Monday, November 25, 2013

VIJIMAMBO VYA NIGERIA.

Huyu mwanamke mnayemuona hapo juu ni muigizaji wa Nigeria anaitwa Genevieve Nnaji, basi week iliyopita alionyesha picha kupicha kupitia mtandao wa instagram, picha hiyo ni hiyo hapo chini  yani ni picha ya simu aina ya Iphone yenye cover la dhahabu. weee hazijapita siku mwenzake kajibu mapigo.

                                             Gold cover ya simu ya Genevieve.
 
Basi jana muigizaji mwenzake na Genevieve anayeitwa Tonto Dokeh na yeye ni wa huko huko Nigeria, nae katupia picha kadhaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha na simu ya Iphone yenye cover la gold pamoja na diamond, picha hiyo imeonyesha kaishika hiyo simu huku kidole chake cha kati kakinyoosha( u know what I mean), sasa wachambuzi wa umbea wanasema hiyo middle finger kanyooshewa Genevieve aliyekua anajishaua na cover la Gold wakati yeye cover lake lina madini mawili Gold na Diamond.
 
TONTO DIKEH
 

 


Kwa kuziba watu midomo kabisa mwanadada huyo akatupia na saa ya Rolex kama mnavyoiona hapo chini. Anasubiriwa Ini edo nae ajibu mapigo.


                                        " AFRICA MOVIE ZINALIPA"......................

No comments: