Saturday, August 23, 2014

DIAMOND LEO KAACHA WATU MIDOMO WAZI...






Kama unaishi Tanzania nadhani ni lazima utakua unajua hili penzi la hawa watu wawili, muigizaji Wema Sepetu na mwanamziki Diamond, juzi kati kama walitibuana hivi, na mi humu ndani nikasema jamani mbona naona hawa watu wamekwepana kwenye birthday ya kaka yake Diamond Rommy Jones, basi bwana kumbe inavyoonekana ni kweli walitibuana, ila kama unavyojua HAWA WATU WANAMAHABA YA KIPEE NA YA DHATI NA WANASTYLE YAO YA KUPENDANA AMBAPO MTU MWINGINE UKIWAINGILIA LAZIMA UAIBIKE MJINI, YANI UKIMUONA MMOJA WAPO YUKO SINGLE UKAINGILIA KITAKACHOKUPATA NI AFADHARI YA KUHAMA MJI, sasa leo bwana harusi mtarajiwa Diamond kaamua kuwashtua watanzania kwa kutupia picha mbalimbali za kwake na za Wema kwenye mtandao wa instagram, picha hizo basi hazikua zenyewe mwanawane, zilisindikizwa na wimbo kutoka kwa marehemu Omary Kopa uliokua unasema " WANAOTAKA KUTUTENGANISHA WABAYA tumewaoooona, ,,,,,,,,,, uwiii hebu niishie hapa .


No comments: