huyu mschana ni muigizaji toka miaka ya 90 mwishoni katika kikundi cha kaole, anaitwa mainda, alishakua na uhusiano na mchekeshaji wa kikundi hicho cha kaole aliyekua akiitwa MAX ambaye kwa sasa ni marehemu, baada ya hapo akaanzisha mahusiano na ...........
na huyu kijana hapo juu, kijana huyu anaitwa Vincent Kigosi au jina la kisanii Ray, Ray na yeye ni msanii wa toka miaka hiyo na yeye alianzia kwenye kundi la kaole, uhusiano kati ya Mainda na Ray ulikua wa siri yani walikua wakisikika kwa nadra sana kwenye magazeti, sasa wakati wakiendelea, maisha nayo yakasonga, wasanii hawa wakaanza kujitafutia vipato zaidi na kujikita kwenye movie badala ya maigizo ya vikundi, huko Ray akakutana na..................
huyu dada hapo juu, yeye anaitwa Johari, na yeye pia kama Ray na Mainda walivyoanzia kaole na yeye alianzia kwenye kundi hilo la maigizo, basi miaka ilivyoenda tukasikia Ray na huyu Johari wameanzisha kampuni yao binafsi ya movie production inayoitwa RJ yani Ray&Johari, huku Ray akiwa ni mpenzi wa Mainda, naona mainda alijua wawili hao ni wanafanya tu kazi pamoja kumbe ni wapenzi pia kwa mujibu wa Mainda mwenyewe, sasa hawa wakawa na strong bond, kwasababu wanajitafutia maisha pamoja, shida zote wanapita pamoja, kama mjuavyo ilivyokazi kuifanya kampuni isimame lakini Johari alisimama na Ray mpaka kampuni ikaeleweka, ila sasa juzi kati tukasikia Johari kapigana na........................................
huyu dada hapo juu anayeitwa CHUCHU HANS, huyu dada yeye pia ni muigizaji wa movie japo yeye hakuanzia kaole, ila inasemekana ni mke na mama wa motto mmoja, basi kwa mujibu wa Mainda inasemekana huyu Chuchu na yeye pia anatembea na Ray. haya si maneno yangu ni story niliyoipata kwenye mahojiano ya mainda na muandshi wa global publisher. tazama mahojiano hayo hapo chini.
No comments:
Post a Comment