Sunday, November 2, 2014

EMBU SIKIA ACTO SHUH RUKH KHAN WA BOLLYWOOD ALIVYOTOA MPYA HUKO INDIA







Kama mnavyomuona hapo juu huyo ni the King of Bollywood movies anaitwa SHAH RUKH KHAN, wengi walianza kumjua kupitia movie yake ya KUCH KUCH HOTAE, basi unaambiwa hivi karibuni kumekuwa na ugomvi kati ya masuperstar wa movie India pamoja na wapiga picha yani ma paparazzi, inasemekana kwamba masuper star wamekuwa na nyodo mno kwa wapiga picha, yani superstar anaweza kuandaa event akawaalika wapiga picha akawaweka wamesimama baada ya lisaa li moja ndo anatokea na wakitaka kumpiga picha anakataa kwamba hana muda, basi jambo hili limewafanya wapiga picha kuzira kuwapiga picha baadhi ya ma super star, na juzi muigizaji mwingine anayeitwa SALMAN KHAN nae pia  alikuwa kwenye event moja baada ya wapiga picha kumuona wakawa wanataka kumpiga picha unaambiwa walinzi wa SALMAN wacha wawasukume vibaya hao wapiga picha kwa hiyo kitendo hicho kiliwafanya wapiga picha wachukie sana.



EH SASA SI NDO THE KING HIM SELF HAPO JUU AKAAMUA ACHANGAMKIE FURSA BWANA, unaambiwa juzi kawaaalika wapiga picha wote kwenye uzinduzi wa movie yake ya HAPPY NEW YEAR,  sasa wapiga picha walipigwa na butwaa baada ya kadi za mialiko kuwataka wapiga picha waje na familia zao zote kwenye hafla hiyo, basi unaambiwa walipiga picha SHUH RUKH KHAN za kumwaga, na wenyewe na familia yao walikula kunywa na kusaza,

KAMA WEWE NI CELEBRITY, MAKE SURE UNAKUWA NA UHUSIANO MZURI NA WATU WA HABARI, HAO NDO WANAOWEZA KUKUSHUSHA AU KUKUPANDISHA.

No comments: