Huyu ndo kichuna wetu wa jumapili ya leo ni muigizaji JACKLINE WOLPER, Jackie bwana mi namuita the real diva, kwanza jinsi unavyomuona kwenye picha zake akiwa na make up au kajiedit unaweza sema ukimuona live atakua sio mzuri kivile, weee, yani HUYU BINTI UKIMUONA LIVE NI MZURI KULIKO ANAVYOONEKANA KWENYE PICHA NA KWENYE TV, YANI HUMU HUWA NAMKANDIA MAMBO MENGINE LAKINI KWENYE SWALA LA UZURI WIVU PEMBENI JAMANI HUYU MSCHANA ANASURA NA NGOZI NZURI MNO, YANI ANANGOZI LAINI MNO, YANI HUYU SIO KAMA WALE MA DIVA WANAOJIEDIT HALAFU UKIJA KUWAONA LIVE NI TOFAUTI, AU ANAIPIGA PICHA SURA KIUPANDE AU KAITENGENEZA HIVI HALAFU UKIMUONA FULL NI TOFAUTI, HAPANA JACKLINE WOLPER NI MZURI MZURI HASWA TENA KWENYE PICHA NDO SIO SANA KAMA AMBAVYO UTAMUONA LIVE NA ANAMACHO MAZURI MNO PIA YANI SURA YAKE NI KAMA MDOLI KWA UFUPI NA NIISHIE HAPA.
tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Sunday, August 31, 2014
Saturday, August 30, 2014
BAADA YA NDOA TAKATIFU HII NI HABARI MPYA KWA WAIGIZAJI BRAD PITT NA MKEWE ANGELINA JOLIE
BRAD,ANGELINA NA WATOTO WAO WATATU WAKUWAZAA WENYEWE
BRAD NA ANGELINA
ANGELINA AKIWA NA MTOTO WAKE WA KUADOPT, HUYU NI WAPILI
BRAD AKIWA NA MTOTO WAO WA KWANZA WA KUADOPT
BRAD NA ANGIE WAKIWA NA WATOTO WAO WALIOWAADOPT
Okay ngoja nitiririke sasa, kama wengi mnavyojua waigizaji Angelina na Brad walifunga ndoa jumamosi iliyopita huko Paris, hivi sasa wanandoa hao na familia yao ya watoto sita wako nchini MALTA ambako wanashoot movie yao mpya itakayoitwa BY THE SEA patamu hapo, kwanza kabisa hawa watu walicheza movie yao ya kwanza wakiwa pamoja na ndo iliyowafanya wawe wapenzi mwaka 2005 movie hyo iliyovutia wengi inaitwa MR&MRS SMITH, na sasa baada ya miaka kupita wameamua kurudi tena na movie yao ya pamoja lakini hivi sasa ni wanandoa.
kinachonoga zaidi kwenye hiyo movie yao ya BY THE SEA ni kwamba wawili hao watecheza kama wanandoa na kutakua NA MA LOVEY DOVEY YA KUFA MTU, yani hapo hata Mungu anawapa Baraka zao wakicheza kimalovey dovey maana ni wanandoa tayari, kingine kinachovutia zaidi ni kwamba MOVIE HIYO IMEANDIKWA NA KUTAYARISHWA NA ANGELIA JOLIE MWENYEWE, mwenyewe Angie alipohojiwa alisema kwamba hii movie sio ya action yani ni movie simple tu ambayo inaelezea story ya mapenzi ya wanandoa basi,
NI HAYO TU WAPENZI....ILA BONGO PIA HATUKO NYUMA RAY NA CHUCHU HANS PIA NI WAPENZI WALIOCHEZA PAMOJA KWENYE MOVIE YAO WENYEWE ILITOKA HIVI KARIBUNI TU, yani huwa inapendeza sana ukiwaona wapenzi wanacheza movie pamoja kama wapenzi..
Friday, August 29, 2014
KUHUSU SINTAH NA KUSHAMBULIWA KUTOKANA NA KAZI YAKE.
Nimekua nikifuatilia jinsi muigzaji Sintah anavyosemwa kutokana na kazi yake ya kila siku kwenye blog yake, kwanza Napata uwoga hata wa kublog kwani nakua nahisi nikiandika kitu kumuhusu mtu Fulani ntashambuliwa lakini pia hii kazi ni ya kuandika matukio mbalimbali yanayotokea kwa watu sasa kama kila mtu atakataa kuandikwa tutaandika habari za wanyama? na nani atasoma, Leo Sintah kashambuliwa kwa kosa la kuandika habari ya mtu Fulani, lakini habari hiyo sio kwamba kaiandika kutoka kichwani au sio kwamba habari hyo kaiandika kwasababu anachuki na huyo mtu bali HABARI HIYO SINTAH KAI COPPY KUTOKA MAHALI KAIPASTE KWAKE sasa hapo kosa lake ni nini? anayetakiwa kushambuliwa si ni muanzilishi wa hiyo habari? Sintah yeye ni muandishi wa habari hapo yeye anafnya tu kazi yake, japo na yeye kuna wakati huwa anakosea lakini kwenye habari ya kucoppy tena hajaongeza chumvi yeyote nadhani hapo haina haja ya kushambuliwa yeye, yeye kaileta tu habari ili wasomaji wake ambao hawajaiona sehemu nyingine waione, hata mimi habari hyo ingemuhusu msanii wa movie pia ningeileta ili na wasomaji wangu waione, hata MTANGAZI WA RADIO ANAPOSIKIA FUNUNU KUHUSU MSANII FULANI ANAWAJIBU WA KUMUITA NA KUMUHOJI ,JE BAADA YAKUMHOJI MTANGAZAJI ANATAKIWA ASHUMBULIWE? HAPANA YE MTANGAZAJI AMEFANYA KAZI YAKE TU, mi ningeshauri kama mtu unajijua wewe ni maarufu na hutaki kuwekwa kwenye blogs then STAY OUT OF DRAMAS.
MSANII SABBY ANGEL JINSI ALIVYOTESWA NA RUSHWA YA NGONO KWENYE BONGO MOVIES.
Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa akifurukuta kutoka kisanii
Akizungumza na Ijumaa Sabby alisema, tatizo hilo la rushwa anaweza kuwa miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna baadhi walipokuwa wakitolewa nje, walikuwa wanajenga bifu naye na wengine kumtishia kumharibia.
“Mimi kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka leo ni jinsi wanawake tunavyodhalilishwa kila siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi mpaka nafikia hapa leo, ila namshukuru Mungu siku zote,” alisema Sabby ambaye ameng’ara kwenye filamu kama vile Siri ya Gining, Hard Price, Moto wa Radi, Dr. Ray na nyinginezo.
DU POLE SANA SABBY, HAYA MAMBO YANAKATISHA SANA TAMAA,
WEMA SEPETU AMSHAURI PETIT MAN KUMUO DADA WA DIAMOND NA NDOA IKO MBIONI.
MAPENZI bwana! Baada ya kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja, hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu, Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilicho karibu na Diamond na Wema ambao penzi lao lilipata ‘mushkeli’ kidogo hivi karibuni, Petit Man tayari ameshakamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanyika kabla ya ndoa na kilichobaki ni kutamka siku husika tu.
Kilidai kuwa, Petit alichukua uamuzi huo baada ya kushauriwa na Wema kuwa umri unakwenda na vishawishi ni vingi hivyo ni bora aoe mapema.“Unajua Petit Man anamheshimu sana Wema kwa hiyo alipomwambia Petit kuwa umri unazidi kwenda na anahitaji kuwa na familia yake akaukubali ushauri wake,” kilinyetisha chanzo hicho
Baada ya kupata maelezo hayo, Ijumaa lilimtafuta Petit Man na kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo, bila kuumauma maneno alikiri.“Ni kweli mama (Wema) aliniweka chini na kuniambia kuwa umri unakwenda hivyo nahitaji niwe na familia yangu kwa hiyo siwezi kuwa na familia bila ya kuwa na mke ndipo aliponichagulia mke ambaye ni dada yake wa damu kabisa na Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayeitwa Esma na kwa taarifa yako tu, tayari nimeshakamilisha kila kitu,” alisema PetitAlipoulizwa kuhusiana na wanawake aliowahi kuwa nao kipindi cha nyuma akiwemo Kajala, Petit alisema huko kote ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ambayo ni ndoa yake na Esma.
“Acha nipumzike na madhira ya dunia maana huko kote nilipopita hakukuwa chaguo langu ila kwa Esma nimekufa nimeoza bado kuzikwa tu yaani mimi ni mfu ninayetembea mbele ya Esma
Thursday, August 28, 2014
ANGELINA JOLIE NA BRAD PITT WAMEFUNGA NDOA NCHINI PARIS.
HILI NDO ENEO WALILOFUNGIA NDOA HUKO PARIS
HAWA NDO HUSBAND AND WIFE
HII NDO PICHA YA KWANZA BRAD KUPIGWA TOKA AWE MUME WA MTU
MMHHH kwanza nasikitika sana BRAD PITT kua off the market, Angelina u are so damn lucky, Brad kwanza anavyovutia hivyo unaweza kusema he is 35 kumbe he is 50 uwiii, halafu huwa hana makashfa ya ajabu ajabu," jamani nilikua nachelewa kuolewa nikitegemea Brad atanioa ha ha ha ha kidding" ANYWAY MASUPER STAR HAWA WA HOLLYWOOD WAMEONA WEEK END HII HUKO PARIS, NDOA YAO ILIKUA NI YA SIRI MNO WATU WAMESHTUKIA BAADA YA KUONA PETE YA NDOA KIDOLENI KWA BRAD PITT, INASEMEKANA MTOTO WA KWANZA WA ANGELINA NA BRAD NDO ALIYEMSINDIKIZA MAMA YAKE PALE MBELE KANISANI, NA WARUSHA MAUA WALIKUA NI WATOTO WAO WAKIKE, MPAKA SASA PICHA ZA SHEREHE HIYO HAZIJATOLEWA.
Wednesday, August 27, 2014
MUIGIZAJI MONALISA NI KAMA GENEVIEVE NNAJI WA NIGERIA.
Huyu hapa chini ni muigizaji wa Tanzania anaitwa MONALISA, na huyo juu ni muigizaji wa Nigeria anaitwa GENEVIEVE NNAJI.
Hawa waigizaji huwa kwanza wanafanana rangi zao za ngozi, wote wana natural African colour, pia wote huwa wanaheshimika sana kwenye jamii, huwa wanajiepusha sana na maskendo ya hapa na pale, na ni wazuri pia kwa muonekano na wanakipaji hasa kwenye uigizaji.
MUIGIZAJI WA HOLLYWOODA BRAD PITT TOKA AWE NA MKEWEANGELINA JOLIE HICHI NDO KITU ALICHOSEMA HATAKIFANYA TENA.
MAMA WATOTO WA BRAD, ANGELINA JOLIE
Muigizaji mwenye mvuto hasa wa kiume wa nchini Marekani Brad Pitt alikutana mama watoto wake kwenye movie waliocheza pamoja mwaka 2006 inayoitwa MR & MRS SMITH, mapenzi yao yaliposhamiri Brad kwa kipindi alikua na mke ambaye pia ni muigizaji JANE ANISTON, ilimbidi Brad amtwange talaka Jane ili kuanzisha familia na Angelina na hivi sasa wanawatoto sita ambao watatu ni wakuwazaa na watato ni wa kuadopt,
KUTOKANA NA BRAD KUMPENDA ANGELNA KWASABABU YA KUCHEZA MOVIE YA KIMAPENZI PAMOJA, BRAD AMESEMA KAMWE HATACHEZA TENA KIMAHABA KWENYE MOVIE ZAKE ZIJAZO, HATA IKITOKEA AKACHEZA KAMA MUME AU MCHUMBA WA MWANAMKE FULANI BASI ATAHAKIKISHA HAKUNA YALE MAMBO YAMAHABA NILIPUE YANI ITAKUA KAMA MAHABA YA KIHINDI KISS YA MBALIIII, BRAD ALIAMUA KWA KUONA KWAMBA ANAHITAJI KUMUHESHIMU MAMA WATOTO WAKE NA KUMFANYA AWE CONFORTABLE MANAKE KAMA UNAVYOJUA KAMA MLIKUTANA KWENYE MOVIE YA MAHABA LAZIMA MUME WAKO AKICHEZA TENA KIMAHABA NA MWANAMKE MWINGINE UOGOPE UHISI NA WEWE UNAWEZA PINDULIWA.
MPYA KUHUSU LULU MICHAEL
MAKUBWA! Mambo yamekuwa mambo, kadi ya gari jipya la staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ imeibua mazito kufuatia Jeshi la Polisi Dar es Salaam kubaini kuwa namba ya Sanduku La Posta (SLP) iliyoandikwa kwenye kadi hiyo ni Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania.
IMEVUJAJE?!
Hilo lilibainika baada ya gazeti dada na hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita kuandika habari yenye kichwa kisemacho; LULU AANDIKA HISTORIA.
Katika habari hiyo, Lulu alipewa shavu kwa vile alinunua gari aina ya Toyota Rav 4 New Model kwa pesa zake mwenyewe tofauti na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao huhongwa magari na wanaume.
SIMU YAPIGWA
Wakati gazeti hilo likiwa mitaani, mtu mmoja aliyedai kuwa ni afisa wa jeshi la polisi jijini Dar es Salaam alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers na kusema kuwa S.L.P ya 9140 iliyotumika kwenye kadi ya gari la Lulu ni ya jeshi hilo.
NI KOSA LA JINAI
Ofisa huyo aliliambia gazeti hili kuwa raia wa kawaida haruhusiwi kutumia sanduku la barua la jeshi kitu alichodai kinaonesha jinai ilifanyika wakati wa usajili ya gari hilo.
“Haiwezekani Lulu atumie Postal Office Box (P.O.Box au S.L.P) ya jeshi kwenye kadi ya gari lake ikizingatiwa kuwa yeye ni raia wa kawaida.
“Ukiachana na hilo hata sisi maofisa wa jeshi la polisi hatuwezi kuitumia hiyo anuani kwa shughuli zetu binafsi labda kuwe na kibali maalum,” alisema afisa huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji wa jeshi hilo.Ofisa huyo aliliambia gazeti hili kuwa raia wa kawaida haruhusiwi kutumia sanduku la barua la jeshi kitu alichodai kinaonesha jinai ilifanyika wakati wa usajili ya gari hilo.
“Haiwezekani Lulu atumie Postal Office Box (P.O.Box au S.L.P) ya jeshi kwenye kadi ya gari lake ikizingatiwa kuwa yeye ni raia wa kawaida.
LULU ANASEMAJE?
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta Lulu ili kujibu madai hayo yenye utata ambapo alisema kuna mtu alimtengenezea namba yake ya TIN (Taxpayer Identification Number) ndiye aliyemwekea anuani hiyo bila yeye kujua.
Huku akisita kumtaja kwa jina mtu huyo lakini akimtaja kwa cheo ambacho kiko wazi na mapaparazi wetu wakamjua, Lulu alifunguka hivi:
“Namiliki gari langu kihalali kabisa na nina kila kitu, niko tayari kwenda kokote kuonesha uhalali wa umiliki wangu. Kuhusu hiyo anuani, mtu aliyenitengenezea TIN Number ili nipate leseni ya udereva ndiye aliyetumia hiyo anuani, mimi sijui chochote jamani.”
AOMBA AHIFADHIWE SIRI
Katika hali ya kushangaza, Lulu aliwaambia mapaparazi wetu wasimtaje jina gazetini mtu huyo aliyemsajilia TIN akisema asitiriwe siri yake.
POLISI NAO WANENAKatika hali ya kushangaza, Lulu aliwaambia mapaparazi wetu wasimtaje jina gazetini mtu huyo aliyemsajilia TIN akisema asitiriwe siri yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ambako ndiko usajili wa gari hili ulifanyika katika ofisi za TRA, Zakaria Sebastian, alisema jeshi lake halina taarifa za kuwepo kwa jambo hilo lakini watalifuatilia kwa karibu.
“Huenda ni mke wa askari au mwanafamilia. Unajua kuna baadhi ya maofisa wana msamaha, huenda alitumia hivyo, lakini tutafuatilia,” alisema kamanda huyo ambaye alielezwa kuwa, Lulu hajawahi kuwa mke wala mwanafamilia ya mwajiriwa wa jeshi la polisi.
