Monday, November 17, 2014

MTANGAZAJI WA BONGO MOVIES JOYCE KIRIA AKWAA SKENDO YA UTAPELI...




WHY Joyce? Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria yupo kwenye wakati mgumu baada ya kukwaa skendo ya utapeli kwa marafiki zake (majina yanahifadhiwa kwa sasa) akidaiwa kuwashawishi kuingia kwenye biashara ya Mtandao ya Telexfree Network Marketing
Kwa mujibu wa sosi makini, ishu hiyo imeibuka juzikati ambapo Joyce alikuwa akishushiwa zigo la lawama na marafiki zake hao huku baadhi wakitishia kumshitaki kwa kuwatapeli kwani wamepoteza fedha nyingi kwenye mpango huo wakidai hawajaona chochote
Dada Joyce aliwashawishi marafiki zake wengi, wakaingia na kila watu walipomshtua na kumwambia kuwa ni utapeli mtupu alikuwa akiwatolea lugha za kuudhi. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Joyce na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: “Ni kweli niliwashawishi marafiki zangu kwa sababu nilijua biashara hiyo inalipa na hata mimi nimeumia sana kuona imekufa kwani sikupenda.
“Nimepoteza fedha nyingi. Ilikuwa ni kama desi ilivyokufa, hakuna wa kulaumiwa.”
Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.
Telexfree Network Marketing ni kampuni iliyokuwa ikijihusisha na biashara ya mtandao ambapo mhusika hutoa kiasi cha fedha huku akiunganisha watu wengine ambapo kipato chake kwa maana ya faida itaongezeka mara kwa mara kwa kadiri anavyounganisha watu wengi

No comments: