Thursday, August 14, 2014

MARTIN KADINDA NA DIAMOND PLATNUMZ KWA NINI WALAUMIWE KWA KUSHUKA KWA WEMA?


Hapo juu hiyo ni picha ya reality show ya Wema, hapo Wema na shosti yake Aunt walikua wanataka kwenda kwenye kigodoro yani hata hicho kigodoro huwa sijui ni kinini anyway hapo walikua wanajiandaa kwenda kwenye kigodoro na ilikua saa saba usiku, Martin akawa akiwakataza tenakwa nguvu zote kwamba wasiende tena akawa anamkumbusha Wema kwamba kesho ni siku ya kazi unataka kwenda kwenye starehe saa saba usiku ili kesho ushinde umelala, tulishuhudia jinsi Wema alivyobisha mpaka ikabidi waende tu, hapo mtamlaumu Martini, kama kazi alishafanya ya kuhakikisha anamuelimisha Wema juu ya hadhari za yeye kwenda na jinsi inavyoaribu image yake lakini zaidi ya hapo jamani hata mimi ningeshindwa.
WEMA AKIWA NA MARTIN


WEMA NA DIAMOND

Wengi wanamlaumu Diamond kwamba anamtumia Wema kupanda chati, hivi wakati Diamond hayuko na Wema kwani alipungukiwa nini? si alitoa wimbo wa NGORORO , na huo wimbo si ndo ulioleta Baraka zote alizonazo Diamond hivi sasa, na je wakati MBAGALA inapigwa kwa kasi Enzi zile Diamond alikua na Wema? Wema si alikua na CHARZ BABA? kwanini Charz hakupanda na yeye akaanza kuimba na wakina FALLY IPUPA kama Diamond anavyoimba na DAVIDO, jamani DIAMOND is a very good artist and he work so hard, hata muda wa kua na Wema hana manake kila mara tunamsikia anasafiri kwenda kwenye mashow, hivi kwani Wema anakatazwa kufanya mambo makubwa na yeye, Diamond akisafiri Wema anabaki nyumbani anasubiri aletewe chocolate na perfume, hivi na yeye Wema angekua anapiga kazi huku nyuma si angekua mbali,

Hiyo picha hapo juu ni kipindi Wema akiwa ameachana na DIAMOND, ilikua ni kwenye tamasha la fiesta pia, sasa je kipindi hichi cha hizi picha WATU WALIKOSA WAKUMLAUMU? manake juzi Wema kakata miuno watu wanamlaumu Diamond, mwanaume hawezi akawa anakwambia kila kitu vitu vingine wewe kama mschana unatakiwa ujue kwamba hichi ni kizuri au hichi ni kibaya, ye mwanaume anakuangalia unavyobehave halafu mwisho wa siku anaamua akumwage au akuoe, sasa cheza jukwaani uchi halafu uone kama hajaoa mschana aliyekaa ndani akajiheshimu,

WEMA KUNA WASCHANA WENGI SANA WAZURI NA SIO MAARUFU AMBAO WANAFAA KUWEKWA NDANI, ANGALIA DIAMOND ASIKUTANE NA MMOJA WAO AKAAMUA KUMUOA, kama unavyojijua unakshfa nyingi, unachotakiwa ni kua na image nzuri ili hata Diamond akiambiwa Wema muhuni awe anajua ni uongo wanakusingizia, PIA HAKUNA NASEMA TENA HAKUNA MWANAUME ANAYETAKA KUOA MWANAMKE ASIYE NA MAENDELEO, DIAMOND ANAKUPENDA KWASABABU ANAKUONA UNAPENDWA KWENYE JAMII, LAKINI ATATAKA AKUOE KABISA PALE ATAKAPOONA JAMII INAKUSIFIA WEMA KAFANYA JAMBO FULANI,



No comments: