Thursday, November 6, 2014

HEMBU USOME USHAURI WA BUSARA ALIOPEWA MAMA WA MUIGIZAJI WEMA SEPETU






HII ni mara yangu ya tatu nazungumza na mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu juu ya mwenendo wake kwa mwanaye, ambaye ana simulizi nyingi zinazomhusisha na mambo yaliyo nje ya fani yake ya uigizaji.
Wakati ule, ilikuwa ni juu ya tabia yake ya mara kwa mara ya kulizungumzia penzi la Wema na Diamond, kabla wawili hao hawajaachana kwa mara ya kwanza. Alikuwa akimpinga waziwazi kijana yule wa Tandale, kwa madai kuwa anampotezea muda mwanaye na mambo mengine kama hayo.
Nilijaribu kumweleza kwa jinsi gani ilikuwa haipendezi kwake kufuatilia sana mambo ya kimapenzi kwa watoto, maana ingawa anayo nafasi kubwa, lakini aina ya maisha ya siku hizi yanatoa nafasi kubwa zaidi kwa wahusika kuliko wazazi.
Lakini wakati akijipongeza kwa kufanikisha kuachana kwa wawili hao, ghafla wakarudiana na kumfanya mama mtu kuaibika, kwani ilionyesha wazi mwanaye alikuwa bado ana mapenzi kwa Baby wake, Diamond Platinumz


Na mara ya pili nilisema naye wakati alipomtukana matusi makubwa ya nguoni shoga wa zamani wa mwanaye, Kajala Masanja, katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wake. Ni matusi ambayo licha ya kuwa hayaandikiki gazetini, lakini pia nilimweleza jinsi gani alivyokosa busara za mzazi kwa kutamka maneno mazito kama yale, mbele ya watoto!
Safari hii, amerudia tena kosa ambalo nina uhakika, kwa tabia za mtoto wake, linaweza kumkuta akiabika tena kwa mara nyingine. Baada ya taarifa za kutengana tena kwa Wema na Diamond, mama huyu anaripotiwa kuwaalika marafiki zake kisha ‘kuangusha’ pati kushangilia kitendo hicho huku akikiri mbele ya magazeti kwamba ni kweli alifanya hivyo na kwamba, eti Diamond atajiju kwani hana hadhi ya kuwa na mwanaye

No comments: