Saturday, August 2, 2014

GARI LA WEMA LAZINGIRWA NA MASHABIKI UWANJA WA NDEGE.







KATIKA hali ya kushangaza watu mbalimbali ambao ni mashabiki wa msanii wa filamu, Wema Sepetu walizingira gari la staa huyo huku wakimuamuru ashuke ili akaungane na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’


Tukio hilo lilitokea Jumatano hii maeneo ya Sinza-Mori, jijini Dar ambapo ndipo kulikuwa kikomo cha msafara uliokwenda kumpokea Diamond Uwanja wa Ndege Julius Nyere, Dar baada ya kutua akitokea kwenye tuzo za Afrimma, mashabiki hao walilizingira gari la mwanadada huyo huku wakimtaka Wema atoke ndani ya gari akapande kwenye gari alilokuwepo mpenzi wake huyo, wapigwe picha lakini hakushuka
Tunamtaka Wema ashuke kwenye gari lake apande huku kwa Diamond akae naye pale juu tuwashangilie kwa pamoja la sivyo hatupishi, tutaendelea kulizingira,” walisikika wakilalama mashabiki hao kwa nyakat tofauti, licha ya Wema kukataa kushuka, baadaye wakatulia na kuachia msafara uendelee






1 comment:

Anonymous said...

Nina imani katika mashabiki wa wema wewe ni mmoja wa ambao wanapata bahati ya kuonana nae au hata kusalimiana na hata kama si kusalimiana nae basis una uwezo wa kumshawishi aje akisome hiki ninachokiandika. Nampenda sana wema sana tena kiasi hata nashindwa kuelezea.. Sipendezwi kwake na kitu kimoja tu.. Kukaa kimya kimya kukaaa bila kufanya kazi.. Nampenda kuona akitolewa kwenye magazeti kwa habari za katoa filam hii anazindua filamu hii au filamu take imeuza zaidi kuliko wasanii wrote naimani hill kwake halishinsikani. Pengine wakati baby take anachukua tuzi huku yeye nae angekuwa ashachukua zake hata mbili... Inaniuma sana kuona yupo yupo tu umaarufu wake umebaki kwa kuwa na dai tu. Hana chochote anachofanya cha maana. Nashindwa kuelewa hata huyu manager wake anamshauri nini anammanage na kwa kazi IPI????? Kweli inasikitisha sana tena sana binafsi naumia nampenda kumuona yupo happy na anafanya kazi zake na tuzo anachukua uwezo wake na nyota take hakuna msanii anaemfikia hapa bongo. Kwanni analala kwann hatumii hii nafasi kwa sasa anatakiwa ajue umri unaenda. Asiishie kuandikwa kwenye magazeti kwa kushiriki vigodoro vya watu. Naomba wema Mimi kama shabiki yako ninaekupenda kwa dhati naomba uleye kazi zako sokoni naomba utufurahishe. Naomba uwajibikemwanamke. Naomba usilewe sofa na umaarufu wa kijinga. Nakupenda sana wema sepetu.... Naumia kwa hili I wish ningepata kujuanmini unawaza???? Juu ya kazi na una mpango gani na hiyo kampuni ulioianzisha hadi Leo hakuna movie hata moja sokoni... Wema plssss I love you