Friday, July 11, 2014

KUHUSU MASWALI YA ZAMARADI MKETEMA WE UNAONAJE?


                                        ZAMARADI MKETEMA
Zamaradi naweza kusema ndo mtangazi pekee mwenye kipindi cha BONGO MOVIES kinachopendwa nchini, ukiniuliza vipindi vingine vinavyohusu movies hapa Bongo sivijui huwa nakijua take one tu cha Zamaradi, leo alikua akimuhoji mama yakee Diamond, ambapo katika kumuuliza maswali mama wa watu ilibidi amwambie Zama unanikwaza sana na maswali yako, JE? WEWE UNAONAJE MDAU? maswali ya Zama yalikuwaje?


MIMI KWA MAONO YANGU NI KWAMBA, ZAMA HANA MASWALI MAGUMU AU MABAYA, TATIZO NI KWAMBA ANATAKIWA AWE ANAANGALIA ANAMUHOJI NANI. mfano kama unamuhoji Wema sio sawa na utakavyomuhoji Mwamvita Makamba, kama unamuhoji mama Diamond sio sawa na utakavyomuhoji RITA PALSEN,


MAMA DIAMOND, ni mama ambaye hakufight ili awe maarufu, wala hakutarajia siku moja atakuja kuwa maarufu, hana kazi inayomfanya awe kwenye media na pia hakuzoea kabisa hayo mambo, imetokea tu mwanae anakipaji kawa maarufu sasa watu wanataka kumuhoji na mama mtu pia, kwa hyo ni wazi hana uzoefu wa kuongea kwenye media, ni wazi hana uzoefu na maswali ya waandishi wa habari, kwa hyo pale Zama alitakiwa ajishushe kidogo na kumuhoji kama mama yeyote wa kawaida wa kitanzania, kama wakina Gea walivyokua wanafanya, yani huwezi kua serious na kumtaka mama Diamond ajibu maswali kama yale ni wazi atashindwa hajazoea, hata ulaya mpaka wasanii wengine wanafundishwa jinsi ya kuongea kwenye media ndo wanaweza kwa hiyo kwa mama Diamond kwa kweli zama ulimuuliza maswali ya kiufundi mno, MASWALI YAKO NILIYAPENDA SANA LAKINI NILIJUA KWA MAMA WA KAWAIDA WA KITANZANIA LAZIMA YAMSHINDE, HATA ANGEKUA MAMA YANGU ANGECHEMKA,





5 comments:

Anonymous said...

Yani Rachel mi Zamaradi ananiudhi kitu kimoja tu, kujibadilisha sauti, yani sijui anamuiga nani jamani, kwenye tv sauti nyingine na akiwa kwenye radio mikogo pia inabadilika, aache hiyo tabia

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

MH ILA MAMA DIAMOND ANANOGA KUMSIKILIZA JAMANI, MUNGU AZIDI KUMBARIKI

Anonymous said...

Wema kafutulisha nyumbani kwake Mbona utuletei habari na picha?au hujui Kama kafutulisha nyumbani kwake?