Tuesday, November 25, 2014

WEMA NA DIAMOND WAHAMISHIA MOVIE YAO UGANDA MWEZI UJAO

 WEMA SEPETU AKIWA NA MPENZI WAKE WA MILELE DIAMOND PLATNUMZ
 
Hivi  majuzi habari zilienea kwamba mwanamziki ambaye ni mchumba wa muigizaji Wema Sepetu alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamama wa Uganda anayeitwa Zari , basi bwana, huyo Zari ameandaa party aliyoipa jina la CYROC WHITE PARTY, party hiyo itafanyika Dec 18 ambapo inasemekana mwanamziki wetu expensive Bongo nzima DIAMOND PLATNUMZ atahudhuria party hiyo. Wema nae kaamua kujibu mapigo, siku hiyo hiyo ya Dec 18 mwanamziki nguli wa Uganda JOSE CHAMELEON na yeye atafanya show ya kufunga mwaka ambapo kiingilio ni million moja ya Uganda WEMA SEPETU atakuwa ndani ya nyumba, basi jana Wema kupitia mtandao wake wa instagram aliwaharifu mashabiki wake kwamba atakuwepo Uganda kwenye show ya JOSE siku ya tarehe 18 muda mchache na Diamond nae akatoa tangazo la kuwaarifu mashabiki wake juu ya party ya Zari siku ya tarehe 18. mashabiki wengi walionekana kufurahishwa na haka kaushindani ka wapendanao hao ambao ni wazi wanakomoana tu ila mwisho wa siku wanapendana mpaka shetani anaogopa, sasa watu wanasubiri jinsi Uganda itakavyozizima, kwasababu ni wazi kwenda kwa Wema Uganda ni kwa ajili ya kumkomoa Diamond tu hivyo hivyo na kwa Diamond pia, ZARI NI MWANAMAMA MWENYE PESA NDEFU NA JOSE CHAMELEON NI MWANAMZIKI MWENYE PESA NDEFU AFRICA MASHARIKI NZIMA,

JOSE CHAMELEON WA UGANDA
 
ZARI
 
WEMA NA DIAMOND WAKIGOMBANA SHIKA JEMBE UKALIME WAKIPATANA BEBA KAPU UKAVUNE, UKIINGILIA UTAPATA AIBU MJINI .

2 comments:

Anonymous said...

Kiekiekie,Diamond ana kwa mbiya kama maneno ya watu Ungelikuwa sumu la kama pendo lao limehisha kufa,kuzikwa na kuhoza ,sasa tuwa ache tu kwa sababu wangali location na tu ngojeye movie tuuuuu

Anonymous said...

Me loving this kwa kweli!