Monday, August 18, 2014

BONGO MOVIES KIMENUKA ..........




KIMENUKA! Klabu ya Bongo Movie Unity imedaiwa kuingia kwenye mpasuko mkubwa baada ya baadhi ya viongozi kutangaza kuachia ngazi kwa madai ya kuwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amechikichia mtonyo (fedha) mwingi wa klabu kwa masilahi yake



Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya klabu hiyo, juzikati viongozi wote wa klabu hiyo walikaa kikao kilichoitishwa na katibu wao, William Mtitu ambacho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kumwajibisha Steve Nyerere kwa madai hayo.
“Kuna fedha zilikuwa ni za maandalizi kwa ajili ya dua ya wasanii waliofariki dunia iliyofanyika Jumamosi.
“Pia kuna fedha nyingine zilitolewa hivi karibuni, walizitafuna akina Steve na baadhi ya viongozi, kilinuka kishenzi,” kilisema chanzo





Imeelezwa kuwa katika kikao hicho, hawakufikia muafaka kwani mtuhumiwa (Steve Nyerere) hakutokea pasipo kujulikana sababu za kutofika kwake.
Chanzo kiliendelea kudai, baada ya Steve kutoonekana, baadhi ya viongozi walisusa na kuondoka ambapo Katibu Msaidizi wa Bongo Movie, Devotha Mbaga na Mwekahazina Msaidizi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ walitangaza kuachia ngazi endapo muafaka wa fedha zinazodaiwa kuliwa kinyemela hautapatikana



Bongo Movie ni kivumbi mtindo mmoja kwa sababu baadhi ya viongozi walio karibu na Steve wanadaiwa kuchikichia fedha nyingi tu, kitu ambacho kinazua mtafaruku kwani siyo mara ya kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Mtitu ambaye ni katibu wa klabu hiyo, alipohojiwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kutokea ambapo alisema hata yeye amejipanga kuachia ngazi endapo hatapewa ufafanuzi wa fedha zinazodaiwa kuliwa na mwenyekiti wao
Steve Nyerere alipopigiwa simu kwa lengo la kuulizwa juu ya madai hayo, simu yake iliita bila majibu. Jitihada za kumtafuta zinaendelea




HIVI KWANI KUNA ULAZIMA WA HII CLUB YA BONGO MOVIES? MAANA KILA SIKU KINAMIGOGORO MNAFANYA HATA WASANII WAOGOPE KUJIUNGA.





No comments: