Saturday, August 30, 2014

BAADA YA NDOA TAKATIFU HII NI HABARI MPYA KWA WAIGIZAJI BRAD PITT NA MKEWE ANGELINA JOLIE




BRAD,ANGELINA NA WATOTO WAO WATATU WAKUWAZAA WENYEWE

BRAD NA ANGELINA
ANGELINA AKIWA NA MTOTO WAKE WA KUADOPT, HUYU NI WAPILI
BRAD AKIWA NA MTOTO WAO WA KWANZA WA KUADOPT
BRAD NA ANGIE WAKIWA NA WATOTO WAO WALIOWAADOPT

Okay ngoja nitiririke sasa, kama wengi mnavyojua waigizaji Angelina na Brad walifunga ndoa jumamosi iliyopita huko Paris, hivi sasa wanandoa hao na familia yao ya watoto sita wako nchini MALTA ambako wanashoot movie yao mpya itakayoitwa BY THE SEA patamu hapo, kwanza kabisa hawa watu walicheza movie yao ya kwanza wakiwa pamoja na ndo iliyowafanya wawe wapenzi mwaka 2005 movie hyo iliyovutia wengi inaitwa MR&MRS SMITH, na sasa baada ya miaka kupita wameamua kurudi tena na movie yao ya pamoja lakini hivi sasa ni wanandoa.

kinachonoga zaidi kwenye hiyo movie yao ya BY THE SEA ni kwamba wawili hao watecheza kama wanandoa na kutakua NA MA LOVEY DOVEY YA KUFA MTU, yani hapo hata Mungu anawapa Baraka zao wakicheza kimalovey dovey maana ni wanandoa tayari, kingine kinachovutia zaidi ni kwamba MOVIE HIYO IMEANDIKWA NA KUTAYARISHWA NA ANGELIA JOLIE MWENYEWE, mwenyewe Angie alipohojiwa alisema kwamba hii movie sio ya action yani ni movie simple tu ambayo inaelezea story ya mapenzi ya wanandoa basi,

NI HAYO TU WAPENZI....ILA BONGO PIA HATUKO NYUMA RAY NA CHUCHU HANS PIA NI WAPENZI WALIOCHEZA PAMOJA KWENYE MOVIE YAO WENYEWE ILITOKA HIVI KARIBUNI TU, yani huwa inapendeza sana ukiwaona wapenzi wanacheza movie pamoja kama wapenzi..


No comments: