tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Thursday, November 6, 2014
JACKLINE WOLPER YADAIWA AMSALITI KAJALA KWA WEMA SEPETU
UNAFIKI 100%! Wakati kila mtu akiamini kwamba staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ni shosti wa Kajala Masanja ‘Kay’, ameibua mshangao baada ya kunaswa akikumbatiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa haziivi na Kay
TUJIUNGE KWENYE BETHIDEI
Tukio hilo lililoibua maswali mengi yasiyokuwa na majibu ya harakaharaka lilijiri hivi karibuni katika bethidei ya shosti wa damu wa Wema, Aunty Ezekiel Grayson ambayo ilifanyika kwenye Mgahawa wa Rodizio, Masaki jijini Dar.
WAKUMBATIANA
Huku paparazi wetu akishuhudia na kuwafotoa picha, Wema alipoingia tu ukumbini humo, alimkuta Wolper akila raha zake ambapo alimkimbilia kisha akamkumbatia kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mabusu kuonesha wamemaliza tofauti zao na kwamba walikuwa ‘wamemisiana’.
Wakati wamekumbatiana na kupigana mabusu walikuwa wakinong’onezana mambo yao ambapo walipomaliza waliachia vicheko vilivyosikika ukumbi mzima ndipo minong’ono ikaanza.
WATAALAM WA UBUYU
Kitendo cha Wema kutumia dakika kadhaa kukumbatiana na Wolper, kilitafsiriwa na wataalam au wafuatiliaji wa mambo ya watu (ubuyu) kuwa ni usaliti mzito kwani Wolper ni Timu Kajala ambaye ni hasimu mkubwa wa Wema
Mh! Mwenzangu makubwa, huyu Wolper si ni Timu Kajala? Inakuwaje anatoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa adui wa Kajala? Hapa kuna tatizo, unafiki kwa mastaa kamwe hauwezi kuisha,” alisikika mtoa ubuyu mmoja aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.
AKUMBUSHA VITA YAO
Kama hiyo haitoshi, mtoa ubuyu huyo alikwenda mbali zaidi kwa kusema, ukiachilia mbali Wolper kuwa karibu na Kajala lakini hata yeye (Wolper) alikuwa kwenye vita nzito na Wema kwa kudaiwa ‘kushea’ naye penzi la msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Wolper jamani mnafiki...si ndiyo huyuhuyu aliwahi kuingia kwenye vita nzito na Wema baada ya kudaiwa kuwa anadondoka dhambini na kipenzi cha Madam, Diamond? Yaani huu ni unafiki asilimia mia,” alisema mtoa ubuyu huyo.
TIMU KAJALA WAJA JUU
Baada ya Timu Kajala kusikia kwamba Wolper ‘ali-spendi’ vya kutosha na Madam kwenye bethidei hiyo, walikuja juu kisha wakamtolea uvivu na kuanza kumshambulia katika mitandao ya kijamii na kudai hafai kuwa timu yao
Wolper msaliti, ataendaje kwenye sherehe ya mpinzani wetu? Tena kama hiyo haitoshi, yeye anakumbatiana na Madam ambaye kwetu sisi hatusaidii lolote,” alisema mmoja wa Timu Kajala.
KUMBUKUMBU IPOJE?
Kabla ya siku hiyo, Wolper na Wema hawakuwahi kuwa na uhusiano mzuri na kila sehemu ambayo utakumta Wolper, kamwe huwezi kuona Wema ametia maguu.
WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya paparazi wetu kushuhudia kitendo hicho ukumbini, alimfuata Wolper na kumuuliza ni kitu gani kilichowasababisha wapatane na kuoneshana ‘mahaba niue’ wakati nyuma ya pazia wana bifu? Msikie alichojibu
Ujue watu wengi sana wamekuwa wakidhani mimi na Wema tuna bifu, sijui kwa kuwa mimi nina ukaribu na Kajala au kwa kuwa hatujawahi kuwa pamoja, lakini ukweli mimi na Wema siyo waongeaji sana japokuwa huwa nikiweka picha au chochote kwenye Instagram, Wema huwa ana-like na mimi huwa na-like vitu vyake hivyo sidhani kama nilikuwa na tatizo naye sana,” alisema Wolper.
TUJIKUMBUSHE
Urafiki wa mastaa huwa mara nyingi haudumu, Wema ambaye hivi sasa shosti wake mkubwa ni Aunty, kabla aliwahi kuwa na urafiki na Snura Mushi, Jamilah wa Temba, Kajala na wote hao akawamwaga
WEMA AKISALIMIANA NA JACKLINE KWA FURAHA
JACKLINE WOLPER AKIWA NA KAJALA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment