Saturday, July 5, 2014

MAMA WEMA KUSEMA ALBADILI .....


                           





Baada ya kumkosa Wema, Risasi Jumamosi lilimtafuta mama yake, naye kwa njia ya simu na alipopatikana aliombwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo.
KUHUSU ALBADILIAkizungumza kwa hasira huku sauti yake ikionesha dalili kwamba bado hayuko sawa, mama Wema alisema:
“Ni kweli, nimeshapanga kufanya hivyo, nitasoma Albadili. Haiwezekani watu wakae na kuamua kunichafua mimi, nimewakosea nini cha mno mpaka kufikia kufanya vile! Siwezi kukubali hata kidogo.”
KUHUSU MASHEHE
“Ni kweli pia, nimeshawasiliana na mashehe. Wao wako tayari wanachosubiri ni kupita kwa siku ambazo nimetoa. Kama hakuna atakayejitokeza kuomba radhi, kisomo cha Albadili kitasomwa, wataanza kupukutika mmoja baada ya mwingine kweli nasema.”
SIKU SABA ZINAANZA LINI?
“Jumamosi ijayo (leo) itakuwa siku ya kwanza. Kwa hiyo mpaka Ijumaa ya Julai 11 (mwaka huu), itakuwa siku ya mwisho.”
NENO LAKE KWA WAHUSIKA
“Nawaambia wale wote wanaojijua walihusika na ile picha ya uongo, ya kutumbukiza kichwa changu kwenye picha nyingine na wale waliohusika kuitupia kwenye mitandao, waje waniombe radhi kabla siku saba hazijaisha, sitanii jamani.”
UKWELI WAKE
“Mimi ni Muislamu safi, nasema sijawahi kupiga picha za namna hiyo katika maisha yangu tangu nizaliwe mpaka utu uzima wangu huu na wala sijawahi kufikiria.”
KUMBUKUMBU YA WEMA
Katika Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Toleo la Juni 25, mwaka huu, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; Wema azimia!


Habari ile ilimhusu Wema kupoteza fahamu kufuatia kuiona picha hiyo kwenye mitandao akidai ililenga kumchafulia mama yake jina.
KILIO KWA TCRA
Kumekuwa na wimbi la watu  kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu, pia wanafunzi wa vyuo wamekuwa waathirika wakubwa.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliowahi kuzungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walitoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa picha chafu mitandaon

No comments: