Friday, November 29, 2013

WEMA SEPETU BILA MARTIN KADINDA INAWEZEKANA.????


Wema ni muigiziaji wa bongo movies mwenye mafanikio makubwa, anaweza kuigiza na pia ni mrembo, kama ni mfuatiliaji mzuri wa reality show yake inayoitwa IN MY SHOES utagundua kitu kimoja, kwamba Wema anaweza akawa kawaida lakini baada ya dakika tano akageuka na kua mkali na kuanza kugomba hovyo, mara nyingi hali hii inapotokea Martin Kadinda mwanamitindo na maneger wa Wema huwa mstari wa mbele kumtuliza na Wema hutulia pale tu Martin akiingilia kati, na pia tunajua Martin ndio chachu kubwa sana ya maendeleo ya Wema, ameweza kumsimamia kwenye kila jambo, na licha ya kazi pia inaonekana hawa ni marafiki walioshibana, Martin kasimama na Wema kwenye shida na raha, hata magazeti na watu walipomkebehi Wema Martin alisimama nae, hata watu wanapomsema Martin kwamba kwanini anaambatana na mtu mwenye skendo kama Wema, still Martin hajawahi kumuacha,  sasa najiuliza, hivi bila Martin,Wema anaweza kusimama mwenyewe?

             ENDELEA KUANGALIA IN MY SHOES KILA JUMATANO SAA TATU NA NUSU EATV.

No comments: