tanzanitemovies blog is a blog that gives you the chance to know everything that happens in the movie industry. rahelimacdonald@gmail.com 0713-608524
Wednesday, November 5, 2014
MTOTO WA MUIGIZAJI KAJALA AWA GUMZO MLIMANI CITY..... INGIA USOME
SEXY lady wa filamu Bongo, Kajala Masanja hivi karibuni aligeuka gumzo yeye na mwanaye walipoenda kufanya ‘shopping’ Mlimani City ambapo watu walikuwa wakiwakodolea macho kwa jinsi alivyolingana na mtoto wake
Kajala alitinga eneo hilo na mtoto wake huyo aitwaye Paula ambapo awali walienda kupata chakula katika mgahawa wa SamakiSamaki na kisha waliingia ndani kwa ajili ya kufanya manunuzi mengine.
“Kwa kweli Kajala amekuza maana yeye na mtoto wake wamelingana sasa na mara nyingi kwa sasa hivi wanaongozana huku wakionekana kuwa na furaha wakati wote,” alisikika mtu mmoja akizungumza
Kajala alipozungumza na mwandishi wetu alisema kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama mtoto wake huyo na anapoongozana naye anazidi kufurahi zaidi
KAJALA NA MWANAE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment