Monday, August 4, 2014

KWA HARAKA HARAKA INASEMEKANA HUYU NDO MWANAMKE MWENYE FWEZA KULIKO WAIGIZAJI WA KIKE WOTE BONGO MOVIES.


                                            DEVOTA



Stori: Mayasa Mariwata  
MSHANGAO! Baadhi ya wasanii wa Klabu ya Bongo Movie Unity wamejikuta wakipigwa butwaa baada ya kutinga nyumbani kwa staa mwenzao, Devota Mbaga ambaye ni katibu wa klabu hiyo na kukuta akiishi maisha ya kifahari
Akipiga stori na gazeti hili, mmoja wa wasanii ambao walitia timu nyumbani kwa msanii huyo, Kigamboni, Dar ambaye hakuwa tayari jina lake lichorwe gazetini alisema, ilikuwa ni kama maajabu kwao kwa kukuta nyumba ya kifahari na kujua miradi yake mbalimbali lakini haringi.
“Kusema ukweli tumeshtuka, hatukutegemea kabisa, tulijua maisha yake ni ya kawaida, maana siyo mtu wa kujivuna kama wengine wenye nazo, nahisi kwa maisha aliyonayo sidhani kama yupo mdada wa Bongo Movie anayempata kwa utajiri alionao,” alisema msanii huyo.
Alipoulizwa Devota kuhusu ishu hiyo, aliishia kuangua kicheko na kusema mafanikio yake hayatokani na shughuli za sanaa pekee bali anajihusisha na miradi mbalimbali

1 comment:

web design los angeles said...

Haiwezekani, kuna waigizaji wenye hela ndefu sema wamejificha na kutulia na hela zao