Saturday, November 30, 2013

SINTAH NDIE ALIYEMRITHISHA WEMA KUANDIKWA MAGAZETINI.

                                                            SINTAH
Enzi za Sintah zilikua balaa, huyu ni muigizaji wa siku nyingi, ingawa hivi sasa haigizi sana, Sintah miaka ya 2000 mwanzoni alikua tishio kuliko tunavyomuona Wema hivi sasa, yani kwa kipindi hicho Sintah ndo alikua anaongoza kwa kuandikwa kwenye magazeti kupita msanii yoyote, ndo msanii aliyekua akiuza magazeti kwa lugha nyingine, hivi sasa nafasi yake imeshikwa na Wema Sepetu.


                                         WEMA SEPETU
Wema ndie anayeng'aa kwa miaka ya hivi sasa, mpaka sasa nafasi yake bado haijukuliwa. ukifwatilia kwa ukaribu utagundua kwamba hakuna watu wanauza magazeti ya udaku kama wasanii wa movie,

Friday, November 29, 2013

WEMA SEPETU BILA MARTIN KADINDA INAWEZEKANA.????


Wema ni muigiziaji wa bongo movies mwenye mafanikio makubwa, anaweza kuigiza na pia ni mrembo, kama ni mfuatiliaji mzuri wa reality show yake inayoitwa IN MY SHOES utagundua kitu kimoja, kwamba Wema anaweza akawa kawaida lakini baada ya dakika tano akageuka na kua mkali na kuanza kugomba hovyo, mara nyingi hali hii inapotokea Martin Kadinda mwanamitindo na maneger wa Wema huwa mstari wa mbele kumtuliza na Wema hutulia pale tu Martin akiingilia kati, na pia tunajua Martin ndio chachu kubwa sana ya maendeleo ya Wema, ameweza kumsimamia kwenye kila jambo, na licha ya kazi pia inaonekana hawa ni marafiki walioshibana, Martin kasimama na Wema kwenye shida na raha, hata magazeti na watu walipomkebehi Wema Martin alisimama nae, hata watu wanapomsema Martin kwamba kwanini anaambatana na mtu mwenye skendo kama Wema, still Martin hajawahi kumuacha,  sasa najiuliza, hivi bila Martin,Wema anaweza kusimama mwenyewe?

             ENDELEA KUANGALIA IN MY SHOES KILA JUMATANO SAA TATU NA NUSU EATV.

MSANII MAINDA AWEKA WAZI YA RAY NA JOHARI + CHUCHU HANS

huyu mschana ni muigizaji toka miaka ya 90 mwishoni katika kikundi cha kaole, anaitwa mainda, alishakua na uhusiano na mchekeshaji wa kikundi hicho cha kaole aliyekua akiitwa MAX ambaye kwa sasa ni marehemu, baada ya hapo akaanzisha mahusiano na ...........


na huyu kijana hapo juu, kijana huyu anaitwa Vincent Kigosi au jina la kisanii Ray, Ray na yeye ni msanii wa toka miaka hiyo na yeye alianzia kwenye kundi la kaole, uhusiano kati ya Mainda na Ray ulikua wa siri yani walikua wakisikika kwa nadra sana kwenye magazeti, sasa wakati wakiendelea, maisha nayo yakasonga, wasanii hawa wakaanza kujitafutia vipato zaidi na  kujikita kwenye movie badala ya maigizo ya vikundi, huko Ray akakutana na..................

huyu dada hapo juu, yeye anaitwa Johari, na yeye pia kama Ray na Mainda walivyoanzia kaole na yeye alianzia kwenye kundi hilo la maigizo, basi miaka ilivyoenda tukasikia Ray na huyu Johari wameanzisha kampuni yao binafsi ya movie production inayoitwa RJ yani Ray&Johari, huku Ray akiwa ni mpenzi wa Mainda, naona mainda alijua wawili hao ni wanafanya tu kazi pamoja kumbe ni wapenzi pia kwa mujibu wa Mainda mwenyewe, sasa hawa wakawa na strong bond, kwasababu wanajitafutia maisha pamoja, shida zote wanapita pamoja, kama mjuavyo ilivyokazi kuifanya kampuni isimame lakini Johari alisimama na Ray mpaka kampuni ikaeleweka, ila sasa juzi kati tukasikia Johari kapigana na........................................

huyu dada hapo juu anayeitwa CHUCHU HANS, huyu dada yeye pia ni muigizaji wa movie japo yeye hakuanzia kaole, ila inasemekana ni mke na mama wa motto mmoja, basi kwa mujibu wa Mainda inasemekana huyu Chuchu na yeye pia anatembea na Ray. haya si maneno yangu ni story niliyoipata kwenye mahojiano ya mainda na muandshi wa global publisher. tazama mahojiano hayo hapo chini.
 


                

Thursday, November 28, 2013

JACKLINE WOLPER........mmmhhhhhhh



Hii ni video inayoonyesha mahojiano kati ya muigizaji mrembo wa Tanzania Jackline Wolper na muandishi wa habari, kwenye haya mahojiano, Wolper amefunguka kuhusu maisha yake na baadhi ya wanaume aliowahi kutembea nao, katika list hiyo yumo Aly Kiba ambae ni mwanamziki, Jux ambaye pia ni mwanamziki, Diamond ambae pia ni mwanamziki pamoja na Dalas ambaye ni mfanyabiashara, Wolper pia amekiri kwamba anayempenzi ila hawezi kumuweka wazi kutokana na yaliyomkuta kwa Dalas, kwanza kabisa huyo mpenzi wa sasa anajisikiaje Wolper anavyoorodhesha wanaume aliowahi kua nao, huku akielezea jinsi alivyowapenda, na kwenye maelezo kuna mapungufu mengi mwenye akili anaweza kumsoma Wolper ni mschana wa aina gani kupitiaa mahojiano hayo, inawezekana huyo mpenzi wa sasa hana neno na haya maelezo, ila kubwa kuliko ni kwamba, zamani Diamond kipindi hicho ndo alikua anaanza kutoka kimziki aliwahi kukiri kua alikua na mahusiano na Wolper, tuhuma ambazo Wolper alizikataa na kusema maneno ya kashfa sana, miaka imeenda na sasa Diamond ndie mwanamziki pekee anayelipwa fedha nyingi Tanzania, na  ndo mwanamziki namba moja kwa sasa hapa nchini na licha ya hivyo Diamond hivi sasa anapesa ndefu kidogo, sasa kinachoshangaza ni jinsi Wolper alivyokiri hivi sasa kwamba alishakua na mahusiano na Diamond, swali, je amekiri kutokana na mafanikio aliyonayo Diamond hivi sasa? kwamba na yeye ataonekana yumo? manake kama mwanzo alimkashifu ni nini kimemfanya akubali sasa hivi? swali lingine, je Diamond angekua choka mbaya bado Wolper angekiri kwamba alishakua na mahusiano naye au bado angemkashifu? NI HAYO TU.

Wednesday, November 27, 2013

Tuesday, November 26, 2013

ANGELINA JOLIE AFANYA KUFURU

huyu ni mwanamama muigizaji wa Marekani anaitwa Angelina Jolie na wa pembeni ni mumewe anaitwa Brad Pitt ambaye pia ni muigizaji mahili. na ukitaka kuona movie yao ya pamoja inaitwa MR&MRS SMITH.
basi inasemekana Brad anatajarijia kusherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni, na mkewe akaamua kumsuprise kwa zawadi matata, manake ukiangalia hawa wote ni matajiri wa kutosha kwa hiyo wakitaka kununuliana zawadi ni lazima zawadi iwe ya tofauti ukizingatia wanauwezo wa kununua chochote duniani.

basi ma girl Angie akaamua kumnunulia mumewe hichi kisiwa ambacho bei yake ni dola million 20, unaambiwa kisiwa hichi kiko very private, kwenye hichi kisiwa kuna jumba zuri linaloweza kukufanya ujisikie hauko duniani uko peponi, hizo hapo chini ni baadhi tu ya picha za jumba hilo linavyoonekana kwa ndani.




haya na WEMA sijui atamnunulia nini Diamond ikifika birthday yake.

Monday, November 25, 2013

STRONG COUPLE,

Huyu dada ni muigizaji wa Marekani anaitwa Grabriela Union, ni mwanamke mwenye miaka 40 ila anaonekana anamiaka 25, na huyo kaka ni mcheza basket lakini pia ni boyfriend wa Gabriela, jamaa anaitwa Dewyane Wade, na huyo dada kampita huyu jamaa miaka 10.





VIJIMAMBO VYA NIGERIA.

Huyu mwanamke mnayemuona hapo juu ni muigizaji wa Nigeria anaitwa Genevieve Nnaji, basi week iliyopita alionyesha picha kupicha kupitia mtandao wa instagram, picha hiyo ni hiyo hapo chini  yani ni picha ya simu aina ya Iphone yenye cover la dhahabu. weee hazijapita siku mwenzake kajibu mapigo.

                                             Gold cover ya simu ya Genevieve.
 
Basi jana muigizaji mwenzake na Genevieve anayeitwa Tonto Dokeh na yeye ni wa huko huko Nigeria, nae katupia picha kadhaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha na simu ya Iphone yenye cover la gold pamoja na diamond, picha hiyo imeonyesha kaishika hiyo simu huku kidole chake cha kati kakinyoosha( u know what I mean), sasa wachambuzi wa umbea wanasema hiyo middle finger kanyooshewa Genevieve aliyekua anajishaua na cover la Gold wakati yeye cover lake lina madini mawili Gold na Diamond.
 
TONTO DIKEH
 

 


Kwa kuziba watu midomo kabisa mwanadada huyo akatupia na saa ya Rolex kama mnavyoiona hapo chini. Anasubiriwa Ini edo nae ajibu mapigo.


                                        " AFRICA MOVIE ZINALIPA"......................

THE HUNGER GAMES,


Friday, November 22, 2013

OLD IS GOLD. VAN DAMME NDANI YA TANGAZO LA VOLVO


 

Jamaa anamiaka 53 bado anamudu kupiga msamba, huyo ni muigizaji wa Enzi hizo VAN DAMME au kwa jina lake halisi JEAN CLAUDE, jamaa alitamba sana na movie zake miaka ya 90, movie kama SYBOG na UNIVERSAL SOLDIER ZILIKUWAGA TISHIO ENZI HIZO.

MOVIE ZINALIPA NIGERIA

Muigiza wa Nigeria Jim Iyke juzi alimpeleka girlfriend wake Ulaya kwenda kusherehekea birthday ya mschana huyo, binti huyo anaitwa Nadia Buari ni muigizaji wa Ghana.
Hapa kidume Jim akajikakamua mpaka akapata limo huko Spain. akakodisha na kumpakia Nadia mpaka kwenye restaurant

 hapo wakiwa kwenye restaurant nadia akiimbiwa  happy birthday.

 hapa wakienda kutembelea maeneo ya kihistoria huko Spain

 
hawa wote ni waigizaji, kwa Tanzania hakuna muigizaji aliyewahi kujaribu kufanya kufuru za fedha nchi za watu, ila kwa Nigeria na Ghana ni kawaida kuwaona wasanii wao wakienda mapumziko nchi mbalimbali, hapa kwetu nilimuona Wema tu kaenda Zanzibar.

HAWA WANGEBAKI NA RANGI ZAO WANGEKUA TISHIO......

                                                      BATULI
 
 
                                  WEMA SEPETU.

Hawa waschana ni wazuri sana wana sura na maumbo mazuri, kama wangebaki na zile rangi zao za zamani sijui ingekuaje.

Thursday, November 21, 2013

MOVIE YA BEYONCE OBSESSED

 Huyu ni muigizaji Beyoncé Knowles, wengi wanamjua kama mwanamziki lakini ndani ya bloh hii ni muigizaji kwani ameshacheza movie kadhaa na mojawapo au niseme movie yake ya kwanza kucheza kama kinara wa movie ni hii movie inayoitwa OBSESSED,

kwenye hii movie Beyoncé amecheza na muigizaji wa uingereza Idris Elba, inahusu maisha ya wanandoa wanaopendana na wanamtoto mmoja halafu baadae penzi lao linaingiliwa na mdada wa mjini.

picha hii inamuonyesha Beyoncé na Idris Elba wakiwa wanaigiza hiyo movie


hizi picha zote ni za hiyo movie ya OBSESSED.
 
 
SASA BASI, HAPO CHINI NIMESHARE NA NYIE VIDEO KUTOKA U TUBE INAYOMUONYESHA MTOTO WA MIAKA MI 2 WA HUKO MAREKANI ANAYEITWA HEVEN, KATOTO HAKO KANACHEZA WIMBO WA BEYONCE KAMA VILE BEYONCE ANAVYOCHEZA, YANI HAKAJAKOSEA HATA STEP MOJA, UKIKAANGALIA KWANZA NI KADOGO LAKINI KANAVYOCHEZA UTASHANGAA, ILA HAKA KATOTO MAMA YAKE NI CHOREOGRAPHER.
 

WEMA SEPETU AKIIMBA.....


inasemekana kwamba waigizaji wengi pia wamebarikiwa sauti ya kuimba, huyu ni WEMA SEPETU na hapa anaonyesha kipaji kingine alichojaliwa na mwenyezi Mungu,

GENEVIEVE NNAJI ANAMILIKI IPHONE YENYE COVER LA DHAHABU.,



 
 
 
Muigizaji kutoka Nigeria Genevieve Nnaji anamiliki simu aina ya Iphone yenye cover la dhahabu tupu, Genevieve ni star mwenye mafanikio makubwa sana barani Africa, life style yake ni ya kisuperstar, mijengo yake, safari za mapumziko ya nchi za nje mara kwa mara, mavazi,viatu na mikoba ya ma designers wakubwa duniani ni vitu vya kawaida kwa Gene, kweli kumbe movie zinalipa na Africa pia,