Sunday, November 30, 2014

MANGE KIMAMBI KWENYE HILI SWALA LA DIAMOND PLATNUMZ NI BIG NOOOO

Mange kwanza mi nishabiki yako namba moja dada yangu, KWANZA KWENYE HII POST NINGEPENDA UMPE HONGERA ZAKE DIAMOND KWA KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA HALAFU NDO USHUKE NA OPINION ZAKO.maana kikubwa hapa ni ushindi wa Diamond haya mengine ni maisha yake private,
                                                
                        DIAMOND AKIWA NA ZARI
A


B
 
MANENO YA MANGE HAYO HAPO CHINI
 
Diamond akiwa na Zari na mamake….
Dah,yani Wema akirudi tena kwenye hii familia basi ntaamini maneno ya mama yake kuwa kalogwa….
Hapana aiseee,,,Wema pls move on jamani, maana sasa mtaleteana magojwa jamani….. KHA!!!!
IMG_5627
MANENO YA MANGE HAPO CHINI,
Uwiiii Mama Diamond akiwa na mkwe wake mpya Bi Zari…..
Hapana jamani huyu mama ni too much sasa,,,uwiiiii…
Hivi tuseme bahati mbaya Diamond apate ngoma sasa hivi hivi mamake si inabidi alaumiwe jamani…
THis is too much now jamani huyu mama, hapana aisee. Hata kama mwanao ndo anakulisha na kukulisha kuna ujinga mwingine inabidi
umkanye mwanao jamani… Yani mama kutwa uko benet na mabibi wa mwanao,, hivi is this normal jamani?? Labda mie mshamba,
Kiruuuuuu….Nimeshindwa kushangaaa jamani
 
 
MAONI YANGU: kwa nionavyo mimi Rachel, Diamond ni kijana mkubwa ambaye kavuka miaka kumi na nae, licha ya hiivyo, Diamond alikuwa single kabla ya kukutana na Zari yani hakumcheat mtu hapo bali aliachwa akawa single na sasa kapata girlf mwingine, Mama DIAMOND hana kosa lolote, kama Diamond angekuwa kijana chini ya miaka 18 ningesema mama huyu anamakosa, lakini Diamond ni kijana mkubwa, anamaamuzi na maisha yake, huyu mama asiweza kukataa kwenda Afrika Kusini kusherekea ushindi wa mwanae eti kisa Zari atakuwepo hata ingekuwa wewe dada yangu usingesusia ushindi wa Kenzo eti kisa girlf hilo haliwezekani, embu kabla hatujamshambulia mama wa watu MUACHENI MSIKIE AKITAMKA KUTOKA MDOMONI MWAKE MANENO YA KUMKASHIFU WEMA NA KUMPENDA ZARI HAPO NDO TUANZE KUMSHAMBULIA MAMA WA WATU, LAKINI MAMA WA WATU HAJATOA LE TAMKOZ LOLOTE ZAIDI YA KUKAA KIMYA TU BASI TUHESHMU HILO, MBONA MAMA WEMA ALITOA LE TAMKOZ KWENYE BIRTDAY KUHUSU KAJALA WATU WALINYAMAZA NA WAKATI HAKUTENDA HAKI KABISA, mi naona tumuheshimu mzazi wa mwenzetu kama ambavyo tunataka wazazi wetu waheshimiwe, vijana wengi kabla ya kuoaa hupeleka waschana kwa wazazi Diamond sio wa kwanza tena huko ulaya ndo balaa zaidi, Wema na Diamond ni wasanii wanaopendwa sana embu tu concentrate na kazi zao habari za mapenzi yao tuziache maana tutaabika baadae hasa ukizingatia ni lazima watarudiana .
 
 
BAADHI YA COMMENT ZA WADAU WA MANGE KIMAMBI.
 
 
Ukisha fikisha 18 wewe ni mtu mzima , sidhani ni sahihi kusema akipata ngoma mamake ndo alaumiwe Chibu ni mtu mzima n let him make mistakes hayakuhusu.
Na hayo ya magonjwa ungeanza kumwambia mdogo wako.
Mange najua unasema kama blogger ila you sound too personal n judgemental tokea hili saga la hawa lianze by the way si ulisema Wema anajua the whole project?
Inachekesha mlisema anasafiria nyota ya nani? mkazila na kupiga kura.
Anyway hakuna cha kurogwa wala nini mmesahau Enzi zile anaburuzwa na mamake kutoka kwa mbangi bangi wake Jumbe na Kanumba mpaka kupelekana polisi?
Kama Diamond na bibie ni couple mimi naona ndo itakuwa woke up call ya huyu Wema kutoka dunia yake ya kusadikika.Hongera Diamond na Wema move on na its not too let not too early ur young and beautiful u can do it wish u all the best.
Akiwa kris Jenner au Madonna mnamuita wow ila Zari ndo Malaya , haki sawa kwa wote kama vibabu vinachukua vitoto kwani wanawake tatizo liko wapi
 
Olga
You have said it all mkirando,apa naomba nipingane na wewe CEO.diamond kupendana na zari kutamfumbua sana macho wema,uvivu wote utamuishia,atachapaje kazi sasa,atakuwaje classic,manake sasa ivi ni mwendo wa kushindana na zari.hata diamond na familia yake wata advance.mama chibu na halima kimwana kizungu lazima kipande,diamond mmemuona alivyokuwa na confidence sasa ivi?muacheni Jamani,mambo ya magonjwa tunamuachia mungu,wanaokufa na ukimwi wote si wazinifu,tena wazinifu.Go Go Diamond,we ni level nyingine sasa ivi,sio wa kulinganishwa na kina Ali kiba tena

Bado namuheshimu mama Diamond…ni bonge la mzungu…Diamond ni mtu mzima…ya nini kununiana na mwanao ukamtie mikosi eti kisa ana date mtu usomtaka…mbona alivyomkubali Wema hamkusema wakati kwa mama mnoko Wema asingetia mguu kwa huyu mama…
Ikija kwa Zari ndio mnamshangaa…
Mimi naona ni mama tu anaye mind her own business ili mwanae afanye analoona linamfaa
Marichui
Reply
Diamond anastress jamani , kama ni kweli ugomvi wao ulikuwa ile gari nyeupe aliyepewa wema kwenye birthday hebu tujiulize ki ukweliiiii kabisa kama Diamond alifikia hatua ya uchumba , Bi Wema kupewa gari na watu/mtu mwingine kama suprize tena kwa wakati hot kama waliokuwa nao haikumake sense! Wema naye kicheche hajatulia bwana hivi Mwanaume Gani mwenye akili timamu hata kama boyfriend tu ashuhudie unapewa Gari ya thamani Live mbele yake bila maelezo ya kueleweka ??? Nop Wema anamatatizo sana ….anaentatain unnecessary issues ambazo zinamuweka pabaya vilevile , ni kweli Diamond hakuwahi kukuoa ila ukishaamua kujiengage na mtu hivyo heshima na utu lazima uwepo ! halafu Bila haya eti ukakimbilia kwa Penny kupatana na kupiga vipichapicha vyenu vya ajabu mnamkomesha nani ?unajichora tu ! Wewe Mtoto wa kike wewe unaishi sana Maisha ya kwenye TV Kwa kucopy toka kwa Kim K ! Yaani naandika hii comment huku machozi yananitoka Wema Jitambue , ungejua kiasi gani unapendwa na watu wa kila rika ungetuheshimu lakini wala hutujali hisia zetu ,ingawa hatujawahi kuona hizo picha za Vibabu vyako wanavyosema ila kwa Mazawadi Makubwamakubwa tunayoshuhudia unaonekana hata wewe unachiti sana !! Maisha ni kuchagua tu Mwanangu , Kama umeamua kuchuna basi wachune hasa hao wazee wa Escrow, hasa ufanye mambo yako fasta , ikiwezekana tafuta mmoja uolewe kama Mama Machache
mkirando
Reply
Embu kwendeni huko , mnajifanya mna maadili kumbe yakinafiki tuu, mtu kaachwa mnataka mtoto wa kiume ajichue na neck massager ya Mange ama?
Kwahiyo mnaona ni bora atiane lakini kwa siri? no wonder ukimwi haushi . Diamond watie tuu si wanajileta wenyewe ulivyokuwa choka mbaya walikuita ndomo watie mpaka watie akili wewe tumia kinga basi ndo cha muhimu eti anadhalilisha wanawake , mnajizalilisha nyie na ujinga wenu mbona hajaja kumtia mfano Mange ni sababu anajiheshimu , mnapeleka K zenu wenyewe mijimama mizima hafu leo ndo mseme anawazalilisha? aliyerekodi si huyo Penny na kuzomea si alizomea Joketi na Andunje wake ni wanaume hao? si wanawake, mnakera , the kid ndo kwanza 25 asipofanya leo aje kufanya akiwa na 50 kaa lile bonge nyanya ama

Jamani tuache kumuonea huyu dogo hata km ana yake yaani Mange umeshindwa kabisa kusema chichote kwa mtz mwenzio umeona ya mama yake tu? Kwanza hata ukimuona huyo mama hapo usi hauonyeshi furaha hivyo, na tusisahau kuwa Wema kapata pedeshee kamuacha Almas, sasa afanyaje? Akae alie? Akichukua rafiki wa Wema tunamponda, akichukua waliomzidi umri tunaponda muacheni kijana wa watu yupo kwenye kujitafuta maana hakutrgemea kibuti cha dizaini ile. Kingeni Mange we ni blogger ungemshauri na mama Wema hamshauri mwanae kwa anayofanya na husiseme hajui maana anajua mpk kwenye video anawachapa waliomchukulia mwanae ck na diamond kulala kitanda alichonunua Ck ila mama yuko happy mwanae kulala na waume za watu. Mange nakupenda ila hata kama unamchukia mtu sio kihivyo halafu huyo unayemteteaga mwenyewe yanaingia huku na kutoka huku mwisho anarudi pale pale. Kama Wema hasirudi kwa Almas basi na Almas hasirudi kwa Wema maana mama Almas pia hafurahi kuwa na mkwe kiruka njia na ni kawaida mwanamke stara babu, sio kupanua miguu kwa kila atakaye.. Muweke pia Wema tumpe laivu sio kila siku Mtoto wa watu tu..NB: acha kuingilia mapenzi ya Wema na Diamond maana huwa unakuwa disappoited kila siku

diamond hamkomoi wema kumbuka wema ndo alibwaga manyanga diamond amemove on sasa tatizo liko wapi? angekuwa diamond ndo kam mwaga wema sijui ingekuwaje.
diamond ni mtu mzima anajua mbovu na mbichi mama sandra wa watu acheni ajilie kivulini maana alichumia juani nani hapendi kula bata? ukizingatia ulikuwa unazuza mkaa vitumbua mwanao ale leo hii unapandishwa pipa business class halafu ninii? eeh bwana eeh tusidanganyane kila mtu anapenda raha maisha yenyewe mafupi.
jlo alimuacha mume wake wa ndoa akaenda kudate kile kitoto kakizidi miaka 20 hakuna mtu aliongea zaidi ya kuwawish lucky wenye mahusiano yao. kubwa la maadui chriss jenner ye ndo kaua kabisa kamuacha hubby wake wa 23 years kachukua kitu black kama mwaye kim tena kamzidi miaka 18 jamani tuwaacheni tu ndo wameamua iwe hivyo.
mbona huku kwetu mabinti wadogo wanadate babu zao halafu kutwa mnawasifia she is so blessed yuko juu bla blaa. watajijua wenyewe kama wana act au wana date kimpango wao. mange ugeachana na hawa watu maana sasa unakuwa kama uko obsessive na hii couple move on maa get used with it mbona mama mzaa chema mwenyewe kauchuna, wapotezee tu usijeonekana unaona gere bure



HAYA HIZO HAPO JUU NI BAADHI ZA COMMENT KUTOKA KWENYE BLOG YA MANGE. Mange jamani mimi ni msomaji wako mzuri tu wa blog kwa hyo kukukosoa hapa sio kwamba nina chuki na wewe ila kama binadamu muda mwingine maoni yanatofautiana, pia Wema mimi nishabiki wake number one na nampenda jinsi ambavyo hukaa kimya yanapotokea mambo kama haya, kwa hiyo kama ambavyo Wema kaka kimya ingependeza na sisi tukakaa kimya, kama ambavyo Wema kampa hongera Diamond kwa ushindi ingependeza na sisi tukampa hongera Chibu kwa ushindi wake, hayo mengine tuwaachie wenyewe, manake tukichukia kwanini mama Diamond kampokea Zari kwanini tusingechukia kwanini mama Diamond kampokea Wema kipindi kile Diamond kamuacha penny, tena ndo tulitakiwa tumkosoe Diamond kwasababu alikuwa anamcheat[enny na Wema, si bora safari hii Dimond aliachwa ndo akaenda kwa Zari kuliko kipindi kile Diamond alikuwa hajaachwa na Penny ila akaenda kwa Wema na watu tukashangilia. WEMA NA DIAMOND WAKIGOMBANA TUBEBE MAJEMBE TUKALIME WAKIPATANA TUSHIKE VIKAPU TUKAVUNE..

Saturday, November 29, 2014

LULU MSANII WA PILI WA MAIGIZO KUKIRI KUWAHI KUBAKWA ...






My confession! (kukiri kwangu)! Mwanadada mwenye taito ya utangazaji na uigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefungua kinywa na kutoa la moyoni akisimulia tukio baya lililowahi kumkuta la jinsi alivyobakwa, Risasi Jumamosi lina ‘exclusive story’
TUJIUNGE DUKANI KWAKE
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni dukani kwake Kinondoni jijini Dar, Aunty Lulu asiyeishiwa na vimbwanga alisema kwamba, kamwe hawezi kusahau tukio hilo maishani mwake.
ALIBAKWA NA RAFIKI WA SHEMEJI YAKE
Aunty Lulu aliyeng’ara kwenye Sinema ya Lost Soul alieleza namna alivyobakwa na rafiki wa shemeji yake (rafiki wa mume wa dada yake) na kumpotezea ndoto zake za kuanza mchezo huo akiwa ndani ya ndoa.
Akieleza kwa uchungu na masikitiko, Aunty Lulu alitiririka kwamba, alikuwa akiishi kwa dada yake ambapo rafiki wa mume wa dada yake huyo alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani kila wakati alipokuwa akifanya kazi maeneo ya Posta jijini Dar
KISUTU SEKONDARI
Aunt Lulu alisema kwamba wakati huo, yeye alikuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Kisutu, Dar, hivyo kila siku jioni mwanaume huyo alikuwa akimpitia na kumpa lifti hadi nyumbani.
Aliendelea kusema kwamba, siku moja jamaa huyo aliyekuwa amemzidi umri maradufu alimtaka wafanye mapenzi lakini alimkatalia kwa madai kwamba hakuwahi kufanya mchezo huo mbaya ambao alifundishwa kuwa ni dhambi.
TUKIO BLOCK 41
“Kwa kawaida yule jamaa alikuwa akinifikisha nyumbani kwa dada yangu pale Makumbusho (Dar), ananisubiri, nabadilisha nguo, naenda naye kwake maeneo ya Block 41 (Kinondoni) ambako alikuwa akinifundisha. So alinibakia nyumbani kwake,” alisema Aunty Lulu, mtangazaji wa zamani wa ITV na C2C
MAUMIVU MAKALI
Staa huyo aliendelea kutiririka kwamba alipomwambia kuwa hajawahi kufanya kitendo hicho, mwanaume huyo alimwambia haamini ndipo akamkamata kinguvu na kumpeleka chumbani kwake kisha akamwingilia na kumsababishia maumivu makali. “Kwa kuwa niliumia sana, nilikuwa natembea kwa shida hivyo dada yangu aligundua.
AGOMA KUTAJA MWANAUME
“Ilibidi dada anibane kujua nina tatizo gani. Kwa kuwa nilikuwa sina ujanja nilimwambia nimeingiliwa kwa mara ya kwanza lakini nilisita kumtaja mwanaume huyo.
“Dada aliponibana sana nilimwambia kwamba niliingiliwa na huyo rafiki wa mume wake.
INASIKITISHA
“Lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana na ukweli liliwaumiza sana dada na shemeji yangu.
“Walimsema sana mwanaume huyo na ikawa ndiyo mwisho wa urafiki wao
ALIKUWA NA UMRI GANI?
“Umri sikumbuki lakini nakumbuka nilikuwa nakaribia kuingia kidato cha nne. Yule mwanaume alizoea kuninunulia vifaa vya shule na kunisisitiza kusoma.
“Nilimuona mtu bora sana, nikamzoea na ikawa rahisi kwenda kwake kusoma maana jamaa alikuwa ‘jiniazi’ na mwanzoni alikuwa jirani yetu kabla ya kuhama.
“Ukweli huwa sipendi kuelezea historia ya maisha yangu ya mapenzi kwani inaniumiza sana.
AMPOTEZEA NDOTO YA KUOLEWA
“Huwa najisikia kulia kwa sababu huyo rafiki wa shemeji yangu alinipotezea ndoto nilizokuwa nazo kwamba nitafanya juu chini niolewe nikiwa ‘mbichi’ hivyo mapenzi ningefanya nikiwa ndani ya ndoa.
“Sikufurahia kabisa kitendo hicho maana naona pia kiliniathiri kisaikolojia,” alisema Aunty Lulu
YUPO WAPI MWANAUME HUYO?“Baada ya tukio lile aliomba anioe ili nimsamehe lakini nilikataa. Baadaye alikwenda kusoma nje ndipo tukapotezana na sijawahi kumuona tena, nasimulia ili liwe fundisho kwa wanawake wanaopenda kuwa na ukaribu kupitiliza na wanaume wasiowajua kiundani,” aliweka nukta Aunty Lulu


BAADA YA SHILOLE KUWAHI KUTOA HISTORIA YAKE YA KUSIKITISHA YA KUBAKWA AKIWA BINTI MDOGO NA KUPATA UJAUZITO WA MMBAKAJI, LULU SEMANGO NAYE KAMA MLIVYOSOMA STORY HAPO JUU NAE KAFUNGUKA.JAMANI WABAKAJI MLAANIWE KWAKWELI MAANA UBAKAJI NI SAWA NA UUAJI , NA HUMUATHIRI MTU KISAIKOLOJIA MAISHA YAKE YOTE,

Wednesday, November 26, 2014

MUIGIZAJI LULU MICHAEL NA SKENDO YA MKANDA WA KUCHEZA UCHI.

                                                      LULU MICHAEL

Hivi majuzi ilitokea hali ya sintofahamu kwa muda kadhaa baada ya habari kuenea kwamba video ya Lulu akiwa anacheza uchi imezagaa , baada ya muda video hiyo ilikuwa imeshasambaa lakini KUMBE HAKUWA LULU MICHAEL HUYU bali ni mschana anayeitwa LULU ambaye ni mpenzi wa mwanamziki dogo ASLAY wa kundi la YAMOTO BAND, mschana huyo aitwae lulu alirekodiwa video hiyo na mchepuko wake kwani inasemekana wakati anarekodiwa akicheza wimbo wa yamoto band huku akiwa uchi wa mnyama hakuwa na boyfriend wake wa siku zote Aslay bali alikuwa na jamaa anayefahamika kwa jina la Rummy.
Lulu Michael wa bongo movies hakuacha hili swala lipite kwani kupitia account yake ya instagram aliamua kukanusha na kusema kwamba wakina Lulu wako wengi Tanzania kwa hiyo mwenye video hiyo sio yeye na yeye kamwe hawezi kukubali mwanaume amfanyie huo uchafu,

ANYWAY TUNASHUKURU HAKUWA MDOGO WETU LULU MICHAEL MAANA BONGO MOVIE HUWA INAKASHFA SANA SASA NDO KWAMFANO HILI SAKATA LINGEMKUTA LULU WETU NAHISI BONGO MOVIE NDO INGEZARAULIKA MARA MBILI ILA HIVI SASA NAONA WASCHANA WENGI WA BONGO MOVIES WANAJIELEWA NA KUJIHESHIMU.

NANI KATOKELEZEA KATI YA WEMA SEPETU NA PENNY MUNGILWA.


WAKE WENZA WA ZAMANI WAMETOKELEZEA NA SARE SARE NAFIKIRI WALIKUWA WANAKWENDA KWENYE KITCHEN PARTY, NANI KATOKELEZEA ZAIDI YA MWENZAKE? YANI NGUO YA NANI IMESHONWA VIZURI, MAKE UP YA NANI IMEKAA VIZURI, NA MTINDO WA NANI WA NYWELE UMEKAA VIZURI.

NGUO HIZI ZILIDESIGNIWA NA KIKI .

WEMA AMWAGA CHOZI KISA KIKIWA NI PICHA YA DIAMOND AKIMBUSU ZARI

              WEMA SEPETU                                                          ZARINAH HASAN
                                  DIAMOND AKIMAHABIKA NA ZARI
Eti kuna chanzo ambacho kipo karibu na Wema kinadai kwamba Wema alipoiona hiyo picha ya Zari na Diamond wakimahabika eti alidondosha chozi, inasemekana eti Wema ghafla alitetemeka na kuanza kulia  hasa ikizingatiwa mwanzo kulikuwa hakuna uhakika kama kweli Diamond kamahabika na Zari ilikuwa inasemekana wanaproject tu eh sasa ushahidi wa picha ulipotoka ndio kila mtu akiwemo na Wema pia ndo wameamini kwamba watu hawa wazee wa LE PROJECT kumbe walifanya project zote duniani.

CHANZO CHA NEWS SWAHILIWP.

SIKIA KISA CHA MENINA NA ANAYEDAIWA KUWA MGANGA WAKE.

MENINA HASIMU WA MUIGIZAJI WEMA SEPETU


Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye aliyemng’arisha
Kwa mujibu wa chanzo makini, mganga huyo amekuwa akimfanyia ndumba msanii huyo ili arudiane na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinum’.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mganga huyo amekuwa akidai kwamba, huwa msanii huyo anatinga nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar kisha kumlilia shida yake akimtaka afanye juu chini kuhakikisha anamrudisha Diamond mikononi mwakestaa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ hivyo kutoa siri nzito ambayo wengi hawakuijua

Baada ya kukisikia chanzo hicho, waandishi wetu walikwenda nyumbani kwa mganga huyo na walipomuuliza ishu hiyo alikiri Meninah kufika kwake ili kufanyiwa ndumba arudiane na Diamond.

“Yule msanii anayeitwa Meninah ambaye habari zilivuma kuwa anatoka na Diamond na kukanusha, huwa anakuja hapa kufuata tiba na kikubwa anachokitaka anataka nimvute Diamond ili warudiane,” alisema.
Meninah alipoulizwa kuhusu madai hayo aliruka kimanga na kudai hakuwahi kuwa na uhusiano na Diamond na wala hamjui mganga huyo

Tuesday, November 25, 2014

MUIGIZAJI DOCTOR CHENI ANYWESHWA SUMU.




Staa wa kiume wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, kwa mara nyingine alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar baada ya kudaiwa kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu (poisonous food
Akizungumza na mwandishi wetu wikiendi iliyopita Dk Cheni alisema kuwa alikuwa mshehereshaji (MC) kwenye harusi moja iliyofanyika maeneo ya Sinza jijini Dar ndipo akala chakula hicho ambapo muda mfupi baadaye alianza kujisikia vibaya ‘kichina’.
Staa huyo alisema kuwa baada ya hatua chache kutoka ukumbini, tumbo lilianza kumuuma kisha akaishiwa nguvu ndipo akaweka gari pembeni na kupiga simu kwa ndugu kuomba msaada.
Dk Cheni aliendelea kueleza kuwa baada ya kupata msaada moja kwa moja alipelekwa kwenye Hospitali ya Burhani jijini Dar
Alisema kuwa baadaye alihamishiwa kwenye Hospitali ya TMJ ambapo madaktari walipompima waligundua alikuwa amekula chakula chenye sumu ndipo wakampatia matibabu na kulazwa.
Alisema siku ya pili yake aliruhusiwa huku akisema kitendo hicho kimemsikitisha mno.
Siyo mara ya kwanza kwa Dk Cheni kulishwa chakula chenye sumu kwani safari hii ni mara ya pili ambapo mwaka jana alilazwa tena kwa ishu kama hiyo, jambo ambalo haelewi kwa nini inakuwa hivyo

UNAAMBIWA IRTHDAY YA BABY MADAHA UCHAFU ASILIMIA 85




SHEREHE ya siku ya kuzaliwa ya msanii wa muziki na filamu, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ilitawaliwa na vitendo vichafu mwanzo mwisho
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wachache wakiwemo baadhi ya wasanii, ilifanyika katika Grosari moja iliyopo Kijitonyama.Miongoni mwa mastaa waliohudhuria alikuwa ni mcheza soka wa zamani wa timu ya Yanga ya jijini Dar, Samson  Mwamanda.
Sherehe hiyo iliyoanza mishale ya saa 6.00 usiku ilitawaliwa na vituko kibao vilivyowaacha midomo wazi baadhi ya wahudhuriaji.Moja ya vituko hivyo ni pale Baby Madaha aliyekuwa amekolea kwa kilevi alipoamua kupigana denda laivu na msanii Isabela Mpanda ambaye naye alikuwa kachangamka ile mbaya
Isabela alikuwa kituko zaidi kufuatia kuvaa kinguo kifupi cha pinki kilichoacha sehemu kubwa ya mwili wake, hasa kuanzia mapajani kuwa wazi.
Msanii huyo pamoja na kujitupa huku na huko kilevi na kucheza muziki kwa kukata nyonga kinoma, alikuwa akiinua nguo yake juu na kuonesha kufuli lake ‘white’ na kujishika sehemu za nyuma jambo lililomfanya mmoja wa wahudhuriaji kusema
Jamani pombe ni noma, mnaona mambo ya aibu anayoyafanya Isabela?”
Kituko kingine ni pale mastaa hao waliokuwa bwii kwa kilevi akiwemo Mwamanda, walipoamua kummwagia pombe kichwani na kwenye nguo zake Baby Madaha baada ya kumuimbia wimbo wa ‘Happy birth day to you

                 BABY MADAHA BILA MAKE UP



JAMANI NIMEZIANGALIA HIZI PICHA SIKUMGUNDUA BABY MADAHA MARA NYINGI NAMUONA AKIWA NA MAKE UP LEO KAWA TOFAUTI KABISA BILA MAKE UP.

WEMA NA DIAMOND WAHAMISHIA MOVIE YAO UGANDA MWEZI UJAO

 WEMA SEPETU AKIWA NA MPENZI WAKE WA MILELE DIAMOND PLATNUMZ
 
Hivi  majuzi habari zilienea kwamba mwanamziki ambaye ni mchumba wa muigizaji Wema Sepetu alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamama wa Uganda anayeitwa Zari , basi bwana, huyo Zari ameandaa party aliyoipa jina la CYROC WHITE PARTY, party hiyo itafanyika Dec 18 ambapo inasemekana mwanamziki wetu expensive Bongo nzima DIAMOND PLATNUMZ atahudhuria party hiyo. Wema nae kaamua kujibu mapigo, siku hiyo hiyo ya Dec 18 mwanamziki nguli wa Uganda JOSE CHAMELEON na yeye atafanya show ya kufunga mwaka ambapo kiingilio ni million moja ya Uganda WEMA SEPETU atakuwa ndani ya nyumba, basi jana Wema kupitia mtandao wake wa instagram aliwaharifu mashabiki wake kwamba atakuwepo Uganda kwenye show ya JOSE siku ya tarehe 18 muda mchache na Diamond nae akatoa tangazo la kuwaarifu mashabiki wake juu ya party ya Zari siku ya tarehe 18. mashabiki wengi walionekana kufurahishwa na haka kaushindani ka wapendanao hao ambao ni wazi wanakomoana tu ila mwisho wa siku wanapendana mpaka shetani anaogopa, sasa watu wanasubiri jinsi Uganda itakavyozizima, kwasababu ni wazi kwenda kwa Wema Uganda ni kwa ajili ya kumkomoa Diamond tu hivyo hivyo na kwa Diamond pia, ZARI NI MWANAMAMA MWENYE PESA NDEFU NA JOSE CHAMELEON NI MWANAMZIKI MWENYE PESA NDEFU AFRICA MASHARIKI NZIMA,

JOSE CHAMELEON WA UGANDA
 
ZARI
 
WEMA NA DIAMOND WAKIGOMBANA SHIKA JEMBE UKALIME WAKIPATANA BEBA KAPU UKAVUNE, UKIINGILIA UTAPATA AIBU MJINI .

DIAMOND PLATNUMZ AWAKALISHA PSQUARE WA NIGERIA..........AFRICA NZIMA HIVI SASA HABAREE YA MJINI NI MOND BIN LADEN



Ma meeeeeen Diamond Platnumz anazidi ku SHINE Africa baada ya video yake mpya ya NTAMPATA WAPI kupata viewers wengi mno kupita video ya wanamziki wa Nigeria PSQUARE, cha kushangaza ni kwamba Psquare walianza wenyewe kutoa video yao ya wimbo wa SHAKIN siku ya tarehe 17 Nov, baada ya siku tatu yani tarehe 20 Diamond nae akadondosha yake ya ntampata wapi, eh kilichotokea bwana ni watu kususia video ya Psquare na kushadadia video ya Diamond, wengi tunajua wanigeria wako wengi sana na wanasurpotiana kinomi nomi lakini safari hii naona wameamua kumsurpot mtanzania Diamond, huku kwenye mitandao yake pia Diamond akiwa anazidi kuongeza mafollowers wa kumwaga.

mpaka sasa kwenye instagram DIAMOND ANAFOLLOWERS MILLION 3 WAKATI MPINZANI WAKE MKUBWA ALI KIBA AKIWA NA FOLLOWERS 81274 TU,

 

MANGE KIMAMBI LE BIG BOSS U KNOW.....

MCHEKI MANGE KIMAMBI AKIWA OFISINI KWAKE MASAKI.
Nimeipenda sana mandhari ya ofisi yake,
 
 
 
 
HONGERA SANA MANGE KIMAMBI MWANAMKE MPIGANAJI, WE NI MFANO WA KUIGWA HUWA NAWAZA HATA KAMA UNAPATA MUDA WA KULALA,

CHEKI JIBU ALILOLITOA MWANAMAMA ZARI JUU YA MAHUSIANO YAKE YA KIMAPENZI NA MWANAMZIKI DIAMOND


Mwanamama wa Uganda aliyetuhumiwa kuwa na mahusiano na mwanamziki wetu bei mbaya DIAMOND PLATNUMZ amekanusha kwamba wapo kwenye mahusiano na Diamond ila amesema wakati wanafanya LE PROJECT  walisambaziana upendo kidogo .

HAPA WAKISAMBAZIANA UPENDO ZARI NA DIAMOND BIN LADEN.




HAYA NI MAJIBU YA ZARI HAPO CHINI

Friday, November 21, 2014

MUIGIZAJI BATULI KUMTAMBULISHA MUMEWE MTARAJIWA DECEMBER TANO...






Inasemekana kwamba muigizaji mwenye mvuto wa ajabu asiye na makeke Batuli yupo mbioni kufunga ndoa, Batuli ambaye ni mama wa watoto wawili amesema kwamba ameshajifunza mambo mengi kwenye maisha hivyo hivi sasa ni wakati wa yeye kutulia na kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi wanayependana sana, Batuli hajamuweka wazi mpenzi huyo ila ameahidi ya kwamba tarehe 5 December ndio itakuwa siku rasmi ya kumtambulisha mpenzi wake huyo ili watu wamjue.

RAY KIGOSI ALINADI UPYA PENZI LAKE NA CHUCHU HANS






Muigizaji handsome na expensive Ray Kigosi ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi hisia zake kwa mpenzi wake wa sasa ambaye pia ni muigizaji CHUCHU HANS, Ray ambaye hapo mwanzo alikuwa hana utaratibu wa kutangaza wapenzi wake hadharani alisema........


 licha ya kupitia katika changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.
“Chuchu ndiye kila kitu kwangu, tunaendana kwa kila kitu hivyo nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe,” alisema Ray.Ray kabla ya kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ na Blandina Chagula ‘Johari’

Thursday, November 20, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AVUNJA RECORD AFRICA MASHARIKI NZIMA..... INGIA USOME

Diamond & Wema_Sepetu


Siku ya jana, mwanamziki Diamond aliachia ngoma yake inayoitwa NTAMPATA WAPI... ngoma hiyo ambayo kwa wanaofahamu uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na Wema ni wazi utajua kwamba huu wimbo kaimbiwa Wema, basi bwana, jana Diamond alivyouachia rasmi wimbo huo unaambiwa NDANI YA MASAA MACHACHE WIMBO HUO ULIPATA VIEWERS ELF 50 UTUBE KITU AMBACHO HAKIJAWAHI KUTOKEA KWA MWANAMZIKI YEYOTE HAPA EAST AFRICA, licha ya huko kwenye utube, mji mzima ulikuwa unamzungumzia Diamond siku ya jana, simu zilikuwa busy watu wanaombana kutumiana wimbo wa Diamond kwenye ma wats up, watu walikuwa busy kusikiliza radio na kuangalia tv kwani wimbo huo ULIGEUKA WIMBO WA TAIFA KWA SIKU YA JANA maana ulipigwa kila kona, hii inamfanya DIAMOND kuwa mwanamziki asiye na mpinzani Tanzania, na KWA KAULI YAKE DIAMOND KABLA HAJAUTOA WIMBO HUO ALISEMA HUU KAUTOA TU LAKINI WIMBO HASWA ULIOPANGWA KUTOLEWA PIA UNAKUJA KABLA YA MWAKA KUISHA,



MASHAHIRI YA WIMBO WA NTAMPATA WAPI.....
Sura yake mtaratibu, mwenye macho ya aibu
msahau mnajarib, ila namkumbuka sanaa
umbo lake mahbibu ,kwenye maradhi alonitibu
siri yangu mnaharibu , bado namkumbuka sanaaa,
alonifanya nisilale,jua kali ntafute tukale
lakini hata kujali darling, akatekwa na walee,

NTAMPATA WAPI kama yule niliyempendaga sana
NTAMPATA WAPI kama yule alonipenda sana.


MANENO YALIYOWAVUTIA SANA WATU NI HAYA HAPA
hii ni sauti ya rais
iliyomshinda ibilis
kwa mwanadam sio rahis

kamwambie lazima wajue kutofautisha KATI YA ALAMA YA MSALABA NA JUMLISHA,NA KUNA X NA KUZIDISHA.




NI HAYO TU WAPENZI MPAKA KESHO AU BAADAE NI MIMI RACHEL KAYUNI WA TANZANITEMOVIES..BYEEE

MPENZI MPYA WA DIAMOND ...ZARI THE BOSSLADY ATOA MPYA YA MWAKA.


Huyo hapo juu ni Zari mpenzi mpya wa mwanamziki classic DIAMOND PLATNUMZ, jana alitoa mpya ya mwaka baada ya kuzifollow account zinazomtukanaga Wema Sepetu huko instagram, ila hiyo haishangazi kwasababu anahaki ya kufollow mtu yoyote anayemtaka, KILICHOCHEKESHA WATU NI KWAMBA HUYU MREMBO ETI AMESHAKARIRIWA MARA NYINGI AKISEMA YEYE HAJUI KISWAHILI, NA HATA WATU WAKE HUWA WANASEMA HUYU HAJUI KISWAHILI KWA HIYO WALE TEAM WEMA HATA WAKIMTUKANA WANAPOTEZA MUDA WAO TU KWANI HAELEWI, SASA JANA WANASHANGAA MREMBO ANAZIFOLLOW ACCOUNT ZA KUMCHAMBA WEMA KWA HIYO KUMBE KISWAHILI KINAPANDA SANA TENA HADI MATUSI YA KISWAZI YANAPANDA MAANA HIZO ACCOUNT HAPO CHINI HUWA ZINACHAMBA HASWA KWA MANENO YA KIBONGO . (ila pengine hajui Kiswahili anaweza akaajili mkarimani wa kumtafsilia hiyo michambo ambayo Wema anachambwaga kwenye hizo account)




 HIZI NDO ACCOUNT ZARI ANAZOZIFOLLOW AMBAZO ZINADILIGI NA KUMCHAMBA WEMA SANA.
 

ZARI AZIDI KUDATA NA PENZI LA DIAMOND PLATNUMZ













EHHH, Basi bwana si mnajua kwamba hivi sasa mwanamziki expensive bongo nzima mr Diamond Platnumz anamsambazia upendo mwanadada wa Uganda anayeitwa ZARI, sasa katika pita pita zangu jana niliona Zari kapost tangazo la kuhimiza watu wampigie kura Diamond kwenye tuzo za chanell o zitakazofanyika hivi karibuni.




HAYA NA SISI TUUNGANE NA ZARI KUMPIGIA KURA OUR SUPER STAR DIAMOND ILI ASHINDE KWENYE TUZO HIZO, NA MWISHO WA SIKU WARUDIANE NA WEMA WETU MAANA NDIO WANAPENDEZEANA.

Wednesday, November 19, 2014

WEMA SEPETU ATOA YA MOYONI.... NI KISA KIKUU CHA YEYE KUMWAGA DIAMOND SUKARI YA WAREMBO




MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.
Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.
SAFARI YAKE CHINA NAYO TATIZO
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake,
Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi
MWISHO WA LIKIZO
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28  kama ilivyo
kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.
AMZUNGUMZIA ZARI
Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
“Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi,” alisema Wema
MWISHO WA LIKIZO
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28  kama ilivyo
kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.
AMZUNGUMZIA ZARI
Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.
DIAMOND AULIZWA KAMA ANAITAMBUA LIKIZO NDEFU
Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.
“Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka kwa ishara ya furaha akijiandaa kuachia ngoma kali mpya iitwayo ‘Nitampata Wapi’ leo
KWENYE WHATSAPP
Wakati Diamond akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”
Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena






SOMA HABARI KUHUSU KESI INAYOMUHUSU MSANII LULU MICHAEL












KESI ya kuua bila kukusudia inayomkabili mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imewekwa kiporo kufuatia kuwepo kwa kesi nyingi za mauaji mahakamani, Risasi Mchanganyiko limetonywa


Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa wa kesi hiyo kusikilizwa tena Februari mwakani kutokana na mlolongo mkubwa wa kesi za mauaji zilizopo Mahakama Kuu ya Tanzania.
Chanzo hicho ambacho kipo ndani ya kamati ya majaji wanaoshughulikia kesi hiyo, kimenyetisha kuwa kesi ya Lulu itakuwa ngumu kusikilizwa wakati huu kwani mbali na wingi wa kesi mahakamani hapo, lakini pia majaji na mawakili watakwenda likizo.
“Ujue kesi ya Lulu ilikuwa miongoni mwa ambazo zingesomwa kabla ya mwaka huu kuisha, ila kulingana na vikao vya majaji inaonyesha wazi kabisa mwaka huu itakuwa ngumu hata Januari haitawezekana kwani wana kesi kama tatu za mauaji na baada ya hapo watakwenda likizo sambamba na mawakili kwani nao ndiyo kipindi chao cha likizo,” kilisema chanzo chetu.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, Aprili 7, 2012  maeneo ya Vatican-Sinza jijini Dar.Kifo cha Kanumba kilichotokea nyumbani kwake, kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa ambapo alipata mtikisiko wa ubongo kisha kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar

Tuesday, November 18, 2014

MUIGIZAJI LUCY KOMBA AMCHARUKIA FLORA LYMO MBUTA NANGA..



                  LUCY KOMBA NA MUMEWE.


Muigizaji Lucy komba jana alimchachamaria mwanamama Flora Lymo kwenye page ya instagram ya team ukweli na uwazi, kisa kikiwa ni kwamba Flora aliwahi kumkashifu Lucy juu ya harusi yake na mavazi yake, basi jana topic ikiwa ni juu ya ule ugomvi ulioshika chati hivi sasa wa Mange Kimambi na Flora Lyimo, muigizaji Lucy alionekana akifurahia jinsi Mange alivyomchamba Flora, na kusema ni afadhari Flora ameshikishwa adabu kwasababu yeye alikuwa akimsakama sana alipofungaga ndoa na mumewe tena bila sababu yoyote.




Mwigizaji mkongwe nchini Lucy Komba afunga ndoa. Tazama picha za harusi


                                                          FLORA LYMO MBUTA NANGA






MANGE KIMAMBI NA FLORA LYMO MBUTA NANGA WAKINUKISHA KINOMA NOMA

 HUYU NI FLORA LYMO MBUTA NANGA WA LONDON

MANGE KIMAMBI NA MUMEWE WAKO MAREKANI
Picha za Man ..


Hawa warembo wawili wote ni wajasiriamali wanaoishi nje ya nchi, wanatoka Kilimanjaro wote ila wamekinukisha balaa huko kwenye mitandao kisa kikiwa ni FROLA kuanza kumshambulia Mange kwenye maoni aliyotoa juu ya mwanamziki Diamond kutembea na sugarmamy Zari. basi hivi sasa kama unataka kuondoa stress ni unapitia tu kwenye blog za hawa wawili unacheka maana kama Mange yeye ni anatoa maneno ya kuchekesha mno, yani yeye hatukani ila ni maneno tu ya mzaha, anyway TUNAWAOMBEA WAYAMALIZE .

Monday, November 17, 2014

MUIGIZAJI LULU MICHAEL TUNAKUPA HONGERA ZAKO





Juzi  nimeangali movie mpya ya Lulu ya MAPENZI YA MUNGU, yani kwanza kabisa Lulu jamani ni muigizaji mzuri mno, yani anajua kuuvaa uhusika hasa, yani nilifurahishwa mno na jinsi alivyocheza ile movie, mi sio shabiki sana wa Lulu lakini kwenye hii movie Lulu ameshanidaka nimekuwa shabiki wake hasa, na hivi ndo msanii anavyotakiwa awe, WATEKE MASHABIKI ZAKO KUPITIA KAZI ZAKO , yani msanii anapofanya kazi ikamfanya shabiki ampende hapo ndo kazi ya msanii inakuwa imepokelewa,
LICHA YA KUIGIZA SIKUJUA KWAMBA LULU UNASAUTI YA KUIMBA KIASI HIKI JAMANI, yani kwenye ile movie Lulu kaimba kwa sauti nzuri mno kupita hata wanamziki wengine,
MAMA KANUMBA; kwa upande wa mama Kanumba nilipenda alivyocheza na pia nimefurahi kumuona kwenye movie ila anahitaji kuzoea camera kidogo.


LINA; mwanamziki Lina nae amejitahidi japo nayeye anahitaji kujifua zaidi


yule aliyecheza kama mchungaji nilimpenda sana na yeye alicheza vizuri mno kwakweli,

MTANGAZAJI WA BONGO MOVIES JOYCE KIRIA AKWAA SKENDO YA UTAPELI...




WHY Joyce? Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria yupo kwenye wakati mgumu baada ya kukwaa skendo ya utapeli kwa marafiki zake (majina yanahifadhiwa kwa sasa) akidaiwa kuwashawishi kuingia kwenye biashara ya Mtandao ya Telexfree Network Marketing
Kwa mujibu wa sosi makini, ishu hiyo imeibuka juzikati ambapo Joyce alikuwa akishushiwa zigo la lawama na marafiki zake hao huku baadhi wakitishia kumshitaki kwa kuwatapeli kwani wamepoteza fedha nyingi kwenye mpango huo wakidai hawajaona chochote
Dada Joyce aliwashawishi marafiki zake wengi, wakaingia na kila watu walipomshtua na kumwambia kuwa ni utapeli mtupu alikuwa akiwatolea lugha za kuudhi. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Joyce na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: “Ni kweli niliwashawishi marafiki zangu kwa sababu nilijua biashara hiyo inalipa na hata mimi nimeumia sana kuona imekufa kwani sikupenda.
“Nimepoteza fedha nyingi. Ilikuwa ni kama desi ilivyokufa, hakuna wa kulaumiwa.”
Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.
Telexfree Network Marketing ni kampuni iliyokuwa ikijihusisha na biashara ya mtandao ambapo mhusika hutoa kiasi cha fedha huku akiunganisha watu wengine ambapo kipato chake kwa maana ya faida itaongezeka mara kwa mara kwa kadiri anavyounganisha watu wengi

NIMEWAMISS MNO............RACHEL KAYUNI TANZANITEMOVIES BLOGGER



Nisameheni wapendwa nilikuwa busy kidogo na majukumu ya hapa na pale nikashindwa kublog,nashukuru sana kwa wale waliotumia muda wao kunitumia msg na kunipigia simu kuniuliza kulikoni niko kimya. nimerudi make tayari kupokea ma habari ya movie toka dunia nzima na mapicha ya haja.

Monday, November 10, 2014

SUGAR MAMY WA DIAMOND PLATNUMZ, ZARI AMETUPIA PICHA YA MWANAE MTANDAONI NA KUSEMA MWANAE ANAFANANA SURA NA DIAMOND EMBU INGIA UIONE HIYO PICHA


 HAPO JUU ZARI THE SUGAR MAMY AKIWA KWENYE GARI LAKE LILIOANDIKWA ZARI kwenye plate number, ( Diamond ndo anakaa kwa huyo motto hivi sasa jamani acheeni Diamond aitwe Diamond yani anavyojipendelea warembo ) ila safari hii Diamond kaongeza na jina jipya embu ngoja nikutajie majina ya Diamond yote, kuna DIAMOND, PLATNUMZ,CHIBU,DANGOTE,SUKARI YA WAREMBO, MONDBINLADEEN, na sasa hivi hili jipya ni DIAMOND THE SERENGETI BOY.....





                                                    MTOTO WA ZARI
 
Huo ujumbe wa hapo kwenye picha ni kutoka kwa sugar mamy wa Diamond bibie Zari ambapo amesema kwamba mwanae anafanana na Diamond sura na style ya nywele zake,
 
ZARI NA SERENGETI BOY WAKE DIAMOND WAMEANZISHA MAPENZI SIKU MBILI HIZI LAKINI INAONEKANA ZARI KAKOLEA KINOMA NOMA MPAKA KAANZA KUONA MWANAE ANAE ANAFANANA NA DIAMOND WAKATI SIKU ZA NYUMA WAKATI HAWANA UHUSIANO HAKULITAMBUA HILO.
 
 

Sunday, November 9, 2014

TANGAZO KUTOKA LE MUTUZ SUPER NATION U KNOW.. KUHUSU THE SUPER STAR DIAMOND PLATNUMZ NA MPENZI WAKE MPYA

Le Mutuz


Le mutuz kama mnavyomjua huwa anaijua sana kazi yake ya uwana habari, sasa basi, jana usiku ametoa tangazo kwamba leo SAA NANE MCHANA KUPITIA INSTAGRAM PAGE YAKE ATATUMEGEA UBUYU WOTE KUHUSU MAPENZI YA DIAMOND NA MPENZI WAKE MPYA ZARI THE BOSS LADY, NA PIA ATATOA PICHA EXCLUSIVE 50 ZA DIAMOND NA ZARI.



 

KABAAAANG........ HABARI YA MUJINI HIVI SASA NI DIAMOND PLATNUMZ KUANZISHA MAPENZI NA MWANADADA MILLIONARE WA UGANDA ANAYEITWA ZARI .....INGIA UONE MAPICHA YA KIMALOVEY DOVEY

Le Mutuz
 
 


Week end yote kulikuwa hakuna habari yoyote iliyosikilizwa mji huu yani hata wangeambiwa OSAMA kafufuka watu wasingesikiliza kisa kikiwa ni macho na masikio yote kuwa kwa DIAMOND PLATNUMZ..... juzi kati Diamond sukari ya warembo alikuwa akitokea south Africa, basi kwa bahati mbaya au nzuri akakaa siti moja na mdada tajiri wa Uganda anayeitwa Zari ambaye zamani alikuwaga mwanamziki, basi Diamond na Zari wakapiga mapicha wakiwa kwenye ndege na kusema wamekutana hapo, eh mambo si yakawa mambo, unaambiwa naona wakaachiana ma namba ya simu na mazagazaga yote , basi baada ya kutua bongo si wakaanza kuonekana viwanja mbalimbali usiku kwa mchana wakila raha kama vile duniani wako peke yao yani, basi unaambiwa walipiga mapicha ya kimahaba ile mbaya, na zari kuna baadhi ya picha akitupia kwenye instagram anasema kabisa ASANTE DARLING KWA KUNIPIGA PICHA yani ilimradi tu kuchangamsha genge, kama unavyojua DIAMOND ni wa Wema hata aende wapi ,,,,, huko tayari account fake zimeshafunguliwa instagram kwa ajili ya kumtukana huyu ZARI,          nisikuchoshe hebu shuka chini utazame picha......
                                             HUYU NDIO ZARI THE BOSSLADY
 
ZARI alishaolewa ila hivi sasa wametengana na mumewe, na nasemekana ana umri wa miaka 35 wakati Diamond anamiaka 26, pia Zari anawatoto wa tatu wakiume wakubwa wa kwanza anamiaka 17 ila Diamond hana motto kabisa.....
 
ZARI
 
ZARI AKIWA NA KOFIA YA DIAMOND
 
ZARI AKIWA NA SUKARI YA WAREMBO INAYOENDAGA KUCHOVYA ILA MWISHO WA SIKU LAZIMA IRUDI MAKAO MAKUU KWA WEMA SEPETU
 
SINA CHA KUSEMA NAKUACHIA WEWE
                                          MAHABA NIGALAGAZE
MAHABA NILIPUE KAMA BOKO HARAM
MAHABA NIUE KAMA EBOLA
MAHABA MAHABANI ZARI NA SERENGETI BOY WAKE
 
EHHHHHH. HAPO NI ZARI NA SERENGETI DIAMOND NA LE BIG SHOW LEMUTUZ NATION U KNOW

Le mutuz ndo mzee wa hitifaki yani kitu kikitokea tu mjini unamuachia yeye atakifwatilia mpaka mwisho wake, asante Lemutuz kwa kuwa mwanahabari sharp, na picha hizi pia nimezipata kwa LE BIG SHOW LE MUTUZ NATION, kwa ambao hawamjui Lemtuz huyu ni motto wa muheshimiwa MALECHELA, yeye ni king of all social media Bongo yani ndo anavyojiita ,,,,     mi NAPENDA KUMUITA MZEE WA KUNIONDOA STRESS MAANA KILA NINAPOINGIA KWENYE PAGE YAKE INSTAGRAM BASI STRESS ZOTE LAZIMA ZINIONDOKE, NA NIKIPITIA NA KWA SHANGAZI YAKE MATIKIBOKO YAO BASI NDO KABISA HATA NIWE NIMEUZIWA VIPI LAZIMA NISAMEHE, KIFUPI NI KWAMBA LE MUTUZ KAZI NZURI SANA UNAIFANYA BONGO WE LOVE U, NA SHANGAZI YAKE MATIKIBOKO YAO NAKUPENDAJE SASA NA WEWE,