 1 NA 2,
KWA WALE WAPENZI WA TOM CRUZ HII MOVIE SI YA KUKUPITA, EMBU WACHEKI PIA NA WAHINDI WALIVYOMUIGA TOM CRUZ.
Hii apo juu ni movie ya kihindi inaitwa BANG BANG, ni bonge la movie na staring wake handsome kweliweli anaitwa RITHIK ROSHAN, basi hii movie ni ya action , lakini story ya hii movie wameichukua kwenye movie iliyochezwa Hollywood na TOM CRUZ ambayo inaitwa NIGHT AND DAY.
RITHIK ROSHAN
Huyu Rithik Roshan wengi wanamtambua kwa jina la KRISH kwani movie iliyomtambulisha kwenye ulimwengu wa movie ni movie iliyokua inaitwa KRISH , na mrembo wetu IRINE UWOYA nae aliamua kumpa mwanae jina la KRISH kutokana na mapenzi ya hiyo mivie ya KRISH , anyway huyu kaka ni actor mkubwa huko India lakini pia baba yake ni actor na producer mkubwa sana kwa hiyo kijana karithi kazi ya baba yake.
TOM CRUISE MOVIE NIGHT AND DAY
Sasa hiyo movie ya kihindi hapo juu ndo walichukua story kutoka kwenye hii movie, jamani jamani yani hii movie ya KNIGHT AND DAY ni bonge la movie kama mnavyomuona staring ni Tom akiwa na mwanadada CAMERON DIAZ pembeni na hawa walishawahi kuwa wapenzi kipindi cha nyuma, basi ndani ya movie hii kuna action za kutosha yani Tom anakinukisha humu jamani , na pia inavichekesho vya hapa na pale, technologia iliyotumika ni ya hali ya juu, yani hii ni aina ya movie unayoweza kuiangalia hata mara kumi.
TOM CRUISE NA CAMERON DIAZ
KAMA HUJAWAHI KUIANGALIA HII MOVIE NA WEWE NI MPENZI WA MOVIE ZA HOLLYWOODA BASI ITAFUTE UITAZAME YANI HUTAICHOKA.
Monday, October 27, 2014
WAKATI WEMA NA DIAMOND PLATNUMZ WANAJICHORA TATOO ZA WAZAZI WAO, NUHU MZIWANDA YUKO BUSY KUCHORA TATOO YENYE SURA YA SHILOLE MKONONI.
HUYU NI BOYFREND WA SHILOLE AKIWA NA TATOO MPYA YENYE SURA YA SHILOLE
Hawa ni kama Romeo and Juliet, lakini pamoja na kupendana kwao na pamoja na kwamba mpaka sasa wamekaa miaka mitano na wanapitia misuko suko mingi lakini hakuna aliyethubutu kuchora tattoo yenye jina la mwenzake na badala yake KILA MTU ANA TATOO YENYE JINA LA MZAZI WAKE.
CHORA TATOO LAKINI WEKA JINA LA WAZAZI AU WATOTO SIO LA MPENZI.
Mwanzo Nuhu alianza kujichora tattoo iliyoandikwa kwa maandishi makubwa jina la Shilole, tena basi sio jina halisi bali A.K.A ya shilole ambayo ni SHISHI BABY. yani litatoo likubwaa limeandikwa SHISHI BABY wakati the real name ya shilole ni ZUWENA, anyway tuachane na huo mkono mmoja, juzi tena mwanakaka kaamua kujichora mkono mwingine kama mnavyouona hapo juu ukiwa na sura ya Shilole. wadau wengine wanasema Nuhu anajichora ili kuwakomoa watu wanaomsema kuhusu mapenzi yake na shilole, sasa wananchi muache kumsema huyu motto manake mkiendelea motto atageuka LIL WAYNE maana atajichora viungo vyote vya Shilole miguu mikono simnaona kaanza na sura,
TATOO NI MCHORO PARMANENT NI HATARI SANA KWA KIJANA MDOGO AMBAYE BADO HAJAJUA MAISHA NI NINI KUJICHORA MAJINA AU PICHA YA MPENZI WAKE MAANA MKIACHANA UTAENDELEA KUBAKI NAYO NDO MAANA ULAYA MTOTO KAMA HAJAFIKA MIAKA 18 WAZAZI HAWAMRUHUSU KUJICHORA TATOO HATA YA UA.
DIAMOND NA WEMA HAPO CHINI WAKIWA NA TATOO ZA WAZAZI WAO.
Hawa ni kama Romeo and Juliet, lakini pamoja na kupendana kwao na pamoja na kwamba mpaka sasa wamekaa miaka mitano na wanapitia misuko suko mingi lakini hakuna aliyethubutu kuchora tattoo yenye jina la mwenzake na badala yake KILA MTU ANA TATOO YENYE JINA LA MZAZI WAKE.
CHORA TATOO LAKINI WEKA JINA LA WAZAZI AU WATOTO SIO LA MPENZI.
Subscribe to:
Posts (Atom)