“Kama hajawahi kuwa mwenye kustahili kutumia anuani hii, basi tutafuatilia ili kujua wakati akiitumia, je alikuwa anakusudia kufanya jinai? Tukijiridhisha hivyo bila shaka sheria itafuata mkondo wake.”
UCHUNGUZI WA RISASI MCHANGANYIKO
Katika uchunguzi wa gazeti hili, anuani hiyo imeshatumika na Jeshi la Polisi Magomeni na Mkoa wa Polisi wa Ilala jijini Dar. Namba hiyo inatofautiana tarakimu moja na ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
NAKUMBUKA KIPINDI WOLPER ALIPOKUA NA LILE GARI LAKE BMW X6 MAGAZETI YALIPOTOA KADI TU YA GARI MATATIZO YAKAANZA NA HATIMAE GARI LIKACHUKULIWA, TUNAMUOMBEA LULU MAMBO HAYO YASIJEKUTOKEA.
Tuesday, August 26, 2014
UNAJUA NI KITU GANI SHILOLE NA KAJALA MASANJA HAWAPENDI KUVAA PAMOJA NA KWAMBA WANAPENDA SANA UREMBO?
KAJALA MASANJA
Waigizaji hawa wenye mvuto wa bongo movies Shilole na Kajala huwa wanapenda sana urembo na kwenda na wakati, lakini kitu kimoja ambacho huwezi kuwakuta wamevaa ni viatu virefu, yani ni mara chache mno ndo unaweza kuwakuta wako kwenye high hells lakini mara nyingin wenyewe hawapendi shida na kukomazana miguu wenyewe wanapenda kua comfortable na flat shoes tu.
HII MOVIE YA KINAIGERIA YA CRY FOR HELP INAWEZA KUKUTOA MACHOZI
NKIRU SYLVANUS
Hii movie ya CRY FOR HELP ilichezwa zamani na star wa movie ni huyu dada muigizaji wa Nigeria anaitwa NKIRU SYLVANUS, yani jamani kama unamachozi ya karibu lazima ulie ukiitazama hii movie, yani huyu dada alifiwa na mume wake aliteswa na ndugu za mume na kuzomewa na kijiiji wakimshutumu kwamba yeye ndo kamuua mumewe, ilifika kipindi mpaka wakamlazima chumba kimoja na maiti ya mumewe na wakamwambia aiogeshe maiti kasha yale maji yaliyooshewa maiti ayanywe, lakini mwisho wa siku akaja kuokolewa na mchungaji na baadae akapata mume mwema akaolewa. ni movie nzuri mno.
Monday, August 25, 2014
BEYONCE NA JAY ZEE KAMA WEMA NA DIAMOND VILE KWENYE SWALA LA KUSTOPISHA SHOW.
The greatest living entertainer' that is how a proud Jay Z introduced his wife when he handed her the night's prestigious Michael Jackson Video Vanguard Award.
The couple, who have been plagued by divorce rumours for a while now, did a good job last night to dispel the rumours when Jay Z, carrying their daughter, joined Beyonce on stage after her incredible performance to hand her the award.
Jay Z, with tears in his eyes, kissed his wife, while she called him "my beloved." And then adorable Blue Ivy said 'Mommy' and a visibly moved Beyonce said;
The couple, who have been plagued by divorce rumours for a while now, did a good job last night to dispel the rumours when Jay Z, carrying their daughter, joined Beyonce on stage after her incredible performance to hand her the award.
Jay Z, with tears in his eyes, kissed his wife, while she called him "my beloved." And then adorable Blue Ivy said 'Mommy' and a visibly moved Beyonce said;
“I'm so full. Thank you. I have nothing to say but I'm filled with so much gratitude. I thank God for this moment. I love you so much. 'Baby Blue, I love You. My beloved, I love you. My fans, I love you. MTV, I love you. Goodnight."
Beyonce was the night's biggest winner with four awards. Do you agree that Beyonce is the greatest living entertainer? I do. Continue to see more photos of the couple at the awards
ehhh hayo ndo yaliyojiri kwa muigizaji wa movie ya OBSESSED Beyonce.
Subscribe to:
Posts (Atom)