tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Wednesday, August 20, 2014
ORIGINAL KOMEDY JINSI WALIVYOSUMBUAGA TANZANIA
Bwana kumbuka Enzi hizo hichi kikundi cha Original komedy kilivyosumbua watu mjini, yani ukienda kwenye maduka siku ya alhamis ikifika saa kumi na mbili wanafunga fasta fasta ili kuwahi komedy, wauza mitumba ndo usiongee, ukipita kwenye maduka yanayouza tv utakuta saa moja usiku siku ya alhamis watu wamejaa nje unaweza kusema duka linawateja hili kumbe wote wanaangalia wakina joti, kwenye ma bar ndo kabisa mtu anahela ya soda moja tu lakini atainywa hiyo mpaka komedy iishe ndo anasepa, wababa sasa mwanzo mwanzo walikua wanadhani watoto na wake zao wanacheka ujinga, mara nawenyewe ikifika alhamis wanawahi kurudi nyumbani wote sebuleni kuangalia komedy, NILIWAHI KUKUTANA NA MZUNGU MMOJA HATA KISWAHILI HAJUI LAKINI ILIPOFIKA ALHAMIS AKASEMA JAMANI NATAKA NIANGALIE THE COMEDY YA KINA JOTI KILA MTU ALIMSHANGAA KAWAJULIA WAPI akasema imebidi niwajue manake toka nimefika Tanzania ikifika alhamis saa moja rafiki zangu hawataki kutoka kwenye tv mpaka hiyo the comedy iishe. kiukweli hawa vijana walivutia sana na wenyewe ndo chachu ya wengine kuunda vikundi kama hivi,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment