Sunday, November 3, 2013

MUIGIZAJI ANALIPWA HELA NYINGI NIGERIA KULIKO WENGINE WOTE NI HUYU HAPA

inasemekana kwamba muigizaji MERCY JONSON wa Nigeria kapanda bei ghafla na kuwaacha hoi watengenezaji wa filamu nchini humo, hivi sasa hachukuliwi kucheza movie mpaka alipwe naira million 1.8, kwa hela hiyo ilivyo ndefu ndio imemfanya awe number moja kwa kuongoza kwa malipo, yani hapo hakuna cha GENEVIEVE wala OMOTOLA wala INI EDO. sasa basi shirikisho la filamu nchini humo limemfungia eti kwasababu kajipandishia bei kubwa, yeye kajibu kwamba kupitia mtandao wa twitter, kama mtu anajiona hawezi kumudu gharama zake akawachukue wa bei za chini na kama mtu atajiona atamudu basi atoe hilo dau na yeye atakua tayari kucheza nafasi yoyote ile. hata hivyo kwa dau hilo hilo MERCY amesha bookiwa na ma producer kadhaa kwa hyo anamovie kama nne hivi za kucheza naona adhabu yake itaanza kufanya kazi mwakani. MERCY  ni mama wa motto mmoja anayeitwa PURITY pia ni mke wa mfanyabiashara mmoja wa nchini humo... okay byeeeeeeni

No comments: