Monday, November 3, 2014

MAMA YAKE WEMA SEPETU AFANYA BONGE LA SHEREHE LA KUFURAHI WEMA KUACHANA NA DIAMOND





CHEREKO chereko! Siku chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu kama ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo, Ijumaa Wikienda linashuka nayo mstari kwa mstari



TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.
“Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar,” kilisema chanzo hicho
 
SHEREHE ILIVYOKUWA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ‘menu’ ya ukweli kabisa, wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria.
“Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake, wakafungua shampeni, wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini,” kilisema chanzo hicho
 
 
MAMA WEMA ANENA Baada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga Diamond.
“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu,” alisema mama Wema
 
TUJIKUMBUSHE Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali walimwagana, wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo, wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema, sasa  wamemwagana tena
 
 
 
 
WAANDISHI WENZANGU PICHA ZA HIYO SHEREHE ZA MAMA WEMA ZIKO WAPI MAANA HAPA NAZIONA ZA BIRTHDAY YA DIAMOND NA YA WEMA TU.
 

No comments: