Tuesday, August 12, 2014

TEAM WEMA SEPETU NA MALUMBANO YASIYOISHA.




Kama mnavyojua wapenzi muigizaji Wema Sepetu ndo star wa kike mwenye mashabiki wengi Tanzania nzima, kwenye mitandao ya kijamii kama instagram mashabiki hupenda kuunda team ambapo team Wema ndo team yenye nguvu kuliko team nyingine zozote na wamekua wakimtetea wema pindi inapoonekana Wema kaonewa.

HIVI KARIBUNI HIZO TEAM WEMA ZIMEKUA KAMA BOKO HARAM KWA JINSI WANAVYOTUPIANA MANENO WENYEWE KWA WENYEWE, mashabiki wa kawaida wanashindwa kuelewa ni nini chanzo cha hao wamiliki wa hizo page zinazomtetea Wema kulumbana, kwanza kabisa wengi  wao hawajuani na wengine hutumia majina fake, sasa kwanini wanalumbana hakuna anayejua, na kwanini walumbane wakati wenyewe lengo lao ni moja kwamba wanampenda Wema, hii inatia shaka na pia inaweza kumpunguzia Wema sifa pia, NI HAYO TU.


No comments: