Tuesday, July 15, 2014

MASHABIKI WA WEMA SEPETU WAFUNGUKA.

















Kama mnavyoona hapo juu hizo picha ni za semina iliyofanyika kwenye ukumbi wa BOT iliyoandaliwa kwa aajili ya wasanii wote wa Tanzania ikiwa ni ahadi ya Rais wetu Kikwete wa kuwasaidia wasanii ili waweze kuinuka kisanii, muheshimiwa Rais aliamua kuwaitwa wadau wakubwa wa sanaa nchini Marekani ili waje wawape somo wasanii wetu jinsi ya kukua katika maswala ya Entertainment, na wadau hao ni TERRENCE J AMBAYE NI MTANGAZAJI WA E, SHAKA ZULU,PRODUCER DAVID BANNER NA RIVER SHELDON.


MASHABIKI wanahoji, ugeni mzito kama huo kwenye sanaa, wenye lengo la kuwanufaisha wasanii wote, kwanini Wema Sepetu hakwenda, maana kwenye picha Wema hajaonekana, wameonekana wakina Lulu Michael na wengine, wengi walitamani wamuone na Wema kwani kwa jinsi Wema alivyojuu angepikwa kidogo na hao wadau basi ni dhahiri kwamba Wema angeongezea mambo mengi sana matamu kwenye maisha yake ya kisanii, licha ya hilo wengi walishangazwa Diamond na Rommy jons kuwepo ambao huishi nyumba moja na Wema na Wema kubaki, shabiki mmoja ameuliza au Wema kaacha usanii kaamua kumpikia Diamond tu, wengi wangetamani kumwona Wema akiwa busy kama Diamond alivyo busy, yani kama Diamond kaenda kupiga show Marekani sio Wema akae nyumbani kumsubiri Diamond bali na yeye awe nchi nyingine anafanya ishu za movie, jina la Diamond likitajwa BET basi na la Wema litajwe E, mbona la Lupita linatajwa,


HAYO NI MANENO YA MASHABIKI WANAOMPENDA WEMA KWA DHATI WALIONITUMIA MSG WAKINITAKA NIANDIKE WAPENZI, SIO MANENO YANGU.

No comments: