Monday, November 17, 2014

MUIGIZAJI LULU MICHAEL TUNAKUPA HONGERA ZAKO





Juzi  nimeangali movie mpya ya Lulu ya MAPENZI YA MUNGU, yani kwanza kabisa Lulu jamani ni muigizaji mzuri mno, yani anajua kuuvaa uhusika hasa, yani nilifurahishwa mno na jinsi alivyocheza ile movie, mi sio shabiki sana wa Lulu lakini kwenye hii movie Lulu ameshanidaka nimekuwa shabiki wake hasa, na hivi ndo msanii anavyotakiwa awe, WATEKE MASHABIKI ZAKO KUPITIA KAZI ZAKO , yani msanii anapofanya kazi ikamfanya shabiki ampende hapo ndo kazi ya msanii inakuwa imepokelewa,
LICHA YA KUIGIZA SIKUJUA KWAMBA LULU UNASAUTI YA KUIMBA KIASI HIKI JAMANI, yani kwenye ile movie Lulu kaimba kwa sauti nzuri mno kupita hata wanamziki wengine,
MAMA KANUMBA; kwa upande wa mama Kanumba nilipenda alivyocheza na pia nimefurahi kumuona kwenye movie ila anahitaji kuzoea camera kidogo.


LINA; mwanamziki Lina nae amejitahidi japo nayeye anahitaji kujifua zaidi


yule aliyecheza kama mchungaji nilimpenda sana na yeye alicheza vizuri mno kwakweli,

2 comments:

Anonymous said...

Mbona dada huna washabiki kwenye blog yako, jitangaze

TANZANITE MOVIE said...

asante mpenzi nitajitangaza, ila mashabiki nawaona kupitia number of viewers wanaoingia kwa siku, lakini usihofu mpenzi nitaufanyia kazi ushauri wako