Friday, August 29, 2014

KUHUSU SINTAH NA KUSHAMBULIWA KUTOKANA NA KAZI YAKE.


Nimekua nikifuatilia jinsi muigzaji Sintah anavyosemwa kutokana na kazi yake ya kila siku kwenye blog yake, kwanza Napata uwoga hata wa kublog kwani nakua nahisi nikiandika kitu kumuhusu mtu Fulani ntashambuliwa lakini pia hii kazi  ni ya kuandika matukio mbalimbali yanayotokea kwa watu sasa kama kila mtu atakataa kuandikwa tutaandika habari za wanyama? na nani atasoma, Leo Sintah kashambuliwa kwa kosa la kuandika habari ya mtu Fulani, lakini habari hiyo sio kwamba kaiandika kutoka kichwani au sio kwamba habari hyo kaiandika kwasababu anachuki na huyo mtu bali HABARI HIYO SINTAH KAI COPPY KUTOKA MAHALI KAIPASTE KWAKE sasa hapo kosa lake ni nini? anayetakiwa kushambuliwa si ni muanzilishi wa hiyo habari?  Sintah yeye ni muandishi wa habari hapo yeye anafnya tu kazi yake, japo na yeye kuna wakati huwa anakosea lakini kwenye habari ya kucoppy tena hajaongeza chumvi yeyote nadhani hapo haina haja ya kushambuliwa yeye, yeye kaileta tu habari ili wasomaji wake ambao hawajaiona sehemu nyingine waione, hata mimi habari hyo ingemuhusu msanii wa movie pia ningeileta ili na wasomaji wangu waione, hata MTANGAZI WA RADIO ANAPOSIKIA FUNUNU KUHUSU MSANII FULANI ANAWAJIBU WA KUMUITA NA KUMUHOJI ,JE BAADA YAKUMHOJI MTANGAZAJI ANATAKIWA ASHUMBULIWE? HAPANA YE MTANGAZAJI AMEFANYA KAZI YAKE TU, mi ningeshauri kama mtu unajijua wewe ni maarufu na hutaki kuwekwa kwenye blogs then STAY OUT OF DRAMAS.



No comments: