Wednesday, July 16, 2014

PENNY NA WEMA SEPETU MAMBO SAFI SASA HIVI






STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema baada ya kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’, sasa ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani





Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema alisema: “Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu.”

Kwa upande wa Penny alifunguka: “Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’




KWA NINAVYOONA MIMI WEMA AMEFANYA SAHIHI KUWEKEANA VINYONGO NA WATU VINAONDOA KUPATA BARAKA KWA MUNGU, pia Wema anakila sababu ya kusamehe kwasababu kama Diamond tayari ni wake, wakwe tayari wako upande wake, yani kila alichokua kakipoteza kimerudi, kwa upande wa Penny, PENNY NI BINTI ANAYEJIELEWA, PIA KAMA WEMA ALIVYO NA YEYE HUWA SI MTU WA MANENO MANENO, KWA HIYO NAIMANI NA YEYE ANAJUA ALIKOSEA NA NAIMANI ATAKUA AMEKUBALI MATOKEO NA ANAENDELEA NA MAISHA YAKE,

No comments: