Yani nimekua nikifuatilia mitandao mbalimbali naona wengi wanaongelea hili swala la kuachana kwa Dida na Ezden, lakini kinachoniumiza ni kwamba wengi wanaacha kuongelea mapungufu yaliyoonekana kwa wawili hao na badala yake wanampiga vijembe EZDEN kwamba hana hela, mara marioo, mara alikua analelewa,
HIVI JAMANI EMBU NIWAULIZE, hivi huyu kijana atakuwaje marioo wakati nikijana mwenye kazi yake, anapokea mshahara kila mwisho wa mwezi, Dida mwenyewe alimkuta huyu kijana akiwa na kazi yake, na zaidi ya kazi pia ni mjasiria mali, mi nadhani marioo ni mwanaume asiyetaka kujishughulisha, kazi yake kula bata na kutazama tv tuu na kulishwa, lakini Ezden kila mtu anajua kwamba huyu kijana anajitahidi sana kupigana na maisha, au kosa lake lilikua kuoa mwanamke mwenye kipato kikubwa zaidi yake? SASA KWA KIJANA mwenye umri wa miaka chini ya 30, kamaliza chuo katafuta kazi sasa kaanza kupiga kazi mnataka awe tajiri na amzidi Dida kipato over night? hivi leo MNGEMUONA EZDEN NA UMRI WAKE HUO MDOGO KAWA NA MIHELA GHAFLA SI MNGESEMA ANABEBA UNGA? WENGI MNGEMWITA PUNDA, Dida mwenyewe wengi tunajua ni chapakazi na anajituma sana kwenye biashara zake lakini kutokana na mafanikio yake ya haraka watu walinyanyua midomo kusema anabeba sembe, kumbe dada wa watu ni juhudi zake tu, sasa Dida alianza zamani ndo maana kafika hapo alipo kwa hyo Ezden kwa kua kiumri ni mdogo na yeye pia mkimpa miaka 5 atafika alipo Dida, labda angekua na kipaji kama Diamond au Hasheem ndo akipata hela haraka watu tusingeshangaa, lakini kwa umri wake mnataka awe na mihela kumzidi Dida jamani jamani sasa naamini jamii ndo inayowafanya vijana wadogo waamue kubeba sembe maana kama KIJANA ANAJIFANYIA KAZI NA BIASHARA YAKE HALALI KABISA MNACHEKA MNASEMA YEYE NI MARIOO SASA SI MNATAKA ABEBE SEMBE, wapo wanaomlaumu Dida kwa kuolewa na mwanaume asiye na pesa, hivi MTU AKIOLEWA NA MWENYE PESA HALAFU PESA ZA HUYO MUME ZIKAISHA GHAFLA MAANA MUNGU HUWA ANAFUNDISHA WATU HUMU DUNIANI SASA JE MKE UTAMUACHA MUME KISA PESA ZIMEISHA? HAKUNA MWENYE GUARANTEE YA KUA NA PESA MILELE, MUNGU SIO MJOMBA WA MTU MPAKA MTU UJIPE GUARANTEE KWAMBA UTAKUA NA PESA MILELE HIZI PESA HUWA ZINAISHA, mi nadhani wakati tunacomment na kuwalaumu au kuwacheka, tuwacheke vyoote lakini sio swala la kipato cha mtu kwani hata Dida alianzia chini ndo akawa hivyo na bado anasafari ndefu, tusifanye pesa iwe mbele ya mapenzi kweli pesa tamu lakini pia na utu tuwe tunathamini, mbona OPRAH ana mihela lakini hajawa girlfriend wa BILL GATE aliyemzidi, mpenzi wa OPRAH hana kipato kikubwa kama alichonacho OPRAH lakini wamedumu miaka 27,
MI NAWAPENDA WOTE DIDA NA EZDEN, NAJUA MAPENZI HAYATABIRIKI MFANO TUNAO WEMA NA DIAMOND WATU WALIWAINGILIA SASA HIVI WAMERUDIANA, HAWA PIA IPO SIKU WANAWEZA KURUDIANA TUKABAKI NA AIBU, SISI TUWAOMBEE HERI TU, NA HATA KAMA WATAENDELEA KUTENGANA BASI TUWAOMBEE WASAMEHEANE, WASIWE MAADUI, yani kwa kifupi tushike jembe tukalime, siku wakipata Dida akaanza kurusha picha wakiwa wawili basi tubebe mikapu tukavune zetu.
No comments:
Post a Comment