Thursday, August 21, 2014

TATIZO LA MASTAR WA MOVIE KU BLOCK MASHABIKI KWENYE INSTAGRAM

                                                          KIM KARDASHIAN

Kwa harakaharaka naweza kusema hakuna superstar anayekosolewa kama KIM KARDASHIAN, wamemtukana matusi yote, wamemshusha na kila anachofanya hata kiwe kizuri vipi watu bado wanakumbushia sex tape yake, akiweka picha popote pale hasa kwenye instagram lazima apokee madongo ya kutosha, lakini hiyo haimaanishi kwamba Kim hapendwi, Kim ni star anayependwa kuliko kawaida nafikiri anafollowers wengi kwenye isntagram kuliko hata BEYONCE, sasa huwa najiuliza hivi Kim angekua anawablock wale wote wanaompaga madongo angebaki na mtu kweli, na huwezi kukuta mtu analalamika ka blockiwa na kim au namsanii yeyote wa nje,

tatizo linakuja kwa wasanii wetu wa bongo, mi ntawazungumzia wa movies, watu wanalalamika sana kublockiwa na hao wasanii, wakikosolewa kidogo tu lazima kesho ukiamka ukute ushablockiwa, sasa kama mtu umekubali kuwa star basi jiandae na kukosolewa, MI HUWA NAAMINI KWAMBA UKIONA MTU ANAKUKOSOA BASI KWANZA USHUKURU KWAMBA HUYO MTU KAKUFOLLOW MPAKA KAPATA CHA KUKUKOSOA, NA PIA KAMA ALICHOKUKOSOA KINA UKWELI BASI NI VIZURI KUJIFUNZA NA KUBADILIKA KULIKO KUBLOCK UTABLOCK MASHABIKI WANGAPI.  sijamlenga mtu wapendwa ila naona tu mashabiki mara nyingi wanalalamika nikaona nilete humu.

No comments: